Safari ya miaka 9 tangu kuacha kazi. Hamasa kwa vijana wenye maono makubwa

Sijui nisemeje ila ndugu, kwa umri wako. Acha kuwa na mawazo mwngi hivo. Embu pambana, maana hata muda wa story yako bado. Yaani usipoangalia kwa hivo. Miaka tisa ijayo. Utatupa story nyingine
Embu jitahidi kidogo kama una roho ya kupambana. Utaachwa tena.
 
Nina ndugu yangu ana ndoto kubwa hadi zinamletea magonjwa ya stress

Wakati mwingine kuwa na ndoto kubwa sana nako ni shida
Hata mimi hicho kimenigharimu sana kweny maisha yangu, lakin naamini nitakuwa tajiri mkubwa tu na wala sio kutaka Kufika level hizo za kina Mo Dewji au Bakhresa huko ni kujitafutia stress zisizo na muhimu kwanza maisha ya kuukimbiza utajiri yana changamoto kibao sana!!
 
Brother A. Upo kaka kitambo sana?
Mara ya mwisho tulionana PPF Towers mwaka 2010. Uko salama Mkuu?
Salama sana kaka Mkubwa. Sio kweli kwamba tuionana 2010, tulikutana Zenji Tamasha la Busara hope 2012 kama sio 2013. Nipo napambania kombe kaka, jiji kubwa hili.
 
Umeandika ukweli mtupu, katika kitu ambacho unaweza kulala tajiri na kesho ukaamka masikini unapiga debe ni biashara...
Katika miaka yangu mi5 ya upambanaji nimejifunza vitu vingi sana na nimefeli katika biashara kadhaa mpaka sas ndo nimetulia kwenye biashara moja hivi ambayo wengi wanaidharau isiyotumia akili nyingi wala mtaji mkubwa sana kuiendesha lakini kukutoa ni chap tu!!
 
Mkuu Chance ndoto naona umempa mleta mada za kichwa kwamba asije akaleta story nyingine baada ya miaka 9 ijayo. 😁😁
 
Haloo, huu uzi unasikitisha sana, acha kazi uone ilivyo kazi kupata kazi. Mkuu nakukumbusha tuu, hakuna tajiri anayefundisha au anayemiliki shule
 
Hadithi nzuri, naweza kuchangia yafuatayo :
1.Kabla ya kuacha kazi ungehakikisha tuition centre yako imesimama JAPO NI PAST ILA ITAKUWA FAIDA KWA WANAOFIKIRIA KUACHA KAZI

2.Hongera kuwa na maono japo unatakiwa kuwa karibu na wanaokuhamasisha! MO DEWJI au BAKHRESA ni juu Sana kwa sasa focus kwenye kufika 1M then 10M Then 100M hadi 1B na kuendelea

3.Usikatishwe Tamaa na mtu yeyote!
 
Tupe hayo madini mkuu, unataka kua tajiri kirahisi peke yako aisee
 
Upo kama mimi mkuu napiga kazi haswa na ninaamini pesa ninazipata na nitazipata zaidi ambazo hazina kikomo lakini sipo serious sana kuusaka japo nafata formula za utafutaji
 
Upo kama mimi mkuu napiga kazi haswa na ninaamini pesa ninazipata na nitazipata zaidi ambazo hazina kikomo lakini sipo serious sana kuusaka japo nafata formula za utafutaji
Mkuu maisha haya ni kma zile mbio za kupokezana kijiti nikimaanisha kuna wakat tu lazima utapungukiwa pumzi alafu ukiangalia hata nusu ya zile ndoto ulizokuwa nazo bado hazijatimia hapo ni umri ukishaenda.

Bottom line: Ni bora zaidi kuwa na ndoto zinazotekelezeka kuliko kuwaza mipango ya billioni moja wakat hata hujawahi shika milioni 50 yako.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…