Njoo hapa brother
Ivan Stepanov utoe neno
Mimi naona jamaa atafute shortcuts za NGO's. Kwa sababu kama ni mwalimu professionally, experience ya tution centre anayo, uwezo mkubwa wa kuandika lakini pia life experience kubwa
Nadhani angeanza kujichanganya kwenye NGO's kama volunteer kwa zile shule zenye mahitaji ili ajifunze wengine wanatengenezaje pesa kupitia foundations.
Lakini pia anaweza kujifunza kutengeneza propasals, machapisho ya kuombea grants and funds ambayo yanaweza mtengenezea stability kuliko hiyo pesa anayoingiza kwa sasa
Ukiachana na misoto ya mahusiano na kusomesha ndugu ambapo hataa Mimi nilikuwa na majukumu ya upande wangu lakini pia mimi sikuwa failure kwenye ajira za private sector maana nimeacha kazi zaidi ya mara tatu..
All I can say is, binadamu tunapambana kila siku lakini siku ya kufanikiwa ni moja hivyo, wengine wanachukua miezi na wengine wanachukua miaka lakini jambo la muhimu pia
Ni kuangalia angle zingine za kutafutia pesa kutokana na kipaji kama hicho cha kuandika au ualimu. Na hii huwezi kupata kama utakosa exposure au connections za kukufanya uingie kwenye milango flani ambayo 350k unayoitafuta kwa mwezi ni hela ya kupozea siku ya mtu..
So, story aliyoiandika imenikumbusha mengi sana na namuelewa anachopitia na pengine najua ana maumivu makubwa kuliko niliyopitia,
Lakini itakuwa vyema kama mkuu akijipatia healing na ayaache yaliyopita then aanze kuingia kwenye rooms za waliofanikiwa kama hizo nilizopendekeza ili aweze kufika anapotaka.