Safari ya Mlandizi mpaka Bagamoyo kwa miguu na tulivyonusurika kushambuliwa na Ngiri

yani nimegundua zamani ndo kulikua na stori ..maisha ya siku hizi sjui tutakuja kuwasimulia nini wajukuu wetu.. au tunawasimulia ya kina mwijaku na spiderman wa bongo?
Siku hizi stiry zipo za kiteknolojia mkuu! Utasimulia jinsi ulivyotapeliwa mtandaoni.
Ila zamani ndio kila kitu fikiria mnapanga safari kabisa mnajua hapa ni kuoiga mguu mwanzo mwisho kilomita za kutosha na mnapita maporoni kujutana na wanyama pori muda wowote tu.
 
Huyo wenyewe wanamuita ofsa mzee wa turbo chui ,simba wenyewe kumkamata mpaka timing.
 
Tuliamka asubuhi na mapema mimi, kaka yangu na dada angu tukaanza safari ya kutoka Mlandizi kwenda Bagamoto kwa miguu. Ikumbukwe wakati huo usafiri ulikua ni wa shida, hivyo suala la kutembea kwa miguu lilikuwa ni jambo la kawaida tu. Mpango wa safari yetu ulikua tutembee kutoka Mlandizi mpaka kijiji kimoja kinaitwa Yombo ambapo tungelala hapo Yombo kisha kesho ndio tungeanza safari ya kuelekea Bagamoyo.

Ilikuwa ni majira ya mvua za vuli na pia hali yangu haikuwa nzuri nulikua nasumbuliwa na macho hivyo uwezo wangu wa kuona mbali ulikua mdogo. Tulianza safari yetu vizuri kwa kupita barabara inayoenda Mbwawa na Miswe mpaka kufika jioni tukawa tumefika Yombo kwa hao ndugu zetu. Tukala na kupumzika pale ili kho tuanze safari ya kwenda Bagamoyo.

Ilipofika asunuhi tukaamka na kuanza safari ya kwenda Bagamoyo, tukapita vijiji kama Maimbwa na kuanza kuitafuta eneo linaitwa Magereza (Hapa kuna Gereza la Kilimo linaitwa Kigongoni). Na hili enoe ndio kuan kama pori hivi na hakuna nyumba karibu na unatemeba bila kukutan na nyumba kwa umbali mrefu. Sasa wakati tupo kwenye hilo pori la Mashamba ya Magereza kwa mbali kule tunapoelekea tukaona kama Ng’ombe na mwanae (Kumbuka hapo mvua inanyesha hivyo tukawa hatuwaoni vizuri) wanakuja usawa tunakoenda sasa. Kwa maana tulikuwa ni kama tunakutana kwa wao kuja tunapotoka sisi na sisi kwenda wanapotoka wao.

Muda si mrefu nyuma yetu ikawa inakuja gari Mitsubishi Pajero tukaipungia ili watupe lifti lakini ile gari haikusimama ikatupita tukaona sawa si tatizo. Wakati tunaendelea na safari na ile gari ikiendelea mbele. Ghafla tukaona imesimama Ghafla. Ikaanza kurudi nyuma kwa mwendo mkali , sisi tukawa hatuelewi nini kinaendelea. Kutahamaki gari imetufikia na ndani kulikuwa na watu watatu wababa hivi. Wakatuambia nyie watoto pandeni upesi ndani ya gari huku wakifungua mlango. Tukapanda ndani ya gari kwa haraka haraka. Na wakati tunaingia ndani ya gari nikitangulizwa mimi, kisha dada na kaka wa mwisho, ile kaka anaingia ndani ya gari na kufungwa milango Ngiri alikuwa tayai kashafika pale kwenye gari.

Gari ikaondoka na tunashukuru tukapelekwa mpaka tulipokuwa tunaenda kufikia. Kiukweli mpaka leo nikilikumbuka lile tukio mwili wangu unasisimka sana.
Nimetembea sana mitaa hiyo.
 
Ngiri tu unatetemeka,
Kweli watu wa pwani waoga
 
Ngiri na Nguruwe Pori ni vitu viwili tofauti!
Sidhani....nadhani ni huyo huyo mfano unaposema Mbogo na Nyati.

Kama una picha zao (Ngiri na Nguruwe pori ) unaweza kutuwekea.

images (2).jpeg

images (1).jpeg

download.jpg

tars download.jpeg

images (3).jpeg

download.jpeg
 
Maeneo hayo tumewinda Sana nguri tukiwa na vibali vya kuuwa wanyama waharibifu 2003 Hadi 2005 walikuwa wengi mno Ila mmmmh tulifaidi
 
Back
Top Bottom