Safari ya mwanza kibiashara!

nitazoea

Senior Member
Joined
Mar 15, 2017
Posts
195
Reaction score
237
Habari!

Natarajia kwenda jiji mwanza mwanzoni mwa mwezi wa nane kibiadhara,naomba kufahamu yafuatayo kutoka wenyeji na wakongwe wa jiji;
1. Biashara yeyote yenye faida kwa mtaji mdogo

2. Maeneo salama yenye nyumba nzuri za kupanga ndani ya jiji.

Ahsante,karibu kwa ushauri na maoni
 
binafsi nina miaka 2 sijakanyaga Mwanza.
1.Biashara ya dagaa ipo vzuri sana kama utapata masoko hasa nje ya Mwanza.

2. Biashara ya chakula pia ipo poa sana kama utaweza kupata wapishi wanaojuwa kupika vizuri.

3. Kwa nyumba siwezi kukushauri coz sijajua utapenda kuishi eneo gani na ubora wa nyumba unaotaka.. Ila wajuzi wenzangu waliopo huko watakupa mengine mapya ya sasa subiri wanakuja.

Yangu ni hayo sijajua kwa sasa pakoje huko.
 
Biashara ya dagaa saivi si nyepesi kiivo, imejaa vibali balaa
 
Karibu utatukuta mabaharia
 
Ukija ntafute kuna biashara zenye pesa nyingi sana lakini ndio zinakaribia kunitoa roho hakuna kukataa tamaa
 
Mkuu Mimi wiki ijayo nitaenda mwanza kwa ajili hiyo, nitakupa mrejesho
 
Ukija ntafute kuna biashara zenye pesa nyingi sana lakini ndio zinakaribia kunitoa roho hakuna kukataa tamaa
Mkuu kama hutajali toa somo la biashara hizo kwa faida ya wote au kama vp nichek pm. Wiki ijayo nakuja kuangalia biashara ya mtaj mdogo. Unaonekana ni mzoefu hapo. Tusaidiane mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…