Safari ya rais Uhuru, China yatia mkataba na kuifanya Kenya kuwa taifa la kwanza Afrika kuuza maparachichi China

Halafu ukitoa parachichi kutoka mbeya iringa kwenda kenya watazuia, yakioza wanafurahi kwa sababu lazima upige kura CCM
Mbona Wakenya wanachukua Iringa tena siku nyingi sana fuatilia
 
Serikali yetu suala la kutafuta masoko nje wako nyuma sana !

Ova

Wawezacho kwa bidii ni marufuku na makatazo we tazama kila siku ni habari ngumu ngumu za kubana watu,si habari za kutia matumaini. Mfano sie marufuku kutumia mifuko ya plastic, wenzetu wao wanatumia taka za plastic kama malighafi ya kuzalisha bidhaa zingine.
 
Same here parachichi nimeskia humu humu JF.......na tikiti maji pia

Vipi na matango, ila magimbi (nduma) na makande (githeri) ndio mtaani huwa naona zikiwapa shida wahudumu, inabidi nizitaje tu kama tulivyozoea.
 
Inatia huruma sana nchi hii ni kweli mkuu hadi leo wakulima wa mbaazi wameacha kulima zao hili
 
Mbona Wakenya wanachukua Iringa tena siku nyingi sana fuatilia
Wenzetu wakenya wanakuja kununua parachichi na machungwa kwa tsh 100 kila moja alafu wao wanaenda kuuza china na ulaya kwa dollar 5.....
Hapo mjanja ni mkenya tu
 
kwa akili zangu za usingizi ningetafuta wateja kenya ili wanunue maparachichi ya njombe,mbeya kilimanjaro na kwingineko afu sasa wale wakinunua na wakiuza uchina na mimi nakua nmeuza uchina indirect maparachichi yangu fursa inakua fursana
 
Nini maana ya Monopolized ?
Mbona hilo la parachichi tulishatangaziwa kuhusu masoko China isipokuwa kwetu biashara ya parachichi imekuwa monopolized na kampuni mbili,moja ipo Mbeya na nyingine ipo Kilimanjaro.

Sijajua kwanini imekuwa monopolized na hizo kampuni mbili?
 
Yule ni mfanyabiashara mkubwa kwa hiyo si ajabu. Sitaona ajabu ikiwa watakuja kununua kwetu halafu wa export kama zao la kenya. Inatakiwa wizara husika zizinduke bila kungoja amri.
 
Nakubaliana na wazo lako kiongozi
Yule ni mfanyabiashara mkubwa kwa hiyo si ajabu. Sitaona ajabu ikiwa watakuja kununua kwetu halafu wa export kama zao la kenya. Inatakiwa wizara husika zizinduke bila kungoja amri.
 
Hiyo ni akili kubwa sana
kwa akili zangu za usingizi ningetafuta wateja kenya ili wanunue maparachichi ya njombe,mbeya kilimanjaro na kwingineko afu sasa wale wakinunua na wakiuza uchina na mimi nakua nmeuza uchina indirect maparachichi yangu fursa inakua fursana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…