Safari ya rais Uhuru, China yatia mkataba na kuifanya Kenya kuwa taifa la kwanza Afrika kuuza maparachichi China

Safari ya rais Uhuru, China yatia mkataba na kuifanya Kenya kuwa taifa la kwanza Afrika kuuza maparachichi China

Malaika akiamka ameota ndoto ndiyo hiyo hiyo inatumika kama sheria
Wawezacho kwa bidii ni marufuku na makatazo we tazama kila siku ni habari ngumu ngumu za kubana watu,si habari za kutia matumaini. Mfano sie marufuku kutumia mifuko ya plastic, wenzetu wao wanatumia taka za plastic kama malighafi ya kuzalisha bidhaa zingine.
 
Hapa kwetu ni majungu tu na kuharibu tulichokwisha kizalisha
Huko China amekwenda seal hiyo deal la ku export avocados China......mambo ya sgr naona haikuwa kwenye kipaumbele kwenye safari hiyo
Wakulima na wafanyabiashara wa avacodos kenya watatusua maana China kuna consumers Karibia billion 1 na point

Tanzania sisi tutabakiaga kupiga kelele
Wahusika wamekaa tu na matai yao hawana habari kuwatufutia wananchi huku masoko ya bidhaa zao nje pamoja na kuwawezesha waweze uza bidhaa zao nje

Ova
 
Tuliambiwa tunasubiri ndege ya mizigo ndiyo tuanze ku export
Hakuna jipya hapo na tutabaki hivi hivi
Siku nikiona hata ndimu ya Tz kwenye soko la Ulaya ntapiga selfie
Ila sijivui nguo kama jamaa
 
Rais Uhuru wa Kenya leo amesaini makubaliano ya kuiuzia China mapalachichi yote yanayo zalishwa nchini humo na kuwa nchi ya kwanza barani Afrika kupata bahati hiyo.

Wakati sisi maparachichi yetu ya Njombe tunaambiwa yatapata kuuzwa baada ya kupata ndege ya mizigo.
Wa kwetu anafanya ziara eti ya kuzindua kiwanda mbeya cha maparachichi.
Badala ya kutafuta masoko yeye anazindua kiwanda cha maparachichi huko tukuyu.
 
Sisi wacha kwanza tupitishe sheria ya kuvidhibiti vyama vya upinzani hasa cdm na act
Mkutano kati ya Rais Kenyatta na mwenzake wa China Xi Jinping huwezesha Kenya nafasi ya kuuza parachichi kwenye soko la China
NA VICTOR ONYANGO
Rais Uhuru Kenyatta leo alikutana na mwenzake wa China Xi Jinping na kusisitiza umuhimu wa kuendeleza ushirikiana wa kufaidi upande zote.
Bwana Kenyatta alitoa shukrani yake kwa rais Xi juu ya mafanikio makubwa Jamhuri ya Watu wa China imetoa tangu mwanzilishi wake miaka 70 iliyopita, na zaidi ya watu million 700 waliondolewa katika umaskini hasa.
Rais wa Kenya alisema kuwa mpangilio wa ukanda na barabara huwezesha nchi tofauti kujenga uhusiano wa karibu wa biashara na ushirikiano, kupata utambuzi mkubwa kutoka kwa jumuiya ya kimataifa na kuunganisha gari na viwanda kwa nchi za Kiafrika.
“Kenya ina nia ya kuimarisha ushirikiano na China katika maeneo kama vile maendeleo ya miundombinu ya kukuza mpango zaidi kwa mikoa ya kati na magharibi mwa Afrika,” asema rais Kenyatta.
Rais Xi alieleza kuwa China ina nia ya kufanya kazi na Kenya ili kudumisha kasi nzuri ya ushirikiano katika maeneo mbalimbali kati ya nchi mbili na kati ya China na Afrika kwa kushirikiana kwa pamoja kwenye Ukanda Mmoja na Njia Moja.
Wakati wa mkutano huo, Kenya iliruhusiwa kuuza parachichi kwenye soko la China.
Baada ya kusaini makubaliano ambayo inaruhusu Kenya kuuza parachichi kwenye soko la China, makubaliano hayo yanaweka Kenya taifa la kwanza la Afrika kuhamisha China inayo solo la watumiaji zaidi ya bilioni 1.4 huja baada ya mchakato wa kibali mrefu na wa kina ambao ulijumuisha wataalam wa China kutembelea wakulima wa Kenya.
Inakadiriwa kuwa wakati mkataba utakapotumika kikamilifu, soko la Kichina litachukua zaidi ya asilimia 40 ya kuzalisha avocado ya Kenya, na kuifanya kuwa moja ya waagizaji wengi wa matunda.
Mkutano kati ya rais Kenyatta na Xi walenga lengo la kuendeleza uchanganuzi wa kiuchumi na biashara katika mipango 8 muhimu iliyotambuliwa wakati wa mkutano juu wa China-Afrika (FOCAC) uliofanyika Beijing mwaka jana. Mipango hii ni pamoja na kukuza viwanda, kuwezesha biashara, uunganishaji wa miundombinu, maendeleo ya kijani na kubadilishana watu kwa watu. Wengine ni kujenga uwezo, huduma za afya, na amani na usalama.
Rais Kenyatta yuko Beijing kwa ajili ya kuhudhuria kongamano la pili ya Ukanda mmoja, Njia moja ya ushirikiano wa kimataifa ambayo itafunguliwa rasmi kesho (Ijumaa) na rais Xi Jinping.
 
Huu uzi ni wa watu wastaarabu habari za matusi peleka kwenu huko mliko zoea kutukana watu na mwenzako chakubanga
Kwani wewe una tofauti gani na wale waliofanya mazishi ya kitaifa ya mbwa?
 
  • Thanks
Reactions: Oii
Sisi zaidi tunamudu mambo ya kipuuzi lakini kwenye makubwa tupo hoi.

Ukitaka kuondoa umaskini katika nchi ni lazima uwe na mbinu zinazowezesha pesa ya mataifa mengine kuja nchini mwako. Na kufanikisha hilo inahitajika werevu na sayansi ya biashara na uchumi. Kwa hilo sisi tupo nyuma sana.

Kwetu sisi, vitengo vyote vilivyotakiwa kushughulika na maendeleo ya nchi, vinashughulika na kazi ya kudhibiti vyama vya siasa na shughuli za kisiasa.
Hapo sasa ndiyo tunazidi kukwama
 
Rais Uhuru wa Kenya leo amesaini makubaliano ya kuiuzia China mapalachichi yote yanayo zalishwa nchini humo na kuwa nchi ya kwanza barani Afrika kupata bahati hiyo.

Wakati sisi maparachichi yetu ya Njombe tunaambiwa yatapata kuuzwa baada ya kupata ndege ya mizigo.
Sasa maparachichi yote yaende China halafu sisi tule nini?
 
Sawa mkuu wacha tuendelee kubishana ba seigi
Ata nchizote za Afrika mashariki zizalishe maparachichi haziwezi kukidhi soko la Uchina, Soko ni kubwa sana, kwaiyo tusinyosheane vidole kila Nchi ilime itapata sokoUchina ilimradi matunda yawe na ubora.
 
Rais Uhuru wa Kenya leo amesaini makubaliano ya kuiuzia China mapalachichi yote yanayo zalishwa nchini humo na kuwa nchi ya kwanza barani Afrika kupata bahati hiyo.

Wakati sisi maparachichi yetu ya Njombe tunaambiwa yatapata kuuzwa baada ya kupata ndege ya mizigo.
Tanzania pia ina makubaliano kama hayo na ndio ilikua ya kwanza.wakenya wanazalisha maparachichi meng lakin ubora wake uko chini kuringanisha na parachichi is Rungwe ambao moja kati ya maparachichi bora.mzarishaji mkubwa kwa sasa ni wilaya ya Rungwe kwa Tanzania.
 
Mwishowe wabaki na afya mbovu....
Wao wabaki wanakula nini!?

Parachichi za Bongo si wenyewe hazitutoshi
 
Back
Top Bottom