erasto Samwel
JF-Expert Member
- Sep 10, 2024
- 211
- 275
Nisipoteze Muda kama Mwanamaombi Niliamua kufunga Masaa 48 ktk Jambo fulani hivi Mwaka mmoja uliopita.
Nilianza asubuhi saa kumi na mbili.Mchana kutwa nilikuwa nafanya kazi zangu ndogondogo.Usiku nilipambana nao hatimaye nikatoboa. Nikaianza siku ya pili Asubuhi nikipunguza shughuli mara Mchana hatimae jioni.Nikaianza tena safari ya usiku saa moja hapo nina masaa 36.kimbembe kilianzia hapo.
Nilidhohofu,Mwili haukuwa na maji baada ya kugundua sina mate hata kujilazimisha kukojo ilishindikana macho yalikosa nguvu ya kuona ,kutembea sasa ikawa shida.
Napepesuka suala la maombi ikawa ni kiroho zaidi manake roho ilikuwa na nguvu.Mara saa tatu usiku nguvu zinazidi kutoweka kabisa na matumaini ya kuumaliza usiku ukawa mdogo kwasababu Asubuhi nilitegemea kufuturu.Usingizi hakuna tena na hakulaliki.
Nilijihisi vibaya.kuongea ilikuwa tabu.ule usiku ulikuwa Mgumu.mpaka hapo nilikuwa na masaa 39.nilishindwa kutoka chumbani kuja sebuleni nikagundua nimefika Mwisho.Mke wangu alijiongeza jioni ile kutunza chakula kidogo maalum aligundua lolote usiku ule ningedai chakula.
Nikamshukuru Mungu kwa ukuu wake na hatimaye nikafuturu kwa udhulu na asubuhi nikafuturu kisawasawa.
1.Nilijifunza kufunga kunahitaji maandalizi ya kuuweka sawa Mwili wiki moja kabla.hasa chakula na kunywa maji ya kutosha.
2.Katika kufunga usisahau kunywa maji.Mwili asilimia kubwa maji ni muhimu sana.
3.Niliona namna roho ilivyokuwa na nguvu ya utendaji wake wa kiroho kisawasawa ktk levo yake.
4.Vilevile ktk kufunga kunahitajika pia maandalizi ya roho kuwa tayari kuukatili Mwili ambao kuushindisha njaa ujipange.ndio ile vita ya roho na Mwili kushindana.
5.Katika kufunga suala la kuoga ni Muhimu ni eneo pia la Mwili kunywa maji na kupata nguvu kulinisaidia.
6.Ni muhimu kusimamisha kazi hilo lilinifelisha kwa mimi kuendelea na tushughuli
7.Nilifanikiwa ktk Mambo yangu.kuna mambo hayafanikiwi ni mpaka kwa kufunga na kuomba
8.Ongereni wafungaji wa Masaa machache na Mengi
Kufunga kusikie tu.