Safari ya Swaumu ya Masaa 48 (siku mbili Mchana,Usiku,Mchana, Usiku bila kula chochote)Funzo

erasto Samwel

JF-Expert Member
Joined
Sep 10, 2024
Posts
211
Reaction score
275
Nisipoteze Muda kama Mwanamaombi Niliamua kufunga Masaa 48 ktk Jambo fulani hivi Mwaka mmoja uliopita.

Nilianza asubuhi saa kumi na mbili.Mchana kutwa nilikuwa nafanya kazi zangu ndogondogo.Usiku nilipambana nao hatimaye nikatoboa. Nikaianza siku ya pili Asubuhi nikipunguza shughuli mara Mchana hatimae jioni.Nikaianza tena safari ya usiku saa moja hapo nina masaa 36.kimbembe kilianzia hapo.

Nilidhohofu,Mwili haukuwa na maji baada ya kugundua sina mate hata kujilazimisha kukojo ilishindikana macho yalikosa nguvu ya kuona ,kutembea sasa ikawa shida.

Napepesuka suala la maombi ikawa ni kiroho zaidi manake roho ilikuwa na nguvu.Mara saa tatu usiku nguvu zinazidi kutoweka kabisa na matumaini ya kuumaliza usiku ukawa mdogo kwasababu Asubuhi nilitegemea kufuturu.Usingizi hakuna tena na hakulaliki.

Nilijihisi vibaya.kuongea ilikuwa tabu.ule usiku ulikuwa Mgumu.mpaka hapo nilikuwa na masaa 39.nilishindwa kutoka chumbani kuja sebuleni nikagundua nimefika Mwisho.Mke wangu alijiongeza jioni ile kutunza chakula kidogo maalum aligundua lolote usiku ule ningedai chakula.

Nikamshukuru Mungu kwa ukuu wake na hatimaye nikafuturu kwa udhulu na asubuhi nikafuturu kisawasawa.

1.Nilijifunza kufunga kunahitaji maandalizi ya kuuweka sawa Mwili wiki moja kabla.hasa chakula na kunywa maji ya kutosha.

2.Katika kufunga usisahau kunywa maji.Mwili asilimia kubwa maji ni muhimu sana.

3.Niliona namna roho ilivyokuwa na nguvu ya utendaji wake wa kiroho kisawasawa ktk levo yake.

4.Vilevile ktk kufunga kunahitajika pia maandalizi ya roho kuwa tayari kuukatili Mwili ambao kuushindisha njaa ujipange.ndio ile vita ya roho na Mwili kushindana.

5.Katika kufunga suala la kuoga ni Muhimu ni eneo pia la Mwili kunywa maji na kupata nguvu kulinisaidia.

6.Ni muhimu kusimamisha kazi hilo lilinifelisha kwa mimi kuendelea na tushughuli

7.Nilifanikiwa ktk Mambo yangu.kuna mambo hayafanikiwi ni mpaka kwa kufunga na kuomba

8.Ongereni wafungaji wa Masaa machache na Mengi
Kufunga kusikie tu.
 
Gentleman,
kula ushibe vizuri, na hakuna haja kujitesa kwa njaa,
ingia tu sirini pako palipotulia vizuri sana, kwa imani thabiti, omba utakalo kwa roho na kweli kwa Mungu nawe utapewa, tafuata kwa bidii bila kukata tamaa wala kushinda na njaa, kwa hakika utapata utakacho taka, na kua na shukrani na ubishe hodi kwa unyenyekevu na milango ya neema na baraka itafunguka mbele na juu yako
 
Kufunga sio kwa namna hiyo. Kama unataka kufunga bila kula kabisa basi lazima ufanye hiki. Unaanza saa 12 asubuhi,ukifika saa 1 jioni kunywa maji ya vuguvugu hata lita 1,kunywa kidogo kidogo,usigugumie. Fanya hivyo na asubuhi saa 12.
 
Mtoa mada,
Nimewahi kufunga mara kadhaa siku 3 bila hata tone la maji ila siyo kwa nguvu zangu mwenyewe..!!

kabla ya kufunga ni lazima kwanza uanze kwa kuiombea hiyo funga yako, lazima uiweke kwenye maombi kwanza na uwe na nia ya dhati,

tofauti na hapo hufungi hata masaa, hivyo wakati mwingine jaribu hiyo njia naamini itakusaidia..!!
 
Ahsante sana kwa ushauri huu, na ahsante kwa kutupa mrejesho kuwa ulifanikiwa.
 
Ulifanya jambo jema...!

Ila Maombi Yako ya mfungo yalivunjika.
Hakuna maombi/Mfungo wenye Nguvu kama Covernent prayer, Kwa sababu unaingia mkataba na Mungu mwenyewe, nidhamu Yako ya kutimiza Yale yote yaliyokua kwenye Mkataba ndiyo yanayofanya Mungu ajibu maombi Yako Kwa haraka..... Na hiyo inafanya Mungu aanze kuamini coz ukimwambia mfano, ukinipa Utajiri nitatumia Utajiri utaonipa kusaidia Masikini na wenye nahitaji, Sasa Mungu kukuamini huko kunaanzia Kwa vitu kama hivyo, ungejitahidi umalize hayo masaa yaliyobaki ungetoboa.

Lakini SI tatizo wakati mwingine tunatakiwa kuanza Mazoezi ya kufunga kidogo kidogo, kufunga siku 3 kavu Kwa mara ya kwanza SI kazi rahisi.

Next time Anza na 24 hours kavu, then 36 hours.....! Then unaweza kwenda 48 hours huku ukinywa Maji tu, hapo Mwili wao utakua unaanza kuzoea, Sasa ndiyo unamwambia Mungu this time nafunga 48 hours.

Jambo la Muhimu usifunge tu vile unataka kufunga, lazima usikie Roho Mtakatifu anakwambia ufunge, na ukifunga Kwa msaada wa Roho Mtakatifu, pale Mwili unapokua hauwezi, unamwambia na yeye anakutia Nguvu, coz Mfungo ni Vita kamili ya kiroho na Shetani hataki kuona ukitoboa.

Mungu akutie Nguvu, Kuna Nguvu katika kufunga, usisubiri mpaka upate matatizo ndo ufunge, wakati mwingine unaweza kumwambia Mungu nataka kufunga na Lengo la kufunga kwangu ni kuwa karibu na wewe, kukusifu na kukuabudu basi, hata kama wakati huo huna kazi, huna pesa, ila unamwambia Mungu nataka kufunga Kwa ajiri ya kukusifu na kukuabudu tu.....! Na ukafanya hivyo Kwa Moyo wao wote..... I'm telling you my Brother Mungu atajibu Matatizo Yako na hukumwomba, atajibu mpaka na Nyongeza....!

Ni maombi yangu Kwa Mungu uwe na tabia ya kufunga hata siku 1 Kila week.
 
Kufunga sio kwa namna hiyo. Kama unataka kufunga bila kula kabisa basi lazima ufanye hiki. Unaanza saa 12 asubuhi,ukifika saa 1 jioni kunywa maji ya vuguvugu hata lita 1,kunywa kidogo kidogo,usigugumie. Fanya hivyo na asubuhi saa 12.
Hapo unakua hujafunga
 
Sijui kwanini nimekutana na huu uzi Leo hii, Ila sawa.
Ahsante kwa ujumbe.

Mtu anaweza akakukasirikia, akaona unajigamba kwa kutangaza matendo yako ya kiimani. Ila ungeandika namna unakula pisi huko mtaani wanaona ni sawa tu.

(AHSANTE KWA INJILI NA IKIWA HULUJIBIWA BASI KITENDO HIKI CHA KUHUBIRI MUNGU AKATUMIE KAMA SABAB YA KUJAZISHIA MATENDO YAKO YA IMANI KATIKA KULUBARIKI KWAYO)
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…