Safari ya Ujasiriamali ni sawa na Story ya Rutu na Familia yao na Walivyo ambiwa wasitazame nyuma wanapo ondoka mji ule

Safari ya Ujasiriamali ni sawa na Story ya Rutu na Familia yao na Walivyo ambiwa wasitazame nyuma wanapo ondoka mji ule

CHASHA FARMING

JF-Expert Member
Joined
Jun 4, 2011
Posts
7,872
Reaction score
9,263
Ni kwa nini Rutu aliambiwa asitzame nyuma pindi anaondoka mji ule?

Ni kwa sababu Mungu alijua fika kitendo cha kutazama nyuma tu kitafanya Rutu abadilishe mawazo yake ya safari na kuamua kurudi kwenye ule mji.

Safari ya Ujasiriamali ni gumu sana, ni safari ambayo ukiwa na huruma na unao waacha nyuma kamwe hutatobo.

Ukiwa na mapenzi yaliyo pitiliza ya unao waacha nyuma kamwe hutatoboa.

Ukiwa unawaza marafiki zako unao waacha kamwe hutaanza safari.

Ukiwa unawaza viwanja unavyo enda kujirisha kamwe hutatoboa.

Ukiwa unawaza Mfumo wako wa zamani wa maisha kamae hutafika mbali.

Wengi huwa hatuwezi fika popote na safari hii kwa sababu ya kuangalia nyuma.

Watu huwa tunatembea tukiangali nyuma ndo maana hatutoboi.

Kuanza safari kuna vitu vingi lazima uviache.
- Lazima marafiki wako wa viwanja wakukose
- Lazima ndugu zako wakuchukie na wakusema sana.
-Lazima familia yako some time wasikuelewe, watoto na hata mke.

MKE WA RUTU uvumilivu ulimshinda mje wa rutu alikumbuka sana starehe za ule mji, Mali zake kwenye ule mji, marafiki zake wakubwa kwenye ule mji.
Ndugu zake na jamaa.

Mke wa Rutu akaona hawezi maliza safari yake bila kutazama vitu anavyo viacha na vitakavyo teketea akaonelea atazame nyuma.




Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kweli kabisa.Bila ya kuwa na roho ngumu mafanikio utayasikia kwa jirani tu.Gharama za mafanikio ni ubahili na lawama toka kwa watu wanakuzunguka.Pasipo pata haya mambo sahau kuwa na mafanikio ya kifedha
 
Hivi nauliza watu wote humu tanzania ni wasukuma "RUTU" ni nani Rekebisha hapo Ni "LUTU"Msituharibie biblia anyway Maudhui yako ni Mazuri
 
Hivi nauliza watu wote humu tanzania ni wasukuma "RUTU" ni nani Rekebisha hapo Ni "LUTU"Msituharibie biblia anyway Maudhui yako ni Mazuri
Nini hujaelewa? Wengine hatujaenda shule hivyo tunafanya kujifunza kuandika, ila kikubwa ni ujumbe na sio imeandikwa vipi, au unataka kuchukua nafasi ya Faiza Fox?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hivi nauliza watu wote humu tanzania ni wasukuma "RUTU" ni nani Rekebisha hapo Ni "LUTU"Msituharibie biblia anyway Maudhui yako ni Mazuri
Nitarara na wewe mbere,i wish i courud be moderator
 
Safari ya mafanikio kwakweli kama wazungu wanavyosema "is not easy job my friend".

Mimi nikiona mtu aliyefanikiwa hua nampa heshima yake na kumpenda,maana najua mpaka pale alipofikia amegina sanaa.

Kwa jamii zetu za kitanzania
Kama bado unawasikiliza wazazi,majirani,marafiki,wanasiasa,viongozi wa dini sahau kabisa mafanikio ya kifedha na ujasiriamali kwa ujumla.

Mimi binafsi toka nianze safari ya ujasiriamali mahusiano yangu na ndugu yamekufa kwa 90%,rafiki zangu wamebaki wachache sana hasa wale ambao wako kwenye ujasiriamali,rafiki zangu wa kike lol sijui wamepotelea wapi ila nimebahatika kukutana wengine ambao wako kwenye ujasiriamali wako vizuri kimtazamo..

Kiufupi safari ya ujasiriamali lazima ujikane nafsi yako na uwakane ndugu zako kwa nia njema lakini ndo utafika unapopataka.

Mtoa mada asante
 
Ni Kweli kabisa kwa wale waajiriwa inakuwa ngumu sana kueleweka kwa mates,ndugu,wazazi,hata familia.Inahitaji ujali wa hali ya juu kuingia katika ujariamali.Note
If you work for money you give the power to you're employer and control it.

great thinker
 
Ni kweli kabisa!! Pia hutakiwi kugeuka nyuma na kuhesabu :

**walioanza na wakashindwa.. Zaidi unatakiwa uangalie wewe umelenga nini

**kuwaza kupata hasara... hapa hunabudi kujua si kila safari katikati ina ajali!! Na si kila ajali husababisha vifo, nyingine hujeruhi tu na maisha yanaendelea. Pia kumbuka ajali zipo kila siku lakini watu hawaachi kusafiri

**usiangalie nyuma kuchungulia walioshindwa wakaanguka, angalia mbele waliofanikiwa japo kweli kushindwa kupo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimeona hii thread nikahisi umeniandika mimi,,recently nimekua kwenye dillema,,kazini nimepewa a very tempting offer,,lakini moyo wangu haupo hapa,,upo kwenye biashara yangu nayoiona ina future nzuri,,uwezo wetu wa kukataa vitu vizuri ndo unaweza kifanya tupate vitu the best,,uzi mzuri umenifikirisha,aksante mkuu
 
Back
Top Bottom