Safari yangu ya kwenda Bulombola ilivyonikutanisha na Mrembo wa Kaskazini

Safari yangu ya kwenda Bulombola ilivyonikutanisha na Mrembo wa Kaskazini

Tajiri Mapesa

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2020
Posts
707
Reaction score
728
Habari za leo wanaJamiiForums, leo nimeamua kufunguka na kutoa kisa changu cha kweli kilicho nitokea mwaka 2013, basi mambo yalikua hivi;

Ilikuwa ni mwezi wa sita mwaka 2013, nikiwa nipo nyumbani nikasikia tetesi kwamba majina ya wa wanafunzi walio hitimu kidato cha sita yametoka. Lkn sikujua ni kwaajili ya nini, ilinibidi niulize vzuri, kumbe yalikua ni majina ya wanafunzi walio chaguliwa kwenda jeshini,

Mapigo ya moyo yalianza kwenda kasi huku nikiomba Jina langu lisiwemo maana niliskia jeshini kuna mateso sana.

Nilichukua simu yangu ya tekno ya batani yenye kamshale nkaingia kwenye mtandao wa gugo nkapakua majina, ghafura moyo wangu ulishatuka paa, mara baada ya kuliona Jina langu. Nilikua nimechaguliwa Kambi ya Burombola kigoma 821 KJ, KJ yaan kikosi cha jeshi. Tangazo lilisema tunatakiwa kuripoti kambini kabla ya tarehe 24 mwezi sita

Kipindi hicho nilikua nafanya kazi ya uwalimu katika shule moja ya sekondari iliyopo mkoani Mbeya. Mimi ndiye nilikuwa mwalimu wa fizikia wa kutegemewa katika shule ile.

Nliogopa sana lkn sikua na jinsi maana mkuu wa jesh alitangaza kuwa ambaye hata huzuria atachukuliwa hatua za kisheria. Ntafanyeje mimi nilibaki na mawazo kichwani, nikasema hamna shida acha tu niende. Ilinibidi niache kazi na kuanza kujipanga ili kwenda jeshini

Nilianza kufanya mazoezi ya kukimbia nyumbani ili kujiweka tayari kwaajili ya jeshi. Nilifanya mazoezi ya pushapu na kukimbia, mapenzi ya nyoka pamoja na zoezi la kubeba dunia.

Saa moja asubuhi nilipanda basi la kosta mpaka Mbeya mjini. Nkafika stend kuu nikachukua ticket ya kwenda sumbawanga, asubuhi sana basi liliondoka mbeya kuelekea sumbawanga tukafka sumbawanga mida ya saa sita mchana. Nlikua nakuogopa sana sumbawanga, watu walikua wakisimulia kuwa kuna wachawi wengi alafu ni kubaya. kumbe ni kuzur kabisa alafu ni mjini.



Mida ya jioni, nilichukua chumba cha kulala sumbawanga bahati nzuri nkakutana na wenzangu wengine gesti house nao pia walikuwa wanaenda jeshini, niliwagundua kwa kuwa walikuwa wamenyoa vipara, nkasema hapa bora tuwe wengi. Usiku nikiwa kitandani nilikuwa makini kuangalia juu ya dari na kwenye kona za chumba, maana niliogopa kukabwa. Baadaye usingizi ulinichukua, nilikuja kushituka asubuhi, kwa kweli usiku nililala usingizi mzuri sana.

Asubuhi sana mida ya saa 11 tuliondoka sumbawanga kwa basi kuelekea mpanda, tukafka mpanda saa nane mchana maana ni mbali, lkn nlikua naskia waziri mkuu anatokea mpanda ananyumba, kweli nilitmani kupaona kwake, ilinibidi niende mpaka kwake, alikuwa na wake zake wengine pale japo yeye alikua anaish Dar, nyumban kwake palikua ni pa kawaida sana. Skutegemea kama ile nyumba ni ya waziri kumbe mawaziri nao huwa wanaishi maisha ya kawaida kabisa

Mida ya saa 11 jioni nilienda stendi kukata tiketi, ya kwenda kigoma. Kipind kile gari ya kwenda kigoma ilikuwa ni moja tu, inaenda kigoma j3 na j5 bac ukichelewa ndio bas.

Kwel siku ile nilikuta basi limekwisha jaa, ila waliniahidi inabidi nisubiri mpaka kesho yake asubuhi sana, walinieleza tukiwapita polisi ndipo nitapanda maana walikuwa wanakataza kujaza watu

Asubuhi niliamka kwa kuchelewa sana kwani basi lilikuwa limekwisha niacha na basi la kwenda kigoma lilikua ndio hilo tu na hiyo ndio ilikua ni tarehe ya kuripoti kambini

Basi basi lilikua limesha niacha, nilibaki stendi skua na cha kufanya nkaanza kulia nitafanya nini, ndipo nilipo mwomba bodaboda anisaidie kulifukuzia basi, nilitoa noti mbili za elfu 10 nkamlipa akaniambia tutalifukuzia

Safari ya kulifukuzia basi ilianza, hiyo ilikua ni saa moja asubuhi, barabara ya mpanda mpaka kigoma ni vumbi jingi, mimi nilipanda nyuma bodaboda ilikua inakimbia kwa mwendo wa kasi sana, tuliendesha umbali wa kama km 12 tukafanikiwa kulikuta basi likasimama ndipo nikapata

Ndani ya basi hamkua na siti hivyo nilisimama watu wote walikua wamechafuka sababu ya vumbi, nilipata rafki kwenye basi tukawa tunapiga naye stori za jeshi. Basi lilifika uvinza nikiwa njiani niliuona mto magadi wenye maji ya Chumvi,

Tulishuka uvinza tukala chakula, tukaendelea na safari, tulifka kigoma mjini saa 12 jioni sana. Sikuwai fika kigoma mjini ndio ilikua mara yangu ya kwanza ni pa kawaida sana utafkiri sio mkoa. Mida ya saa 12 na 1/2 jion nilitafuta daladala ya kwenda Bulombola nkaipata nkapanda Daladala ilikua inaendeshwa kwa kasi sana, utadhani inaendeshwa na mwanajeshi, nikiwa njiani nkaliona ziwa Tanganyika karibu na barabara,

Mara tu tukashushiwa kwenye geti la Kambi. Kweli tulishuka wengi hadi wazungu wachina na wahindi pia walishuka wakiwa na majiko yao ya stove kwaajili ya kupikia.

Itaendelea……

Inaendelea Sehemu ya Kwanza

Baada ya kushuka pale getini tuliingia ndani ya ile kambi. Pale mapokezi tuliambiwa tuweke mabegi yetu kwenye kichumba fulani ambacho kilikuwa jirani na pale reception.

Tukiwa tumesimama pale akaja afande mmoja ambaye ana mwili wa mazoezi, mrefu na mnene kiasi. Akatuambia tupange mstari, wanawake mbele na wanaume nyuma.

Lahaula... Nilishangaa yule askari akituambia tuvue nguo zote tubaki kama tulivyozaliwa. Wengi wetu tulisitasita kufanya zoezi ilo, hadi pale wawili miongoni mwetu walipopigwa kelebu za nguvu na kuangukia mtaroni.

Basi hapo ndio kila mtu akaanza kusaula manguo yake, mbele yangu nakumbuka alikuwa dada mmoja hivi mweupe mweupe na alikuwa amevaa ligauni lirefu hadi miguuni. Basi baada ya kuambiwa tuvue nguo ndio nikauona uzuri wa umbo lake halisi jinsi alivyokuwa amejazia.

Hali hiyo ilinifanya nisahau nipo wapi nikajikuta naanza kumtani nimgijigiji, nilianza kuwanza nipo nae kitandani hali iliyonifanya nisisikie maelekezo tuliyokuwa tunapewa na yule afande hadi pale nilipotolewa kwenye lile lindi la mawazo baada ya kuhisi nimepigwa na kitu kizito kama mbao mgongoni kumbe ni yule afande alikuja kunipiga kofi la mgongo baada ya kuniona nimeconcentrate kuangalia lile tako la mtoto wa kaskazini.

Itaendelea......


Shemu ya Pili

Safari yangu ya kwenda Burombola ilivyo nikutanisha na mrembo wa kaskazini sehemu ya 2.

Basi mara baada ya kushushiwa getini tulishitushwa na sauti kubwa ya afande, "wote mikono juu, piga magoti, piga magoti" tukaswagwa mpaka kwenye kiunga kimoja karibu na geti la kambi huku tukiwa tunatembelea magoti. Wenye mabegi na mizigo mikubwa walitembea kwa magoti huku mabegi yao yakiwa kichwani.

Mimi bahati nzuri niliambiwa na rafiki yangu aliye jiunga na mafunzo intake ya kwanza kuwa nisiende na begi kubwa, hivyo nilibeba kisport changu kidogo kimeandikwa luck Dube, ndani nilibeba kikombe, kijiko, sahani moja, nguo mbili yaani shati moja na suruali moja pamoja na zile nilizo kuwa nimevaa jumla nguo nne.

Mara baada ya kuswagwa mpaka kwenye kile kiunga karibia na geti la kambi afande aling'aka na kusema "toa simu yako haraka na umpigie mzazi wako kuwa umefika kambini" mimi nilikua nikichelewa kutoa Mara afande alikuja upande wangu alinizaba banzi moja la mgongo, nilitoa simu yangu haraka huku nasikilizia maumivu. Afande alikua haraka kama mashine ya cherehani utazani amevuta Bangi maana hata macho yake yalikua mekundu sana, watu walikua wazabuliwa mabanzi utazani magunia.

Basi kila mmoja alibaki kuwa na hofu moyoni huku machozi yakimlenga. Nilitoa simu yangu na kumpigia simu mama, na kumtaarifu kuwa tayari nimefika salama kambini, basi mama aligundua kuwa kama nilikua nalia, ndipo alipo niuliza ni kwema huko, ile nataka kumwambia afande aliamuru kila mmoja atoe laini ya simu kwenye simu na tumkabidhi simu zote. Alikua akizungumza kwa sauti kali utafikiri Simba aliye ona swala, na wakati anazungumza alikua akipitisha mabanzi na mabuti ya migongoni. Basi mara baada ya zoezi lile la kumkabidhi zile simu afande mawasiliano na wazazi na ndugu zetu wa karibu yalikatika ghafura.

Tulipelekwa na afande mpaka mabwenini ambapo kwa lugha ya kijeshi wanaita mahanga, tulipangiwa kila mmoja maeneo yake ya kulala. Baadaye afande alitupeleka mpaka jikoni tukapewa msosi tukala, nakumbuka ulikua ni wali, na maharage na chai rangi. Mimi tangia nianze nijiunge na masomo yangu ya advance kwa kweli sikuwai kubakisha wali kwasababu tulikua tukipimiwa ratio ndogo sana, kwasababu katika shule ile niliyo soma kulikuwaga na ufisadi mkubwa sana wa wali na nyama. Lakini kwa mara ya kwanza siku ile nafika jeshini nilipewa wali mwingi sana lakini pamoja na juhudi zangu zote katika swala ulaji sikufanikiwa kuumaliza bali niliishia kuutupa kwenye dampo lililo kuwepo pembeni mwa lile jengo la jiko.

Lakini nilipo angalia na wenzangu nao pia hawakufanikiwa kumaliza kile chakula. Mara alikuja kijana mmoja ambaye ni service man yaani kijana aliye maliza mafunzo yake tayari akaanza kutupigisha stori. Kwanza alianza "wazalendoooooo ni kawaida ya mzalendo kutomaliza chakula. Mmeshiba lakini au tuwaongeze, kula mzalendo kula mzalendo mzabuni hanaga nomaa" kiukweli yale maneno ya yule service man yalianza kunitia mashaka. Baadaye alikuja afande mmoja ambaye alijulikana kwa jina la afande mwita, akamwambia yule service man kuwa atupeleke kulala na alisisitiza kuwa wazalendo wasiteswe na wasisumbuliwe walale mapema.

Basi kila mmoja alienda kulala kwenye hanga lake asubuhi tuliamka mida ya saa mbili asubuhi tukaenda kunywa chai, kabla ya kupewa chai tuliamriwa kupanga mistari nikiwa kwenye mstari macho yangu yalikua yakiangaza kila pembe, nilianza kuwaona wototo wakali wa kila aina, wengine weupe, maji ya kunde na wengine mablack beauty, wengine wahindi wengine wachina. Alafu wengi wao walikua ni wale watoto laini walio toka shule kali kama za fedha girls, Baobab, Marian girls n.k. Basi baadaye nililifikia dirisha la mgawaji ambaye pia alikua ni afande aliye julikana kwa jina la mzabuni. Yule afande akinipatia mkate mmoja mkubwa uliopakwa blue band safi, karanga pamoja na chai kwenywe kikombe kikubwa.

Niliondoka nikakaa karibu na Marafiki zangu tukaanza kuifakamia chai, kiukweli katika maisha yangu sijawai kula mkate mkubwa kama ule, mara tu baada ya kunywa chai nilishiba sana, afande alipo toa nafasi ya kubasti mimi sikuwa na hamu tena lakini pia nilishangaa sana hata rafiki zangu pia hawakuwa na hamu tena. Basi akati naangaza macho huku na kule, nilishituka nilipo gonganisha macho na afande mmoja wa kike.

Afande yule alikua mrefu, mweupe, mwenye umbo zuri na macho yake yalikua yanavutia sana lips zake nazo zilikua ni tamu kwa kuzitizama tu. Afande yule ambaye nilisikia akiitwa kwa jina la afande Suzan, alikua amevalia kombati ya kijani isiyo na bakabaka na buti. Nilipo mwangalia kwa muda mrefu sana nilianza kuvuta picha na kumfananisha na binti mmoja wa kichaga mrembo niliyetokea kumpenda sana, jina lake Sophia, kiikweli Sophia alifanikiwa kuuteka moyo wangu wote hakubakiza hata nusu.

Naweza kusema pale kijijini kwetu hakuna binti aliye kuwa anamzidi uzuri. Sophia alikua ni mzuri tena ule uzuri wa asili wa bila losheni, maana alikuwa akitokea kwenye familia ya kimasikini ambayo haikuwa na uwezo wa kumudu kununua hata carolaiti. Nina uhakika mafuta aliyo akipaka Sophia yalikua ni top raise lakini kutokana na kwamba Mungu alimzawadia rangi nyeupe ya kuvutia, Sophia bado alionyesha uzuri wa asili.

Sophia nilitokea kumpenda lakini umbali uliokuwepo kati ya nyumbani kwao na kwetu ulipelekea mimi kutofikisha ujumbe wangu kwake. Alafu ukizingatia kwao kulikua ni polini sana kwa hiyo walikuwa wamefuga limbwa likali sana. Siku moja nilifunga safari kwenda kwao kwa mguu ambapo ulikua ni umbali kama wa kilometa 5 tokea nyumbani, mara nilipofika tu niishia kufukuzwa na mbwa mkali sana. Baadaye nikabadirisha njia ili kumkwepa yule mbwa nikawa namsubiria Sophia kwenye njia moja ya kwenda mtoni ili nimbane kama akitokea kwenda mtoni labda anaweza akatoka lakini sikufanikiwa kumwona. Mpaka ilipofika jioni nikaamua kurudi nyumbani bila mafanikio.

Alafu kibaya zaidi kipindi hicho Sophia hakua na simu, kwa hiyo nilitumia zaidi njia ya barua kuwasiliana naye. Lakini kuonana naye ana kwa ana ilikuwa ni mtihani sana. Basi nilivyo mwona yule afande kiukweli walikuwa wanafanana copy write utafikiri alikuwa ni dada yake, kwakweli nilianza kutamani kwenda kuongea na yule afande. Na kwa vile mimi sikuwa mwoga basi niliamua kumface afande yule wa kike ili nimuulize vizuri kama ana undugu wowote na Sophia wangu.

Itaendelea...........
..
 
Dah bro umenikumbusha mbali sana hapo burombola nakumbuka kuna mtoto nilitokea kumpenda sana sema katika michakato ya kumtemea madini ilikuwa ngumu sababu ya maovyoovyo siku moja tuko kwenye six week nikammendea ile tumelala nikamla mate nilishangaa sana alirespond positively mpk nikaanza kupima oil bahati mbaya makamanda wakapiga filimbi tuamke dah ile moment sitasahau kumbe mtoto naye alikuwa na nyegez zake tu dah
 
Hii post inanikumbusha mbali wakati huo Nina full kombati npo kwenye mashamba ya mpunga na silaha yangu nipo guard zamu yangu hapo napigwa na baridi kwelikweli mpaka natoa kamasi puani kwenye mfuko wa koti kuna picha ya mtoto nilipiga nae naichomoa namuuangalia nakumbuka good memory napata morali nasema yes one day nitarudi uraiani nikuone ..


I miss her a lot


82_? KJ




Sent using Jamii Forums mobile app
 
Funguka bibie

Ma service man

Na ma privite

Walikuwa wanakusumbua kuruta wa mungu ?

Au ulikuwa unadosolewa kwa kua ulizidi kuwa nanga

Sent using Jamii Forums mobile app
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787] Nimeishia kucheka tyuuuh lol, yaan weeee khaaaaah

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom