Safari yangu ya Mji Mwema ikageuka kuwa ya mateso

LA7

JF-Expert Member
Joined
Aug 26, 2019
Posts
655
Reaction score
2,369
Habari zenu humu ngoja Leo niwape kastory kafupi

Nakumbuka nikiwa naishi maisha ya homeless siku hiyo nikiwa pale kigamboni kwenye boti za uvuvi, upande wa chuo cha mwalimu Nyerere memorial

Muda wa saa 9 jioni nikachukua baiskel yangu na kuamua kwenda kutembea Mji mwema

Nikafika na kuanza kutafuta namna ya kutokea ufukweni, lakini Kila njia niliyoifuata nilikutana na maandishi yaliyosomeka FAMILY BEACH nilijaribu zaidi ya njia tatu zenye urefu wa zaidi ya 1km Hadi nikakata tamaa,

Nikaamua kurudi zangu Sasa nikaamua kupitia shortkat kosa nililofanya ni kufuata jua, baadae nikakutana na njia ya lami inashuka nikaamua kuteremka nayo, nilikuja kujua kuwa nimepotea baada ya Kuona Yale maghorofa pacha pale posta kwa mbalisana yakiwa kama kwenye Moshi Moshi hivi, hapo nikaamua kuyafuata kwa kunyokea huku nakokota baiskeli muda huo ni saa1 inaelekea hivi kwani baiskel ilipata pancha,

Nilijikuta nimetokea kongowe mpaka nafika daraja la reli pale sijui ndo mto ngani nikaamua kutembea na reli mpaka nikajikuta nipo katikati ya makontena na matanki ya mafuta pale bandarini, muda huo inaelekea saa4 usiku nikatokea eneo Moja ambalo nilizunguka kama saa nzima, kwani Kila njia niliyoifuata isiponipeleka chooni basi itanipeleka nyumba ya mtu au inakuwa na mwisho,

Basi bhana nikafanikiwa kutoka mpaka saatano hivi nikafika kivukoni nilikuwa na buku tu mfukoni nikanywa juisi ya 500 iliyobakia nikavuka upande wa pili nikaenda boti Moja mbovu nikaficha baiskeli kwa kuifukia kwenye nyavu na mm nikajikunja na usingizi ukanipitia mpaka kukakucha nikaamka na kupeleka usafiri wangu kwa mtu ambaye hunitunzia tuamoyo.
 
Tuliokulia huku madongo poromoka tutasema ulikanyaga kale ka mdudu, inasemwa eti kuna kadudu flani ukikakanyaga hata kama uko nje ya nyumba utajiona upo mazingira mengine kabisa
 
Motivesheni spika anakuambia ndo ikawa chanzo Cha kuanzia kampuni ya tour guide
 
Habari zenu humu ngoja Leo niwape kastory kafupi

Nakumbuka nikiwa naishi maisha ya homeless siku hiyo nikiwa pale kigamboni kwenye boti za uvuvi, upande wa chuo cha mwalimu Nyerere memorial

Muda wa saa 9 jioni nikachukua baiskel yangu na kuamua kwenda kutembea Mji mwema

Nikafika na kuanza kutafuta namna ya kutokea ufukweni, lakini Kila njia niliyoifuata nilikutana na maandishi yaliyosomeka FAMILY BEACH nilijaribu zaidi ya njia tatu zenye urefu wa zaidi ya 1km Hadi nikakata tamaa,

Nikaamua kurudi zangu Sasa nikaamua kupitia shortkat kosa nililofanya ni kufuata jua, baadae nikakutana na njia ya lami inashuka nikaamua kuteremka nayo, nilikuja kujua kuwa nimepotea baada ya Kuona Yale maghorofa pacha pale posta kwa mbalisana yakiwa kama kwenye Moshi Moshi hivi, hapo nikaamua kuyafuata kwa kunyokea huku nakokota baiskeli muda huo ni saa1 inaelekea hivi kwani baiskel ilipata pancha,

Nilijikuta nimetokea kongowe mpaka nafika daraja la reli pale sijui ndo mto ngani nikaamua kutembea na reli mpaka nikajikuta nipo katikati ya makontena na matanki ya mafuta pale bandarini, muda huo inaelekea saa4 usiku nikatokea eneo Moja ambalo nilizunguka kama saa nzima, kwani Kila njia niliyoifuata isiponipeleka chooni basi itanipeleka nyumba ya mtu au inakuwa na mwisho,

Basi bhana nikafanikiwa kutoka mpaka saatano hivi nikafika kivukoni nilikuwa na buku tu mfukoni nikanywa juisi ya 500 iliyobakia nikavuka upande wa pili nikaenda boti Moja mbovu nikaficha baiskeli kwa kuifukia kwenye nyavu na mm nikajikunja na usingizi ukanipitia mpaka kukakucha nikaamka na kupeleka usafiri wangu kwa mtu ambaye hunitunzia tuamoyo.
Hii iliwahi kunitokea pia ilikuwa maeneo ya tabata matumbi nikakutana na foreni Kali nijihisi uhasibu ni hapo Tu basi nikashuka nikasema nitembee huku nikilifahamu jiji
Nilitembea mpaka buguruni, nikakatisha kwenda ila vichochoroni huko nikapotea

Imagine tangu saa saba mchana nimekuja kutokea machinga complex saa 11 jioni
Hapo natetemeka, siwezi kuuliza naogopa kuibiwa mjini wala kupiga simu kwa mwenyeji wangu ajue nimepotea wakati me ndio mjanja
Nilikujakuona gari zimeandikwa kawe-mbagala nikasema ndio hizihizi ila kimbembe ikawa bado kujua gari ipi inatoka mbagala na ipi inaenda kawe

Aisee hapo ilinibidi kuuliza Tu, mpaka nafika uhasibu ni saa 1 jioni..nilikoma na jiji hili

Nilikaa zaidi ya miezi mitatu ndio nikashare story hii yakupotea
 
Back
Top Bottom