Safari za ndege za masafa marefu zinaweza kuathiri vipi mwili wako?

Safari za ndege za masafa marefu zinaweza kuathiri vipi mwili wako?

Faana

JF-Expert Member
Joined
Dec 12, 2011
Posts
38,657
Reaction score
44,759
Qantas imetangaza kuwa itazindua safari za ndege za moja kwa moja kutoka pwani ya mashariki ya Australia hadi London, Uingereza kutoka mwisho wa 2025, na muda wa ndege wa zaidi ya saa 19.

Kwa kulinganisha, ndege za sasa huchukua saa 24, lakini kwa kuunganisha ndege, imegawanywa katika safari fupi.

Kwa hivyo, mwili unaweza kubadilikaje wakati wa kusafiri kwa muda mrefu? Je, itakuwa tofauti na ndege za leo za masafa marefu?

1. Uwezekano wa upungufu wa maji mwilini

Chanzo cha picha, Getty Images

Upungufu wa maji mwilini ni jambo la kawaida kwenye safari za ndege za masafa marefu. Ndiyo maana unaweza kuhisi ukavu wa koo, pua na ngozi yako kwenye ndege. Muda mrefu wa safari kunaweza kusababisha hatari kubwa ya upungufu wa maji mwilini.

Hii ni kutokana na unyevu ikilinganishwa na ule ulio ardhini. Hii ni hasa kwa sababu hewa inaingia kwenye ndege kutoka nje, na hakuna unyevu mwingi katika hewa ya angani.

Unaweza pia kukosa maji mwilini kwa kutokunywa maji ya kutosha, au kwa kunywa pombe kupita kiasi (pombe ni diuretiki na husababisha kuongezeka kwa upotezaji wa maji). Kwa hiyo, kunywa maji kabla ya kupanda ndege. Pia kunywa maji zaidi kuliko kawaida wakati wa kusafiri.

2. Safari inaweza kuathiri umakini, masikio, tumbo na usingizi

Chanzo cha picha, Getty Images

Kadiri mgandamizo kwenye ndege unavyobadilika, hewa katika mwili wako hubadilika pia.Huongezeka ndege inapopanda na mgandamizo wa hewa unapungua, na kinyume chake wakati ndege inashuka. Hii inasababisha baadhi ya matatizo ya kawaida kama vile:

Maumivu ya masikio: Shinikizo kwenye ngoma za masikio wakati kuna tofauti katika shinikizo la hewa kati ya ndani na nje ya ngoma za masikio.

Maumivu ya kichwa : Inaweza kusababishwa na kutanuka kwa hewa katika mfupa hasa ndani ya fuvu ( Sinus)

Matatizo ya tumbo : Unaweza kusumbuliwa na gesi zaidi.

Unaweza pia kuhisi usingizi zaidi kuliko kawaida. Hii husababishwa na mwili kushindwa kunyonya oksijeni nyingi kutoka kwenye ndege kama ilivyo kawaida ardhini.

Hali hii inaweza kukufanya uhisi usingizi. Lakini habari njema ni kwamba matatizo mengi si lazima yaonekane zaidi kwenye safari ndefu za ndege, mara nyingi huonekana wakati ndege inapanda na kushuka.

3. Damu kuganda na kuziba mishipa ya damu (thrombosis )

Chanzo cha picha, Getty Images

Mara nyingi wasiwasi mkubwa kwa abiria ni kuganda damu kutokana na kutotembea kwa muda mrefu.

Hii ni pamoja na kuganda kwa damu ambayo hujiunda kwenye miguu (deep vein thrombosis, DVT), athari ambayo inaweza kusafiri hadi kwenye mapafu

Kadiri sababu zifuatazo za hatari zinavyozidi, ndivyo uwezekano wako wa kupata donge la damu unavyoongezeka:

Umri mkubwa

Uzito mkubwa

Historia ya tatizo la kuganda damu katika familia

Matatizo fulani ya damu

Ujauzito au kwa aliyejifungua hivi karibuni

Saratani

Upasuaji wa hivi karibuni au baada ya upasuaji mjamzito au hivi karibuni alikuwa na mtoto

Aliyetumia tiba ya homoni au kumeza dawa za uzazi wa mpango

Kadiri safari ya ndege inavyoendelea, ndivyo hatari ya kuganda kwa damu inavyoongezeka, kulingana na hakiki ya 2022 iliyojumuisha data kutoka kwa tafiti 18.

Watafiti walihesabu kuwa hatari ya kuganda kwa damu iliongezeka kwa asilimia 26 kwa kila saa 2 za kusafiri kuanzia baada ya saa 4 za safari.

Kwa hivyo ni hatari gani ya kuganda kwa damu kwenye safari ndefu ya ndege?

Hatutaweza kuthibitisha hatari hiyo hadi tuanze kuwachunguza abiria kwenye safari hizo za ndege.

Hadi ushahidi utakapopatikana, mapendekezo ya sasa yanabaki kutumika.

Endelea kufanya kazi, kunywa maji mengi na punguza unywaji wa pombe.

Pia kuna ushahidi kwamba kuvaa soksi za kubana pia kunaweza kusaidia kuzuia kuganda kwa damu.

Soksi hizo zinasemekana kuboresha mzunguko wa damu kwenye miguu na kusaidia kurudisha damu kwenye moyo.

Kwa kawaida, hii hutokea kutokana na kupungua kwa misuli inayosababishwa na kutembea.

Ukaguzi wa Cochrane wa 2021 ulijumuisha matokeo kutoka kwa majaribio tisa yaliyohusisha watu 2,637 ambao walichaguliwa bila mpangilio kuvaa au kutovaa soksi za kubana kwenye safari za ndege zilizochukua zaidi ya saa tano.

Hakuna hata mmoja wa washiriki aliyepata dalili. Lakini kuna ushahidi kwamba watu wanaovaa soksi za kubana wana nafasi iliyopunguzwa sana ya kupata vidonda vya damu visivyo na dalili.

Tunajua kwamba damu iliyoganda ina uwezo wa kukua, kusonga na kusababisha dalili. Kwa hivyo ikiwa una wasiwasi juu ya kuganda kwa damu, ni bora kushauriana na daktari wako kabla ya kuruka.

Kwa kawaida, ukiwa na damu iliyoganda, huijui wakati huo, hujui hadi ushuke kwenye ndege (kawaida) kwa sababu inachukua muda kuganda na kuzunguka mwilini.

Kwa hiyo angalia dalili zifuatazo baada ya kusafiri: maumivu ya mguu na uvimbe (mara nyingi mguu mmoja tu), maumivu ya kifua, kikohozi na upungufu wa pumzi. Pata usaidizi wa dharura wa matibabu ikihitajika.

4. Mionzi

Chanzo cha picha, Getty Images

Ikiwa unaruka umbali mrefu mara kwa mara, ni busara kudhani kwamba kadiri unavyokaa angani, ndivyo mwili wako unavyopata mionzi ya anga.

Kama jina linavyopendekeza, hii ni mionzi kutoka angani, ambayo inaweza kuongeza saratani na hatari za uzazi.

Hatujui ni viwango gani vya mionzi ni salama. Lakini isipokuwa ukiruka sana, hii kwa ujumla haiwezi kuwa shida.

Ikiwa wewe ni mjamzito au una matatizo mengine, bado ni bora kushauriana na daktari wako kabla ya kuruka.

Baadhi ya tahadhari za kawaida zinahitajika kuchukuliwa, kama vile kunawa mikono mara kwa mara, kuvaa barakoa, na kutosafiri ikiwa unajisikia vibaya.

Kwa kifupi, utafiti kuhusu jinsi mwili wa binadamu unavyoweza kuguswa na safari ndefu za ndege za moja kwa moja kati ya Australia na Ulaya bado uko katika hatua zake za awali, na timu ya Australia kwa sasa inashughulikia hilo.

Hadi matokeo yawepo, ushauri wa kushughulika na safari za ndege za masafa marefu ni wa moja kwa moja. Fuata vidokezo vya shirika la ndege na, ikiwa ni lazima, umuone daktari kabla ya kusafiri.

Wakati wa safari ya ndege, fanya jitihada za ziada kuzunguka, kunywa maji mengi, kuvaa barakoa, na kudumisha tabia nzuri za usafi za kunawa mikono mara kwa mara.

Tafuta matibabu ya haraka ikiwa utapata dalili zozote za kutisha baada ya safari ya ndege, kwani inaweza kuchukua saa, ikiwa si siku, kwa donge la damu kujitengeneza, kukua na kusafiri kupitia mshipa wa damu.

BBC
 
Back
Top Bottom