Safari zimemfanya Tyson apate chanjo ya Corona

Safari zimemfanya Tyson apate chanjo ya Corona

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
Gwiji wa ngumi za kulipwa, Mike Tyson amepata chanjo dhidi ya ugonjwa wa virusi vya corona, Covid-19, lakini amesema hakufanya hivyo kwa hiari akieleza kuwa umuhimu kusafiri ndio umemlazimisha.

"I didn't do it willingly," Tyson alisema bondia huyo mwenye miaka 55 akikaririwa na tovuti ya Washington Examiner Jumanne.

"Nina woga kidogo na hilo. Nilijikuta nalazimika kusalimu amri kwa sababu nina safario kimataifa. Na kama sisafiri, hatuli."

Bondia huyo aliyetamba katika ngumi za uzito wa juu duniani aliwahi kuambukizwa Covid-19 wakati wa janga hilo, lakini anasema anajisikia vizuri kwa sasa.

"Naweza kuwa niliupata, lakini najisikia vizuri sasa," tovuti hiyo inamkariri Tysion alipoongea na gazeti la USA Today Sports katika mahojiano yaliyofanyika katika ofisi za kampuni yake inayojihusisha na biashara ya bidhaa zitokanazo na bangi.

"Najisikia vizuri kuliko wakati mwingine wowote."

Mwananchi
 
Back
Top Bottom