Safina ya Nuhu ni mfano bora wa ukombozi kupitia kwa Yesu Kristo

Safina ya Nuhu ni mfano bora wa ukombozi kupitia kwa Yesu Kristo

Dr Adam Francis

JF-Expert Member
Joined
Aug 12, 2011
Posts
790
Reaction score
1,316
Wanadamu wote wametenda dhambi na wanastahili hukumu ya Mungu.
Katika Mwanzo 6:5-7 twasoma "BWANA akaona ya kuwa maovu ya mwanadamu ni makubwa duniani na kwamba kila kusudi analowaza moyoni mwake ni baya tu sikuzote. BWANA akaghairi kwa kuwa amemfanya mwanadamu duniani, akahuzunika moyo. BWANA akasema, Nitamfutilia mbali mwanadamu niliyemwumba usoni pa nchi; mwanadamu na mnyama, na kitambaacho na ndege wa angani; kwa maana naghairi ya kwamba nimewafanya"

Wokovu ni kwa neema kwa njia ya Imani
Katika Mwanzo 6:8,13-14 twasoma "Lakini Nuhu akapata neema machoni pa BWANA. Mungu akamwambia Nuhu, Mwisho wa kila mwenye mwili umekuja mbele zangu; kwa sababu wameijaza dunia dhuluma, basi nitawaharibu pamoja na dunia. Ujifanyie safina ya mti wa mvinje; fanya na vyumba ndani ya safina, ukaifunike ndani na nje kwa lami"

Waebrania 11:7 "Kwa imani Nuhu akiisha kuonywa na Mungu katika habari za mambo yasiyoonekana bado, kwa jinsi alivyomcha Mungu, aliunda safina, apate kuokoa nyumba yake. Na hivyo akauhukumu makosa ulimwengu, akawa mrithi wa haki ipatikanayo kwa imani"

Waefeso 2:8-9 Kwa maana mmeokolewa kwa neema, kwa njia ya imani; ambayo hiyo haikutokana na nafsi zenu, ni kipawa cha Mungu; wala si kwa matendo, mtu awaye yote asije akajisifu.

Njia pekee ya wokovu ni kuwa ndani ya Safina ambayo ni yesu Kristo
Katika Mwanzo 7:1,7,16,18,23 twasoma "BWANA akamwambia Nuhu, Ingia wewe na jamaa yako yote katika safina; kwa maana nimekuona wewe u mwenye haki mbele zangu katika kizazi hiki. Nuhu akaingia katika safina, yeye, na wanawe, na mkewe, na wake za wanawe pamoja naye; kwa sababu ya maji ya gharika. Na walioingia, waliingia mume na mke, wa kila kitu chenye mwili, kama vile alivyomwamuru Mungu; BWANA akamfungia. Maji yakapata nguvu, yakazidi sana juu ya nchi; na ile safina ikaelea juu ya uso wa maji. Kila kilicho hai juu ya uso wa nchi kikafutiliwa mbali tangu mwanadamu hata mnyama wa kufugwa, na kitambaacho, na ndege wa angani; vilifutiliwa mbali katika nchi, akabaki Nuhu tu, na hao walio pamoja naye katika safina"

Yohana 3:16,18 "Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele. Amwaminiye yeye hahukumiwi; asiyeamini amekwisha kuhukumiwa; kwa sababu hakuliamini jina la Mwana pekee wa Mungu"

Matendo ya Mitume 4:12 "Wala hakuna wokovu katika mwingine awaye yote, kwa maana hapana jina jingine chini ya mbingu walilopewa wanadamu litupasalo sisi kuokolewa kwalo"

Warumi 8:1 "Sasa, basi, hakuna hukumu ya adhabu juu yao walio katika Kristo Yesu"

Na sisi je! Tutapataje kupona, tusipojali wokovu mkuu namna hii?
2 Petro 2:4-6Kwa maana ikiwa Mungu hakuwaachilia malaika waliokosa, bali aliwatupa shimoni, akawatia katika vifungo vya giza, walindwe hata ije hukumu;
wala hakuuachilia ulimwengu wa kale, bali alimhifadhi Nuhu, mjumbe wa haki, na watu wengine saba, hapo alipoleta Gharika juu ya ulimwengu wa wasiomcha Mungu;
tena akaihukumu miji ya Sodoma na Gomora, akiipindua na kuifanya majivu, akaifanya iwe ishara kwa watu watakaokuwa hawamchi Mungu baada ya haya;

Luka 17:26-30 "Na kama ilivyokuwa siku za Nuhu, ndivyo itakavyokuwa katika siku zake Mwana wa Adamu. Walikuwa wakila na kunywa, walikuwa wakioa na kuolewa, hata siku ile Nuhu aliyoingia katika safina, gharika ikashuka ikawaangamiza wote.
Na kadhalika, kama ilivyokuwa katika siku za Lutu, walikuwa wakila na kunywa, walikuwa wakinunua na kuuza, wakipanda na kujenga;
lakini siku ile Lutu aliyotoka Sodoma kulinyesha moto na kibiriti kutoka mbinguni vikawaangamiza wote. Hivyo ndivyo itakavyokuwa siku ile atakayofunuliwa Mwana wa Adamu.
 
Hakuna ushahidi wa gharika ya dunia nzima kuwahi kutokea duniani, Ile ilikuwa hadithi ya kutunga tu
 
Hakuna ushahidi wa gharika ya dunia nzima kuwahi kutokea duniani, Ile ilikuwa hadithi ya kutunga tu
wewe sio wa kwanza mkuu walikuwepo waigiriki wanaosadikika ndio wenye uwezo mkubwa wa kuhoji katika kuchunguza, Waliitwa waberoya waliisha maliza hili swala, Chukua muda kujielimisha.
 
Back
Top Bottom