SoC04 Safisha eneo lako Dar iwe safi

SoC04 Safisha eneo lako Dar iwe safi

Tanzania Tuitakayo competition threads

pute kitogo

Member
Joined
Apr 26, 2024
Posts
6
Reaction score
3
SAFISHA ENEO LAKO DAR IWE SAFI

Hapo zamani za kale ilijulikana kama mzizima ila kwa sasa hivi inaitwa Dar es salaam ni mkoa wa nchini ya Tanzania pia ni moja wapo la jiji la Tanzania, inawakazi wengi sana kuliko mkoa mwengine wowote Tanzania na ni mkoa mdogo kieneo ukilinganisha na mikoa mingine, makao makuu ya nchi yalikuwa hapa kabla ya kuhamishiwa Dodoma ila cha kushangaza ni mkoa unaongoza kwa uchafu.

Ajabu sasa mkoa wa Dar es salaam hakuna eneo ambalo halina mwenyewe maeneo yote yanawenyewe swali la kujiuliza kwa nini ni chafu? Wakazi wa Dar tunasubiri kitu gani? au jambo gani? Kuifanya Dar iwe safi tunasubiri madaraja?, barabara za angani? au Njia 20 za barabara, kwenda kumi kurudi kumi najiuliza tunasubiri nini?? Dar iwe safi maana kwa uchafu huu wengi wameathirika wapo waliokufa kwa kipindupindu.

Natumia maneno makali kwani? Basi samahani nataka unielewe turudi juu hapo, sio juu mawinguni kwenye nyota na mwezi hapana juu hapo ukitoka aya ya pili ya makala hii na itafuata ya kwanza inayofuatia tena ni kichwa cha makala hii inasomeka hivi nirudie SAFISHA ENEO LAKO DAR IWE SAFI natamani iwe kampeni ya kulifanya jiji la Dar es salaam kuwa safi kwa sababu kila eneo la Dar linawenyewe na asilimia kubwa ya wakazi wa jiji hili kila mkazi anaeneo lake eneo hilo laweza kuwa la kupanga au la kwake na eneo hilo linaweza kuwa la kufanyia kazi yani ofisini kwake au la yeye kuishi.

Ndugu zangu wakazi wa Dar es salaam kwa nini hatusafishi, hatufanyi usafi wa maeneo yetu??, ila tunavaa tunapendeza! tunanukia! majumba yetu na ofisi zetu ni zuri kwa ndani ila nje mtihani pachafu kama eneo lako linauzio basi utasafisha ndani ya uzio ila nje ya uzio ni pachafu unataka aje Mkuu wa mkoa, Mkuu wa wilaya, Mbunge wa Jimbo lako, Mwenyekiti wa chama chako cha siasa, aje mchezaji wa mpira unayempenda, Rais au Mwenyekiti wa klabu yako, Supastaa wako, Mtendaji wa kata yako au Mwenyekiti wako wa Mtaa aje kufanya usafi?? Au unataka nani afanye usafi?

Mimi nina imani bila ya kulazimishwa na mtu yoyote kwa hiyali yetu tukiamuwa kwa kushirikiana kwa kila mkazi wa Dar tunaweza kuifanya Dar iwe safi kabisa kwanza tukikubali kufanya yafuatayo

• Tuwe tunafanya usafi kila siku na usafi utafanywa kwa vipindi viwili asubuhi na jioni, kama unakazi yingi sio tatizo muajiri mtu awe anakufanyia usafi

• Kama mtu atakata au akachafua mazingira bila kujali hakujua au vipi atatakiwa kulipa faini eneo lako likikutwa chafu unapigwa faini au ukichafua mazingira ukikamatwa utapigwa faini

• Serikali ya mkoa wafanye maamuzi ya kuwaweka maafisa mazingira kwa kila mtaa wao watakuwa na majukumu ya kusimamia usafi na kufanya usafi kwa kulipwa pesa tena ili wasimamiwe vizuri watu hawa waajiriwe na walipwe pesa zuri ili wasimamie vizuri jambo hili

• Walipwe mishahara je hiyo mishahara zitatoka wapi ? Zitatoka kwenye faini na pesa za kusafisha eneo kwa yule atakayetaka kusafishiwa eneo lake, faini ziwe kubwa ili watu waogope kuchafua mazingira na itasaidia kulipa mishahara

• Ili kampeni hii iende vizuri Serikali inatakiwa kushirikiana na vyombo vya habari vyote hadi vya mtandaoni ili kutoa elimu ili watu wasafishe maeneo yao kwa kupenda bila kulazimishwa vyombo vya habari wanaweza hili kwa kuweka matangazo mbalimbali ya kuhamasisha kampeni hii kama vile KUWA MZALENDO SAFISHA ENEO LAKO, IPENDE FAMILIA YAKO SAFISHA ENEO LAKO AU IPENDE FAMILIA YAKO WAEPUSHE NA MARADHI YANAYOTOKANA NA UCHAFU SAFISHA ENEO LAKO na zingine yingi

• Kuwatumia watu maarufu kuwa mabalozi wa Usafi kwa kutumia umaarufu wao kupitia akaunti zao za mitandao ya kijamii kuhamasisha kufanya usafi kwa hiyali, watajirekodi video kwa kusema "NAMPENDA MAMA YANGU, BABA YANGU, MKE WANGU NA WATOTO WANGU PAMOJA NA TAIFA LANGU NAWALINDA NA MARADHI YANAYOTOKANA NA UCHAFU BILA KULAZIMISHWA NASAFISHA ENEO LANGU" hii ni mfano ya kuhamasisha kufanya usafi

• Matamasha ya Usafi kutakuwa na wasanii wa kuimba na kuchekesha ili kuendelea kuhamasisha watu kufanya Usafi kwa kupenda bila kulazimishwa hii nayo itasaidia jiji la Dar es Salaam kuwa safi na kupandikiza tabia ya kusafisha maeneo yetu kila siku kwa ajili kulinda na kutunza afya zetu na mazingira yetu pia matamasha haya yatalenga kuhamasisha kufanywa usafi sehemu zile za muhimu mfano Fukwe za bahari, Mto na Masoko maan sehemu hizi zinaongoza kwa uchafu

FAIDA
• Kampeni hii nayo italeta ajira za kudumu (muda mrefu) baada ya hao maafisa mazingira pindi wakiajiliwa zitaongeza ajira pia itaongeza kodi kwa sababu watu hao wakipata mishahara watanunua bidhaa mbalimbali pia watafanya mihamala zote hizo zitaongeza kodi kwenye nchi yetu.

• Kuondoa magojwa ya uchafu kama kipindupindu
Kuongeza maeneo ya kuchukulia video (location) ambazo zinatumiwa kwenye filamu, tamthilia na kwenye mziki pindi msanii akitaka kutoa video ya wimbo wake
HASARA

• Migogoro pindi hatua za kisheria zikichukuliwa kwa mtu asiyefuata maelezo

Inawezekana labda mawazo yangu sio sawa ila natumaini kwa ambaye ataweka muda wake wa thamani akasoma kuanzia mwanzo hadi mwisho basi atapata kitu anaweza akapata wazo la kufanya jiji letu la Dar es salaam likawa safi kila sehemu.

Natumaini kiongozi utakayesoma hapa basi nakuomba tafute mbinu zaidi kulifanya jiji hili kuwa safi na tukifanikiwa kulifnya jiji la Dar es salaam likawa safi basi natumaini mikoa na majiji mengine nayo yatakuwa masafi na salama

Safisha eneo lako dar iwe safi Usafi ni afya Safisha ujikinge na magojwa Kipindupindu hadi malaria Eneo lako likiwa chafu wewe utaumwa Naukipotezea unaweza kufa

Jiji likipendeza uwekezaji utaongezeka Pesa zitamiminika maendeleo yatakuja Dar kama ulaya video hapa hapa bongo Hakuna haja ya kwenda South Africa Tunasafisha eneo letu kuonyesha tunaweza
 
Upvote 2
Mimi kama mdau wa suala zima la uwajibikaji ninakuunga mkono kabisa.

Usafi unaanza na mtu mmoja mmoja, familia mkoa kisha taifa kwa ujumla.

Tatizo linakuja kwenye wajibu wa muhusika. Mfano taka zikikutwa kwenye mtaro mbele ya nyumba yako anapaswa ashtakiwe nani? Maana huyu wa mtaa wa pili atataka lisafishwe na aliyeziweka taka humo mtaroni wa mtaa wa kwanza maji yalikoanzia. Na binafsi ninaona ni haki tu.

Maeneo ambayo tunayamiliki wote kupitia serikali, basi tuyasafishe wote kupitia tenda kwa makampuni yatakayolipiwa na wote kupitia kodi ushuru na tozo.

Hapo sasa linakuja suala la kuumiliki uchafu kwa jamii nzima. Napendekeza maeneo yanayomilikiwa na umma kama madaraja na mitaro na barabara. Zipewe kandarasi kuanzia usafi hadi ulinzi wa usafi wake. Na hai maafisa mazingira na serikali watasimamia utaratibu huo wa zabuni na tenda.

Nasema hivyo kwa sababu, hata sasa hizo tenda zipo na zinatolewa swali linabaki kuwa je? Kila muhusika anatimiza majukuku yake?
 
Mimi kama mdau wa suala zima la uwajibikaji ninakuunga mkono kabisa.

Usafi unaanza na mtu mmoja mmoja, familia mkoa kisha taifa kwa ujumla.

Tatizo linakuja kwenye wajibu wa muhusika. Mfano taka zikikutwa kwenye mtaro mbele ya nyumba yako anapaswa ashtakiwe nani? Maana huyu wa mtaa wa pili atataka lisafishwe na aliyeziweka taka humo mtaroni wa mtaa wa kwanza maji yalikoanzia. Na binafsi ninaona ni haki tu.

Maeneo ambayo tunayamiliki wote kupitia serikali, basi tuyasafishe wote kupitia tenda kwa makampuni yatakayolipiwa na wote kupitia kodi ushuru na tozo.

Hapo sasa linakuja suala la kuumiliki uchafu kwa jamii nzima. Napendekeza maeneo yanayomilikiwa na umma kama madaraja na mitaro na barabara. Zipewe kandarasi kuanzia usafi hadi ulinzi wa usafi wake. Na hai maafisa mazingira na serikali watasimamia utaratibu huo wa zabuni na tenda.

Nasema hivyo kwa sababu, hata sasa hizo tenda zipo na zinatolewa swali linabaki kuwa je? Kila muhusika anatimiza majukuku yake?
Tukiamuwa tunaweza ila kila jambo linatakiwa kuwekewa Sheria na kanuni tunaweza serikali ikiamuwa
 
Back
Top Bottom