Wonderful
JF-Expert Member
- Apr 8, 2015
- 7,347
- 5,986
MFANYABIASHARA maarufu nchini, Yussuf Mehboob Manji ataendelea kuiongoza Yanga kwa miaka mingine minne, baada ya kutetea nafasi yake katika uchaguzi uliofanyika jana ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar es Salaam.
Manji ambaye hakuwa na mpinzani, ameshinda kwa kukusanya zaidi ya asilimia 90 ya kura, huku Makamu wake, Clement Sanga akifanikiwa pia kutetea nafasi yake kwa kumshinda mpinzani pekee, Tito Osoro.
Sanga amekusanya zaidi ya asilimia 80.
Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano ya Yanga, Jerry Muro amesema Manji ametangazwa mshindi baada kupata kura 1, 468 kati ya 1,470 zilizopigwa huku kura mbili tu zikiharibika na hakukuwa na kura ya hapana.
Muro amesema Sanga ameibuka mshindi baada ya kujizolea kura 1, 428 kati ya 1,508 zilizopigwa, huku mpinzani wake wake pekee, Osoro akiambulia kura 80 tu.
Walioshinda nafasi za Ujumbe wa Kamati ya Utendaji ni Siza Augustino Lymo kura 1027, Omary Said Amir kura 1069, Tobias Lingalangala kura 889, Salum Mkemi kura 894, Ayoub Nyenzi kura 889, Samuel Lukumay kura 818, Hashim Abdallah kura 727 na Hussein Nyika kura 770.