Sagini ameagiza TANESCO na REA kueleza vigezo vinavyotumika kuunganisha umeme kwa Sh 350,000/-

Sagini ameagiza TANESCO na REA kueleza vigezo vinavyotumika kuunganisha umeme kwa Sh 350,000/-

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
5,352
Reaction score
15,876
WhatsApp Image 2025-03-29 at 18.32.26_8f9b0806.jpg
Mbunge wa Jimbo la Butiama na Naibu Waziri wa Katiba na Sheria, Jumanne Sagini ameagiza watumishi wa Shirika la Umeme (TANESCO) na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) Wilaya ya Butiama kutoa elimu kwa wananchi wa Sirorisimba juu ya vigezo vilivyotumika mpaka kufikia kutoa huduma kwa shilingi 350,000/= badala ya 27000/- kama ilivyoelekezwa.

Maagizo hayo ameyatoa wakati alipokuwa Ziara ya Kusikiliza na Kutatua kero za wananchi na Viongozi wa CCM kwenye Matawi ya Kitaramanka, Rwasereta, Nyambili na Sirorisimba ambapo alipokea malalamiko kutoka kwa kwa wananchi yakituhumu TANESCO na REA kutowapa gharama za uhalisia pale wanapohitaji kuunganishiwa Umeme.

"Tumekuwa tukishirikiana vyema TANESCO na REA hapa Jimboni kwangu kila kijiji kimefikiwa na umeme kilichochabakia ni baadhi ya vitongoji hivyo niwaombe TANESCO kutolea ufafanuzi malalamiko haya yanayokuwa mwiba kwa mwananchi pale wanapohitaji kuunganishwa na umeme," amesema Sagini.
WhatsApp Image 2025-03-29 at 18.32.29_b235392d.jpg
Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Sirorisimba, Juma Sendi amempongeza Mbunge Sagini kwa juhudi anayofanya ya kusambaza maendeleo kwa wananchi jimboni kwani mpaka sasa kazi aliyofanya inaonekana ikiwemo ujenzi wa Shule ya Sekondari Sirorisimba
 
Inatafutwa pesa ya iptl ndugu watanzania tuwe waelewa
 
27,000 hadi 350,00 mwananchi wa kijijini anamudu vipi hizo gharama. Mbona kwa miaka 4 gharama ilibaki za 27,000.

Lengo ni kweli kuwasaidia wananchi au upigaji, kutojali maisha ya Watanzania.
 
  • Thanks
Reactions: vnn
27,000 hadi 350,00 mwananchi wa kijijini anamudu vipi hizo gharama. Mbona kwa miaka 4 gharama ilibaki za 27,000.

Lengo ni kweli kuwasaidia wananchi au upigaji, kutojali maisha ya Watanzania.
Hamieni Namibia,mkutane na secretary mwingine kule
 
Hamieni Namibia,mkutane na secretary mwingine kule
Huyo wa Namibia ni Mzalendo, amezaliwa nchini kwake. Amepigania uhuru na ni msomi wa ukweli sio elimu ya kuungaunga. Mme wake alikuwa mkuu wa majeshi. Wote walipambana Namibia kuwa huru.
 
Mbunge wa Jimbo la Butiama na Naibu Waziri wa Katiba na Sheria, Jumanne Sagini ameagiza watumishi wa Shirika la Umeme (TANESCO) na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) Wilaya ya Butiama kutoa elimu kwa wananchi wa Sirorisimba juu ya vigezo vilivyotumika mpaka kufikia kutoa huduma kwa shilingi 350,000/= badala ya 27000/- kama ilivyoelekezwa.
Sasa na yeye serikali anashangaa badala ya kutumia nafasi yake kuwasiliana na waziri mwenye dhamana
 
Back
Top Bottom