Sahihi Serikali kuongeza ndege nyingine tano ilihali huduma za afya bado zipo duni?

Nyankurungu2020

JF-Expert Member
Joined
Oct 2, 2020
Posts
4,170
Reaction score
6,757
Nimeona kwenye news kuwa serikali imefanya malipo ya ndege tano mpya. Dreamliner moja, boeing 737-9 mbili na Dash 8 q 400 moja. Malipo haya kwa haraka haraka yanakadiliwa kugharimu zaidi ya tril 1.8.

Kwa jinsi watanzania wanavyohangaika kupata huduma za afya ni bora pesa hizi zingewekezwa kwenye kubaoresha upatikanaji wa huduma za afya na vifaa tiaba kuliko kuongeza idadi ya ndege zisizo na tija kwa raia wa kawaida

Wachumi wa CCM wanatuangusha sana.
 
Wakati ananunua magufuli mlikuwa mkisifia sana. Akinunua Samia anakosea.
 
Alipinunua yule mropokaji wa wanyonge mlishangilia sana Ila wengine ndio hazina umuhimu. Watu walijaa airport mpaka wakaingia kwenye runway na ikashangiliwa sana kisa waione ndege ya Meko. Kunya anye kuku akinya Bata kaharisha.
 
Mkuu kabla sijajibu hii hoja yako naomba unifafanulie nini maana ya HUDUMA duni za afya
 
 
Alipinunua yule mropokaji wa wanyonge mlishangilia sana Ila wengine ndio hazina umuhimu. Watu walijaa airport mpaka wakaingia kwenye runway na ikashangiliwa sana kisa waione ndege ya Meko. Kunya anye kuku akinya Bata kaharisha.
 
Rais wa awamu ya 6,Mama yetu tafadhali nunua ndege zifike 50 maana haiwezekaniki vinchi vidogo tulingane navyo idadi ya ndege kwny mashirika Yao ya ndege na Nashauri destination ziendelee kua hizo hizo 3 tulizonazo Wala tusiongeze nyingine maana sisi Ni donor country,we're doing this for fun.
 
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…