Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
MASAHIHISHO PICHA TAWI LA TANU: DUA NYUMBANI KWA ALI MSHAM SAFARI YA UNO 1955
Hapo chini ni picha ya Mtaa wa Jaribu Magomeni Mapipa nyumbani kwa Ali Msham ambako alifungua tawi la TANU mwaka wa 1955.
Huo si Mtaa wa Congo mwaka wa 1920.
Siku hii ni February 1955 Nyerere alikuwa anakwenda UNO kwa mara ya kwanza na huo umma uliofurika hapo ni kuwa hapo nyumbani kwa Ali Msham lilipo tawi la TANU palifanyika dua ya kumuombea Nyerere salama katika safari ile.
Ukiangalia vizuri hii picha mkono wa kulia nyumba ya kwanza kuna watu wamevaa kanzu na koti wamekaa barazani wanafanya kisomo.
Wanae Ali Msham wamenieleza historia ya baba yao na uhusiano wake na Mwalimu Nyerere na Mama Maria walipohamia Magomeni uhusiano uliodumu hadi Tanganyika ilipopata uhuru wake mwaka wa 1961.
Naishukuru familia hii kwa kunipa picha nyingi za baba yao wakati anapigania uhuru wa Tanganyika na kuniruhusu nizitumie nipendavyo.
Mfaume Ali Msham nje ya nyumba yao ambayo baba yake alifungua tawi la TANU wakati wa kupigania uhuru wa Tanganyika.