Said Khamis Jr, rafiki wa nyavu ughaibuni

Albinoomweusi

JF-Expert Member
Joined
Oct 28, 2016
Posts
3,433
Reaction score
8,585
Kinda Mtanzania Said Khamis jana amerudi kambani mara tano kitaalam tunaita GLUT (Mabao matano) akiisaidia klabu yake ya Baniyas Sports kuendelea kutamba dhidi ya Zafra FC

Katika hizo bao tano kuna Perfect Hatrick imepigwa, limepigwa bao la mguu wa kushoto, limepigwa bao la mguu wa kulia na limepigwa bao la kichwa, Said kwenye form bora kabisa.

Kwa idadi hiyo ya mabao anasogea mpaka mabao 20 kwenye orodha ya Wafungaji kwenye ligi yao na anaemfuata ana mabao 15 wakiwa wamesalia na mchezo mmoja pekee, Kijana anaongoza orodha ya wacheka na nyavu.

Bila shaka mwishoni mwa msimu pia atapokea kiatu chake cha ufungaji bora, upepo unaendelea kuvuma kutoka Mashariki ya kati mpaka nyumbani, ujumbe unatumwa kuwa yupo tayari.


 
Yupo daraja la ngapi? Wasifu wake na umri?
 
Unaandika habari husemi anacheza ligi gani,daraja la ngp,nchi gani au ughaibuni nayo ni nchi?
 
Huyu dogo tangu yupo mbao fc alikuwa ni fundi wa kucheka na nyavu. Hivyo anastahili. Yule mwenzake mwingine sijui yuko wapi kwa sasa (somebody Habib Kiombo)!

Nae alikuwa na kipaji cha hali ya juu sana kabla ya kuandamwa na majeraha na hivyo kupotelea kusiko julikana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…