Albinoomweusi
JF-Expert Member
- Oct 28, 2016
- 3,433
- 8,585
Kinda Mtanzania Said Khamis jana amerudi kambani mara tano kitaalam tunaita GLUT (Mabao matano) akiisaidia klabu yake ya Baniyas Sports kuendelea kutamba dhidi ya Zafra FC
Katika hizo bao tano kuna Perfect Hatrick imepigwa, limepigwa bao la mguu wa kushoto, limepigwa bao la mguu wa kulia na limepigwa bao la kichwa, Said kwenye form bora kabisa.
Kwa idadi hiyo ya mabao anasogea mpaka mabao 20 kwenye orodha ya Wafungaji kwenye ligi yao na anaemfuata ana mabao 15 wakiwa wamesalia na mchezo mmoja pekee, Kijana anaongoza orodha ya wacheka na nyavu.
Bila shaka mwishoni mwa msimu pia atapokea kiatu chake cha ufungaji bora, upepo unaendelea kuvuma kutoka Mashariki ya kati mpaka nyumbani, ujumbe unatumwa kuwa yupo tayari.