Said Salim Bakhresa akamata nafasi ya 30 katika orodha ya watu matajiri 40 barani Afrika – Forbes

Said Salim Bakhresa akamata nafasi ya 30 katika orodha ya watu matajiri 40 barani Afrika – Forbes

Money Stunna

JF-Expert Member
Joined
Aug 9, 2011
Posts
13,053
Reaction score
6,304
Bakhresa.jpg

Bakhresa (kulia) alipokuwa akisalimiana na rais wa Zanzibar Ali Mohamed Shein

Orodha ya jarida la Forbes la watu 40 matajiri zaidi barani Afrika imetupa jibu la ‘uhakika' nani ni mtu tajiri zaidi kuliko wote nchini Tanzania. Si mwingine zaidi ya Said Salim Bakhresa ambaye amekamata nafasi ya 30 kati ya matajiri 40 wa barani Afrika kwa kuwa na utajiri unaofikia dola milioni 520 hadi kufikia November, 2012.

Bakhresa ana historia ya pekee kwa kuacha shule akiwa na miaka 14 na kujiingiza kwenye biashara ndogo ndogo ikiwa pamoja na mgahawa na biashara ya unga wa kusaga. Leo hii Bakhresa Group imeajiri zaidi ya watu 2,000 na ni kampuni kubwa zaidi Tanzania. Bidhaa zake zina umaarufu mno nchini na nje ya nchi ambazo ni pamoja na unga, vinywaji, ice cream, usafiri wa meli na mafuta miongoni mwa nyingine.

Kampuni ya Bakhresa ni wazalishaji wakubwa zaidi wa unga wa ngano Afrika Mashariki na kati ambayo huzalisha kiasi cha 3,200 za tani za metric. Kampuni yake huendeshwa na wanae wa kiume waliogawana vitengo mbalimbali.

Angalia list nzima hapa:
Africa
 
Hongera Bakheresa!!! Watoto wetu wakisoma hapa wasije wakaacha shule at 14 wakijua ni kama zamani!!! Again, umefanya makubwa kwa uchumi wa Tanzania na Afrika kwa ujumla (hasa East and Central Afrika).
 
Hongera sana SSB, nadhani utakuwa unaongoza kwa mbalii ulipaji kodi haapa nchini.
 
Swali ni Je, kodi anayolipa inaendana na kipato chake anachoingiza?
 
Cha kushangaza tajiri huyo huyo hayupo kwenye hata 20 bora ya walipa kodi wa nchi hii. Nina mpango wa kuanzisha compaign ya kwenye watu waache kununua bidha za makampuni ambayo hayalipi kodi stahiki na yanaongoza kuwanyonya wananchi.
Baadhi ni haya Hapa upande wa:

mazao: Export Trading, Mohamed Enterprises, Patel Export, Bakhressa Food Products.

Upande wa uzalishaji & Usindikaji: chemi & Cotex, Morogoro Canvas, Alluminium Africa, Rafian Bag, Bakhresa group of companies,

Telephone: Vodacom, tigo & Airtel
 
Utamuonea bure!Umeambiwa anaviwanda hadi nje ya nchi lakini collectively ndiyo anahela ndefu!Kwahiyo usikariri kuwa mapato yake yote yanatokea tanzania maana unawezakukuta kwa investment zake za bongo peke yake wapo wanaomburuza so siajabu kutokuwepo ktk orodha ya walipa kodi bora 20 hapa nchini.

Au kama una-data za kuthibitisha madai yako basi tuwekee jamvini na sisi tujionee.
 
yani huyu jamaa simuoni ktk mambo ya kijamii mfano kujenga shul, hospital nk alafu hata kwenye list ya walipa kodi wazuri hayupo
utazani utajiri wake wa mapepo hapo ndo simuelewagi huyu tajiri asiye enda shule sijui wenzangu mnamuonaje huyu tajiri wa kitanzania ?
 
Kwa wanaolipa kodi kashika nafasi ya ngapi??

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
Ni barani Afrika lakini hawa tycoons robo tatu ni ngozi nyeupe!
 
halafu huu mfumo kristu mbaya sana

kama sio mfumo kristu huyu jamaa angekua tajiri dunia nzima:becky::becky::becky::becky::becky:
 
yani huyu jamaa simuoni ktk mambo ya kijamii mfano kujenga shul,hospital nk
alafu hata kwenye list ya walipa kodi wazuri hayupo
utazani utajiri wake wa mapepo
hapo ndo simuelewagi huyu tajiri asiye enda shule
sijui wenzangu mnamuonaje huyu tajiri wa kitanzania ?

Huyu ni katika wale wanaosaidia bila kujionyesha ni mara moja moja
kuonekana kwenye TV akitoa misaada na hapendi iwe hivyo kama mimi
na wewe ambao tunataka hata ukitoa kuku kwa watoto yatima uonyeshwe
kwenye TV.
 
Cha kushangaza tajiri huyo huyo hayupo kwenye hata 20 bora ya walipa kodi wa nchi hii. Nina mpango wa kuanzisha compaign ya kwenye watu waache kununua bidha za makampuni ambayo hayalipi kodi stahiki na yanaongoza kuwanyonya wananchi.
Baadhi ni haya Hapa upande wa:

mazao: Export Trading, Mohamed Enterprises, Patel Export, Bakhressa Food Products.

Upande wa uzalishaji & Usindikaji: chemi & Cotex, Morogoro Canvas, Alluminium Africa, Rafian Bag, Bakhresa group of companies,

Telephone: Vodacom, tigo & Airtel
Pia mishahara ya wafanyakazi wake mmhh,kuna wakati waliwahi kulalamika kuwa wanalipwa viduchu
 
Back
Top Bottom