GE2025 Said Soud: Wanzibar acheni mihemko na misukumo ya kisiasa inayoweza kuhatarisha amani na utulivu wa nchi

GE2025 Said Soud: Wanzibar acheni mihemko na misukumo ya kisiasa inayoweza kuhatarisha amani na utulivu wa nchi

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Mkalukungone Mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
3,141
Reaction score
7,205
Mgombea Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya Chama cha Wakulima (AAFP), Said Soud Said, amewataka Watanzania, hususan Wazanzibari, kuacha mihemko na misukumo ya kisiasa inayoweza kuhatarisha amani na utulivu wa nchi.

Soud ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na vyombo vya habari katika ofisi za chama hicho Kichangani, kisiwani Pemba. Amesema amani ni nguzo muhimu ya maendeleo, hivyo wanasiasa pamoja na wananchi wanapaswa kuzingatia maslahi ya taifa badala ya kugawanyika kwa misingi ya kisiasa.

Amebainisha kwamba wananchi wasikubali kuivuruga na kuichezea amani yao kwa hoja ya siasa au maandamano, kwani haileti tija bali inawea kuleta maafa makubwa na gharama kubwa. Mgombea huyo ameongeza kwamba baadhi ya nchi kama Libya, Tunisia na nyinginezo zimekumbwa na umasikini kutokana na machafuko yaliyowakumba.
 
Back
Top Bottom