Said Tewa Mtoto wa Tewa Said Tewa Atembelea Maktaba

Said Tewa Mtoto wa Tewa Said Tewa Atembelea Maktaba

Mohamed Said

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2008
Posts
21,967
Reaction score
32,074
SAID TEWA MTOTO WA TEWA SAID TEWA MUASISI WA TANU ATEMBELEA MAKTABA

Leo ndugu yangu Said Tewa mtoto wa mmoja wa wazalendo 17 walioasisi TANU kanitembelea.

Said tumekuwa pamoja Dar-es-Salaam lakini baadae Said alihamia Ulaya.
Miaka mingi sasa yuko huko lakini huja nyumbani kusalimia.

Kumuona Said Tewa Maktaba kulinipa nafasi ya kumshukuru kwani miaka kiasi miwili hivi Said akiwa nyumbani kwake Ulaya tulizungumza na nilimuomba picha za baba yake.

Nilichopokea kutoka kwake sikutegemea.
Said alinihamishia maktaba ya picha ya baba yake kuja kwangu.

Picha hizi zinaeleza historia nzima ya Tewa Said Tewa kwanza katika picha zake akiwa kijana miaka ya 1950 wakati wakipigania uhuru wa Tanganyika.

Katika maktaba ile ya picha iliyoletwa kwangu Magomeni Mapipa ikirushwa hewani fumba na kufumbua kuna picha za safari ya kwanza ya Mwalimu Nyerere China mwaka wa 1965 Mzee Tewa akiwa Balozi wa Tanzania Peking.

Picha hizi zinaeleza safari nzima ya Mwalimu Nyerere na msafara wake.

Huwa nawatazama wale viongozi walioambatana na Mwalimu nikabaki nimejiinamia.

Hakuna hata mmoja aliye hai.

Wote wametangulia mbele ya haki.
Mmoja baada ya mwingine.

Hii ni hazina kubwa ambayo huwezi kuipata popote imekusanywa mahali pamoja.

Nilichukua fursa hii ya kuwa na Said Tewa kumshukuru na pia kutabaruku na Mzee Tewa na mama yetu Bi. Zainab kwa kuwakumbuka wazazi wetu hawa na kuwaombea dua.

Nyumbani kwa Tewa Said Tewa katika miaka ya 1950 ilikuwa Mtaa wa Stanley na Swahili na nyumba yake ilikuwa jirani sana na nyumba ya Ramadhani Fundikira, Mzee Kubbe, Msikiti wa Warufiji, Ofisi ya Tanganyika Federation of Labour (TFL), nyumba ya Mzee Maleta, nyumba ya Abdul Sykes - Stanley na Sikukuu.

Nyumba hii ina historia kubwa sana katika kupigania uhuru wa Tanganyika.

Ilikuwa kama kesho TANU itakuwa na mkutano wa hadhara Mnazi Mmoja na Julius Nyerere anazungumza na wananchi leo jioni nyumbani kwa Abdul Sykes watakusanyika viongozi wa TANU kamati ya ndani kabisa - Dossa,

John Rupia, Abdul na Ally Sykes pamoja na akina mama Bibi Titi Mohamed,

Halima Khamis, Tatu bint Mzee, Hawa bint Maftah kwa kuwataja wachache kupanga nini cha kufanya kujaza uwanja.

Mnazi Mmoja ilikuwa inawaka moto.

Ukivuka Kitchwele sasa Mtaa wa Uhuru ndiyo Mtaa wa Kipata ndiyo kwetu.
Baba zetu na mama zetu wote wakijuana.

Nyumba zote hizi ni za wana TANU mume na mkewe na watoto ndiyo sisi leo tunakumbushana historia hii ya uhuru.

Hawa ndiyo waliounda TANU na kukipa nguvu chama.

Said Tewa kuja kwangu kumeufanya moyo wangu ububujikwe machozi ndani kwa ndani.

Said ndugu yangu umenikumbushe mengi na kanirejesha nyuma miaka mingi na mbali sana.

https://youtu.be/B6Am7NCxuzU?si=dm7LXncZ-WoMvfkZ\\

1719572662926.png
1719572707824.png

1719572746175.png

1719572783417.png
 
Back
Top Bottom