TangaKunani
New Member
- Sep 12, 2006
- 4
- 0
Anafanya kazi Ikulu akiwa na wadhifa gani? Na kwanini tunafikiri ni msemaji wa Ikulu? Ninachojua ni mwandishi wa habari na sijaona mahali ambapo amazungumza kwa niaba ya spika. Or am I missing sumtgn?
Saidi Yakubu ni member humu jamvini JF, aje mwenyewe ajibu hoja hizi
ni tatizo la watu wengi hapa tanzania kuchangia mada au kuongelea kitu bila ya kufamnya utafiti.hili ni kosa kubwa sana sana,ndo manake kuna msemom maarufu wa kichina wenye maana "no research no right to speak".
jengine kuna tatizo kwa vijana wetu tena wasomi kuwa na uoni mfupi wao wanamawazo madogo sana kwamba mafanikio yanapatikana ccm tuuuu,na kwamba haitatokea ccm ikadondoka ata mara moja hawa pia huwa ni wale ambao tunaweza waita pia ma opportunist (mi jitu yenye tamaa ya kupata kwa njia zozote iwe halali au haramu kwa sifa au kwa upendeleo na mara nyingi ni kwa kujipendekeza).
Nadhani huyo Said Yakub sio mwanaharakati au ni mwanaharakati maslahi.
Mkuu Kakalende,Bwana Said Yakubu alisitisha uanachama wake hapa kuanzia Mwaka jana baada ya kuona kama (Kuwa) kazi yake mpya itaingiliana maslahi na uchangiaji hapa JF...Akikubali ataingia hapa kujibu swali la Mwanachama Tangakunani kuhusu utata uliojitokeza kama ni msemaji wa Mheshimiwa Spika.
Said Yakubu ni kweli kwamba anafanya kazi na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Lakini si muajiriwa wa Bunge...Mkuu Lunyungu angalia vyanzo vyako vya habari vizuri na wala si kweli kwamba Said Yakubu ni Mfanyakazi wa Shirika la Habari la Uingereza (BBC),Alikwishaacha kazi huko na kurejea Nyumbani toka mwaka Juzi.
Baada ya kumaliza Shahada yake ya sheria ,Said aliajiriwa na Umoja wa Mabunge ya Jumuiya ya Madola, alipangiwa kazi Tanzania,na alipelekwa kwenye Ofisi ya Bunge kuangalia Mfumo na Utendaji kazi wa Bunge la Jamhuri ya Muungano.Mpaka sasa anafanya kazi hiyo.
Said ni Mwanaharakati kwa asili yake,na ni Kiongozi wa muda mrefu.....nae ni mmoja kati ya Vijana wengi wanaotajwa kuingia kwenye kinyang'anyiro cha Ubunge kwa tiketi ya CCM mwakani.
kwahiyo wana JF ukishaingia tu kwenye system unatakiwa usitishe membership yako??? Hii ni tete kidogo, inamaana hapa ni kijiweni tunasubiria what next??Mkuu Kakalende,Bwana Said Yakubu alisitisha uanachama wake hapa kuanzia Mwaka jana baada ya kuona kama (Kuwa) kazi yake mpya itaingiliana maslahi na uchangiaji hapa JF...Akikubali ataingia hapa kujibu swali la Mwanachama Tangakunani kuhusu utata uliojitokeza kama ni msemaji wa Mheshimiwa Spika.