Mkuu Kakalende,Bwana Said Yakubu alisitisha uanachama wake hapa kuanzia Mwaka jana baada ya kuona kama (Kuwa) kazi yake mpya itaingiliana maslahi na uchangiaji hapa JF...Akikubali ataingia hapa kujibu swali la Mwanachama Tangakunani kuhusu utata uliojitokeza kama ni msemaji wa Mheshimiwa Spika.
Said Yakubu ni kweli kwamba anafanya kazi na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Lakini si muajiriwa wa Bunge...Mkuu Lunyungu angalia vyanzo vyako vya habari vizuri na wala si kweli kwamba Said Yakubu ni Mfanyakazi wa Shirika la Habari la Uingereza (BBC),Alikwishaacha kazi huko na kurejea Nyumbani toka mwaka Juzi.
Baada ya kumaliza Shahada yake ya sheria ,Said aliajiriwa na Umoja wa Mabunge ya Jumuiya ya Madola, alipangiwa kazi Tanzania,na alipelekwa kwenye Ofisi ya Bunge kuangalia Mfumo na Utendaji kazi wa Bunge la Jamhuri ya Muungano.Mpaka sasa anafanya kazi hiyo.
Said ni Mwanaharakati kwa asili yake,na ni Kiongozi wa muda mrefu.....nae ni mmoja kati ya Vijana wengi wanaotajwa kuingia kwenye kinyang'anyiro cha Ubunge kwa tiketi ya CCM mwakani.