Saida Karoli: Meneja wangu amemtapeli Diamond mamilioni, mi nilimpa wimbo bure

Saida Karoli: Meneja wangu amemtapeli Diamond mamilioni, mi nilimpa wimbo bure

Sallam kama kawaida yake kampiga Saida Chenga ya mwili.

Diamond alitamba siku ile kuwa kuna hela wamempa Saida alafu Saida kaja kutoa siri kumbe aliwapa wimbo bure wao wakaenda kumpa hela meneja.

Kama kawaida yao kuongeza sifuri wapate kiki bado meneja kutoa siri kuwa nae akupewa chochote ulikuwa ujanja ujanja tu
Kwan wimbo ni mali ya saida au mali ya meneja
 
Alikuambia kuingiza sauti mpaka mue pamoja studio na nani?
Nakwambia tena saida kaloli na diamond hawakuonana na bado hawajaonana face to face tangu wimbo umetengenezwa hadi umetoka, hata saida mwenyewe process zote zinafanyika alikuwa Bukoba, nenda kasikilize interview tena uelewe vizuri.
Msaada kwako : kuna nyimbo kibao zinafanyika bila wasanii kukutana unatumiana sauti shughuli inaisha.
Kuna nyimbo Yemi Alade amemshirikisha Diamond na imeshakamilika na hawajaingia studio pamoja , diamond amefanya part yake akamtumia kila kitu kipo sawa bado kufanya Video tu.

Wewe ndio hata uelewi wapi niliposema kuwa lazima mkutane studio ndio mfanye wimbo pamoja?!

Na sio lazima Diamond akutane na Saida...Diamond ana viongozi wanne Ricardo Momo,Sallam,Tale na Fella unataka kusema Saida alivyokwenda Studio kutia sauti yake viongozi wote hawa wa Diamond hawakuwepo siku hiyo?

Maana unachotengeneza wewe ionekane kuwa Saida hakuwa anajua lolote ili mumpe kesi meneja wake kumbe na nyie mnausika kumpiga changa dada wa watu.

Jibuni hoja hizo hela alizosema Diamond alimpa Saida alimpa saida yupi na hizo 25% ambazo zinakwenda kwa mama ni mama yupi au mama ake Diamond?

Saida anazidi kuweka mambo hadharani...na umwambie baba ako Diamond tabia za kuongeza ongeza sifuri sio fresh maana sasa anaelekea kuumbuka na kuonekana tapeli.
 
Kwan wimbo ni mali ya saida au mali ya meneja
Sijui mkataba wao ukoje maana inawezekana na wimbo ukawa mali ya producer pia.

ninachosema ni kuwa Diamond alisema kampa hela Saida alafu wakamalizana na Meneja wake sasa Saida kaja kuweka wazi kuwa Yeye alitoa wimbo bure na diamond alimpa hela meneja wake na sio yeye

Sasa swala lipo hivi kwanini Diamond na uongozi wake walidanganya?
 
Acha kukurupuka, kumbe hata mwenye hakimiliki ya wimbo humjui alafu unaleta porojo?
Diamond amefuata taratibu zote zilizotakiwa na jamaa yuko makini sana
Story zako za kuongeza sifuri kawasimylie watoto wenzio wa instagram
 
Nipeni namba ya maneger nina dada yangu anatafuta mchumba mwenye angalau 20milion kwenye account yake ya bank. . maana kipindi hiki ni kigumu kiuchumi ila naona maneger kavuka kiwango.
 
Beat ni mali ya producer na wala sio saida wala meneja.....
 
“Kitu tulichokifanya kabla ya kurelease wimbo,tulizungumza na uongozi wake,tukawaambia tunafanya hiki na hiki na kuna kiasi pia tukakitoa ili kiende kwake halafu tukampa 25% ya publishing.Kila income ya publishing ikiwa inaingia katika huu wimbo,mama atakuwa anapata percent,”

Hayo yalikuwa maneno ya Diamond mwenyewe waliongea na uongozi wake alafu alafu kuna kiasi walikitoa kwenda kwake.Alafu wakampa 25% na kila senti itakayoingia mama atakuwa anapata senti...

sasa Kati yangu mimi na wewe sijui nani kakurupuka hapo.we unasema hawakuonana wakati Saida anasema alikuwepo studio na aliingiza sauti yake kwenye chorus ya ule wimbo...

Saida anasema alitoa wimbo bure akuchukua hata senti baba ako Diamond anasema walimpa hela Saida na sio Meneja wa Saida.

Muda mwingine weka mapenzi kando kwenye hili swala kuna ujanja mwingi na kuongeza sifuri ila Saida kaamua kusema basi tutasikia mengi mno round hii.
Mm nakumbuka alipokuw anaulizwa icho alisema alienda kuonana na aliyekuwa meneja wa saida karoli ndo wakapatana kuwa inabidi watoe asilimia 25 za publidhing na wakatoa kiasi kazaa cha hela kwa huyo meneja maana ndo mliki halali wa uwo wimbo.....lakini hakusema kuwa wameonana na saida mbona unajaribu kubadilisha ukweli kuwa uwongo punguza chuki ndo utapanuka kimawazo
 
Na nakumbuka kuna interview moja domo aliulizwa kuhusu hilo swala la kufaidika saida na iyo project ya Salome...domo akasema wenyewe wameonana na uongozi wa saida ule wa zamani coz ndo wamiliki halali kisheria ndo aliyewaruhusu kutoa iyo ngoma na kuna kiasi kazaa cha hela ilibidi walipe kwa huyo meneja muta ajili ya publishing na hakusema kuwa izo hela kamlipa saida karoli....cc mzaramo acha kupotosha watu ingia YouTube usikilize upya ukiona sehem kasema iyo percent walimpa saida nitag
 
Kwa maelezo hayo, hakuna aliyemdhurumu. Yeye alitoa wimbo bure kwa maana ya kwamba hataki hata senti moja. Hajapewa chochote kwa kuwa hakutaka, sasa analalamika nini? Kama meneja amepewa, Saida hana haja ya kumuonea wivu. Hiyo ni facilitation fee, yaani ni malipo ya WCB kwa meneja kwa kuwezesha Saida atoe wimbo bure. Kwenye mkataba, kila mtu anapata alichokubaliana nacho

Elimu ndogo ya Saida ndio chanzo cha yote haya. WCB wangetumia akili ya busara tu, wakamlipa chochote huyu mama. Kama alivyoongea mwenyewe, anaamini akitoa wimbo wake kwa msanii mwingine itasaidia ainuke, ni mtazamo wake kwa elimu aliyonayo. Ukijua hili, unampa tu kitu kidogo kama ruzuku maana mwisho wa siku wimbo ni wake na wewe umeuchakachua kwa style yako. Wasanii na meneja wake wa zamani wasitumie advantage ya ku benefit kwa mgongo wake only kwa sababu elimu yake ni ndogo. This is not fair kabisa
 
Huyo meneja aitwa Felician Muta, namchukia sana huyo mzee tangu alivyomwingiza kingi na kumsainisha saida mikataba ya Mangungo huku akitumia fursa ya kutokujua kusoma wala kuandika kwa Saida hapo mwanzoni.
Huyo Muta (FM) alikua anamiliki Silent Inn na FM Music band (kuna waliostukaga na kujitoa wakaanzisha FM Academia. Nadhani ndio ngwasuma ya sasa).

Pia alikua anamiliki FM Music Studio akirekodi kanda za bolingo sana. Baadae niliskia kaokoka baada ya sailentini kuvunjwa.

Hakuna alichoanzisha ambacho haikua magumashi. Labda hiyo studio ila sina hakika km alikua na rights kurekodi zile kanda.
 
Elimu ndogo ya Saida ndio chanzo cha yote haya. WCB wangetumia akili ya busara tu, wakamlipa chochote huyu mama. Kama alivyoongea mwenyewe, anaamini akitoa wimbo wake kwa msanii mwingine itasaidia ainuke, ni mtazamo wake kwa elimu aliyonayo. Ukijua hili, unampa tu kitu kidogo kama ruzuku maana mwisho wa siku wimbo ni wake na wewe umeuchakachua kwa style yako. Wasanii na meneja wake wa zamani wasitumie advantage ya ku benefit kwa mgongo wake only kwa sababu elimu yake ni ndogo. This is not fair kabisa
Hilo ungemwambia FM maana kamnyoosha Saida tangu zamani sana. Saida aliambulia Mark 2 na kupangushiwa nyumba Sinza. Wahaya wengi kwa kupenda dhuluma hawajambo (in the name of mikataba).

Yuko mwingine nae kaingiza wabongo wote mkenge kalamba bn70 kagawa hapo km 30 saa hz kila mtu mamlakani kalowa hawezi kumwambia kitu. Hadi msaidizi wa kadinali kapewa rushwa na kabeba.
 
Mm nakumbuka alipokuw anaulizwa icho alisema alienda kuonana na aliyekuwa meneja wa saida karoli ndo wakapatana kuwa inabidi watoe asilimia 25 za publidhing na wakatoa kiasi kazaa cha hela kwa huyo meneja maana ndo mliki halali wa uwo wimbo.....lakini hakusema kuwa wameonana na saida mbona unajaribu kubadilisha ukweli kuwa uwongo punguza chuki ndo utapanuka kimawazo
Wapi niliposema kuwa walionana na Saida?
 
Acha kukurupuka, kumbe hata mwenye hakimiliki ya wimbo humjui alafu unaleta porojo?
Diamond amefuata taratibu zote zilizotakiwa na jamaa yuko makini sana
Story zako za kuongeza sifuri kawasimylie watoto wenzio wa instagram
Tumeshamaliza hapa nashukuru Umeelewa.Ngoja niendelee kufafanulia wengine ambao bado wapo gizani kama ulivyokuwa wewe.
 
Sijui mkataba wao ukoje maana inawezekana na wimbo ukawa mali ya producer pia.

ninachosema ni kuwa Diamond alisema kampa hela Saida alafu wakamalizana na Meneja wake sasa Saida kaja kuweka wazi kuwa Yeye alitoa wimbo bure na diamond alimpa hela meneja wake na sio yeye

Sasa swala lipo hivi kwanini Diamond na uongozi wake walidanganya?
Mbona Ali kiba alitudanganya kasoma mpaka chuo alafu kingereza hajui, uwongo ni sehemu moja wapo ya kunogesha story
 
Back
Top Bottom