Saida Karoli: Najihisi kuzaliwa upya

Haaa!
Hivi kumbe yuko hai
Nilijua kafa
Safi sana domo endelea kuwaibua wote walio potea.
 
Kwa hili Diamond anastahili pongezi. Huh ndio utu wa Mtanzania.
 
Yote kwa yote,pia si vibaya next time Diamond akafanya nae collabo, la 2 Diamond anaweza kumsainisha kwenye lebo yao then huyu dada akawa anapafom ngoma za kiasili.

Well said, amwambie Saida a stick kwenye ngoma za asili siyo kuchanganya kiarabu asije akajiaribia tena, wimbo wa hivi karibuni wa Diamond angeshirikisha Saida kwenye Vocal na ngoma kwa mbali ingenoga zaidi - Saida ana sauti ambayo ni unique kabisa inaradana na ya Diamond mwenyewe, Lionel Richie, Bill Ocean, marehemu Fred Mercury ,M.Jackson na Shakira.

Kitu kingine ambacho Diamond anapashwa kukumbuka ni kwamba: Saida ana vipaji vingi vikiwemo - Sauti vile vile kutunga nyimbo ingawa elimu yake siyo kubwa sana lakini kimziki anajua kijipanga vizuri kivocal, ngoma na za zana nyingine za mziki, Diamond anacho pashwa kufanya ni ku-refine hapa na pale utunzi wa Saida. Siyo kwamba labda nataka kumpamba Saida - hapa! Lakini kwa wale tuonao fahamu maneno yote ya kilugha anacho imba ubaki tunajiuliza maswali mengi, hivi huyu Saida maneno haya yote yakuchekesha sana uyaibua wapi? Ana kipaji sana.
 
Ukipewa kipaji halafu ukanyimwa Akili, kitakachotokea ni kutumikishwa tu.
Saida Karoli huenda ni mhanga wa hilo. Upeo wake wa kiakili upo chini, mara kadhaa nilimsikiliza kwenye interview kadhaa siku zilizopita na kuliona hilo wazi wazi.

Yaani pamoja na kuvuma sana plus kipaji kikubwa tena cha kipekee sana cha kuimba na kucheza, Saida Karoli bado anaamini anahitaji kusaidiwa ili atoke kimziki na kimaisha!
 
Yaani mpaka msanii maarufu kama Diamond anakuja kuCopy wazo la nyimbo yako basi ujui huo wimbo wako ni Muhimu sana katika mafanikio ya kimuziki.
Diamond yuko kibiashara 100% na hayuko kutoa huduma, Saida Karoli anapaswa kujua hilo.
 
Mi naamini Team WCB wanapita hapa na watayabeba haya mawazo ili kuboresha zaidi biashara zao za kimuziki....Ila ukweli kama WCB itataka kusain mkataba na mwanamuziki wa kike,wamuangalie huyohuyo Chambua kama karanga
 
Mapromota wezi walimmaliza dada huyu, Diamond Mungu ambariki angalau dada wa watu aache kuishi kishetani
unamaanisha nini kusema aache kuishi kishetani
 
Kwa kitendo ambacho promota alimfanyia saida kaloli basi tu si ya kusema zaidi ni kusema

MUNGU ANAMUONA PROMOTA.
 
Naona kama sasa imekua nongwa....zigo lote hilo abebeshwe diamond kisa tu kurudia wimbo wa saida.

Akimsaidia sio mbaya kama uwezo unaruhusu ile isiwe masharti sasa.
 
MAMA WAKATI WAKO UMEKWISHA.. HAUWEZI KUWAKA KAMA JUA. KWA SASA UKIJITAHIDI KUWAKA SANA UTAWAKA KAMA TOCHI..WAKATI NI UKUTA.
 
Naona kama sasa imekua nongwa....zigo lote hilo abebeshwe diamond kisa tu kurudia wimbo wa saida.

Akimsaidia sio mbaya kama uwezo unaruhusu ile isiwe masharti sasa.

Pamoja na 'innuendo' zako kuhusu Saida ambazo zinashangaza kidogo!! Kumbuka hapa tunazungumzia watu wawili wenye vipaji vya mziki, mmoja ana exposure kutokana na elimu yake, mwingine alitoka kijijini elimu yake ndogo masuala ya Music Industry ni mageni sana kwake ndiyo maana watu wenye nia mbaya walikuwa wana exploit her talent to maximum bila ya Saida kufaidi chochote cha maana.

On the other end, Diamond is a bit different, kutembea kwake nchi mbali mbali na kuchanganyikana na wana mziki mbali mbali Duniani kumemuongezea upeo wa kuona mbali, ndiyo maana kafungua kampuni yake yenye label yakwake hii ni hatua nzuri sana itampa uwezo wa kurekodi, kutafuta soko la kuuza cd za audio na video za kwake na za wanamziki wengine watakao kubali kujiunga na Record label yake hii ni very smart move ya dogo huyu!

Kama nilivyo fafanua hapo juu kazi yake kubwa itabaki kuwalipa loyality wanamziki wenye kipaji ambao watatumia Record label yake, mwisho ataendeleza au kuibua wanamziki wengine wenye kipaji kama Saida na hii doesn't mean anawajili au nini sijui.

Lazima tukubali kwamba Daimond ana business acumen sana na ni mwepesi kujifunza kutoka kwa wenzake wa nchi zilizo endelea na kusema kweli atafanikiwa kwa kuwa hana choyo na wala ajihusishi na malumbano ya vijiweni ambayo hayana tija.

Tatizo letu kuu kama Taifa utakuta baadhi ya watanzania ambao awaelewi vizuri masuala ya music Industry ndiyo wanakuja humu na maneno ya kashfa eti: Diamond kuimba wimbo wa Saida ndiyo iwe nongwa mara ooh Saida anataka kumtwisha mzigo Diamond mara Saida hana akili - lini baadhi yetu tutapunguza roho za kutu za kuwatakia watu wengine mabaya! Nani kawambieni Saida anaganga njaa - nani alimfuata mwingine?

Diamond katumia instinct alizo zaliwa nazo akaona aki imba na kucheza wimbo wa Saida anaweza kuvutia watazamaji na wasikilizaji wengi na kujiongezea soko na umaharufu na hicho ndiyo kimekuja kutokea - hits za wimbo huo kwenye U-Tube imezidi millioni moja ndani ya siku nne - je, hilo ni jambo la kawaida - think again.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…