Saida Karoli: Najihisi kuzaliwa upya

Saida Karoli: Najihisi kuzaliwa upya

Well said, amwambie Saida a stick kwenye ngoma za asili siyo kuchanganya kiarabu asije akajiaribia tena, wimbo wa hivi karibuni wa Diamond angeshirikisha Saida kwenye Vocal na ngoma kwa mbali ingenoga zaidi - Saida ana sauti ambayo ni unique kabisa inaradana na ya Diamond mwenyewe, Lionel Richie, Bill Ocean, marehemu Fred Mercury ,M.Jackson na Shakira.

Kitu kingine ambacho Diamond anapashwa kukumbuka ni kwamba: Saida ana vipaji vingi vikiwemo - Sauti vile vile kutunga nyimbo ingawa elimu yake siyo kubwa sana lakini kimziki anajua kijipanga vizuri kivocal, ngoma na za zana nyingine za mziki, Diamond anacho pashwa kufanya ni ku-refine hapa na pale utunzi wa Saida. Siyo kwamba labda nataka kumpamba Saida - hapa! Lakini kwa wale tuonao fahamu maneno yote ya kilugha anacho imba ubaki tunajiuliza maswali mengi, hivi huyu Saida maneno haya yote yakuchekesha sana uyaibua wapi? Ana kipaji sana.
ulikuwa wapi siku zote usiseme haya mpaka diamond akamuibua? Diamond ameshamrudisha kinachotakiwa ni saida mwenyewe kujipanga sasa
 
ulikuwa wapi siku zote usiseme haya mpaka diamond akamuibua? Diamond ameshamrudisha kinachotakiwa ni saida mwenyewe kujipanga sasa

Majibu yako yanaonyesha uelewa wako katika masuala ya Music Industry ni dismal kabisa, unasumbuliwa na inbuilt arrogance ndiyo maana unazungumza chochote kinacho kujia kichwani!!

Unapo sema nilikuwa wapi siku zote una maana gani? Soma maoni yangu ya ziada kuhusu mada hii, may be narudia "may be" hilo litakusaidia kuheshimu bibadamu wenzako na kujifunza kutumia lugha ya staha hata kama ukubaliani na maoni yao.
 
Msanii wa nyimbo za asili Saifa Karoli aliyevuma kitambo amefunguka na kusema kuwa kitendo cha msanii Diamond Platnumz kurudia moja ya kazi yake anajihisi kuzaliwa upya.
View attachment 404280
Saida Karoli
Saida Karoli ambaye aliwahi kufanya vizuri na nyimbo kama"Mapenzi kizunguzungu,Kaisiki,Maria Salome na nyingine kibao na alifanikiwa kilele soko la Afrika Mashariki kwa nyimbo hizo na kujipatia umaarufu mkubwa mwanzoni mwa miaka ya 2000.
Said a Kalori amesikika kwenye clip ambayo ameipost Diamond Platnumz kwenye mitandao yake ya kijamii na kusema kuwa mwanzoni waandishi wa habari walisha msahau walikuwa hawanfuatilii tena,laki I hata baadhi ya watu pamoja na ndugu zake walikua waliambiwa kuwa amekufa lakini baada ya kazi ya Diamond Platnumz kutoka imemrejesha watu kwenye himaya take kwani wameanza kumtafuta na Kumpigia simu sana.
"Mimi nimejisikia vizuri hii kazi tunayofanya ni kwa ajili ya mashabiki,mashabiki ndiyo wadau wetu wanaotufanya sisi,tuwe juu kwa hiyo si kazi ya kwangu Mimi peke yangu,ila Mimi kama Mimi,nimejisikia vizuri kusikiliza kwa sababu hata vyombo vya habari vilinisahau Leo hii vinanitafuta,haya ndugu zangu baadhi na wengine wanajua hata siko duniani wanajua nilishakufa lakini Leo hii naona watu mbalimbali wananitafuta kweli nimefunguka najihisi kuzaliwa upya" alisikika Saida Kalori.

Chanzo:East Africa Television (EATV)
alipotelea wapi baada ya laana aliyoipata ya kumpiga chini mume wake kipenzi wa kijijini baada ya kupata mafanikio? hapo ndio huwa nawavulia kofia wanawake. muta amemfikisha wapi sasa, sijamsikia kitambo huyo dada.
 
alipotelea wapi baada ya laana aliyoipata ya kumpiga chini mume wake kipenzi wa kijijini baada ya kupata mafanikio? hapo ndio huwa nawavulia kofia wanawake. muta amemfikisha wapi sasa, sijamsikia kitambo huyo dada.
Acha urongo mumewe ndio alianza kumpiga chini akaondoka na mnenguaji wa kike na yeye akaona isiwe tabu akabeba mcheza shoo wa kiume. Pia naona kuna watu wana wivu saana alivyoibuliwa na kijana kama umefuatilia matukio ya huyu kijana maarufu anaona fahari sana kuwa na wanamuziki wazuri kama yeye kutoka Tanzania na si mbinafsi mfano mzuri ni hiyo wasafi.
 
Back
Top Bottom