Saida karoli " Nilitumiwa, ukiona ninapoishi utasikitika

Saida karoli " Nilitumiwa, ukiona ninapoishi utasikitika

brave one

JF-Expert Member
Joined
Feb 5, 2013
Posts
4,879
Reaction score
7,386
Saida Karoli anaogopa kugusa hata jani, akidhani
ni nyoka anayetaka kumng’ata
1475653908414.jpg

Ni kwasababu licha ya kufanya vizuri kimuziki miaka kadhaa iliyopita, hakupata chochote na bado anaishi katika mazingira magumu.
“Niliumizwa kuanzia mwanzo, ni vitu vichache nilivyovipata, kama mkibahatika waandishi wa habari wenye makamera na wakija kwangu watashuti kulingana na nilivyo, wataona
mazingira ninayoishi ndipo watanzania watazidi kufunguka zaidi,” Saida alimwambia mtangazaji wa Jembe FM, Natty E.
Kwa sasa Saida Karoli anaishi jijini Mwanza. Hivi karibuni amerejea tena kwenye midomo ya watu baada ya Diamond kurudia wimbo wake Salome.
 
Inasikitisha sana, ila asilaumu sana aombe baraka anaweza kukutana na mtu mzuri aka mfanya akawa msanii wa kujivunia kazi yake, ila watu wabaya jamani kama marehemu Bi Kidude na umaarufu wake wote alikufa hana hata kitu jamani, looh inasikitisha.
 
Shida ni kwamba saida alikuwa hana hatimiliki ya nyimbo zake so hata mrabaha ukiingia hauendi kwake moja kwa moja
 
Ashukuru Mungu, wala asilalamike kwa kuwa wakati wake ule muziki ulikuwa haujachanganya sana kwenye vipato vya fedha. Asijilinganishe na akina Diamond, ajilinganishe na wenzake wa wakati ule aone kama walivuna chochote cha maana. Kwani kati ya Lunyamila na Simon Msuva, nani ni winga hatari kuliko mwenzake? Nani ana hela/mali kuliko mwenzake? Haya mambo yana wakati wake, ampe shukurani hata huyo aliyempromote na kumuexpose
 
Huyu Dada na wasanii wenzake wengi wa kipindi cha nyuma wanaishi maisha ya chini kwasababu kipindi wao wanafanya mziki walikuwa hawauchukulii mziki Kama kazi zinazoweza kuwalipa wakawa wanabweteka na umaarufu na pesa kidogo walizokuwa wanapata sasa wanaona hawa vijana wakina alikiba wanatumia fursa ya mziki vizuri kupiga pesa ndo na wao wanashtuka wanaanza kutoa lawama kwa watu!
 
Wanamuziki wa miaka ya nyuma sio kama walikuwa hawautumii muziki kama kazi,walikuwa wanajua kuwa ni kazi lakini walikuwa hawatambui kuwa muziki ni kazi ambayo inaweza kukupaisha kimaisha.
 
Saida Kalori
Mr Nice
Ferooz
Daz Baba
Chid Benz n.k

Hawa wasanii wanatoa funzo kubwa kwa hawa wasanii wachanga.

Hawakutakiwa kuwa ni wasanii wa kuishi maisha ya namna hiyo tuyasikiayo na hii nadhani sababu ya Elimu.

Big Up kwa AY, PRO JAY, MWANA FA Elimu yao kidogo walioipata imeweza kuwasaidia katika kuundeleza Muziki wao na Mavuno yao.
 
Saida Karoli anaogopa kugusa hata jani, akidhani
ni nyoka anayetaka kumng’ata
View attachment 412452
Ni kwasababu licha ya kufanya vizuri kimuziki
miaka kadhaa iliyopita, hakupata chochote na
bado anaishi katika mazingira magumu.
“Niliumizwa kuanzia mwanzo, ni vitu vichache
nilivyovipata, kama mkibahatika waandishi wa
habari wenye makamera na wakija kwangu
watashuti kulingana na nilivyo, wataona
mazingira ninayoishi ndipo watanzania watazidi
kufunguka zaidi,” Saida alimwambia mtangazaji
wa Jembe FM, Natty E.
Kwa sasa Saida Karoli anaishi jijini Mwanza. Hivi
karibuni amerejea tena kwenye midomo ya watu
baada ya Diamond kurudia wimbo wake Salome.
ooh bibi pole wakati wako umekwisha ndivyo maisha yalivyo.. endelea kupiga mziki kwenye harusi, send off, ubarikio, na graduations za sekondary.. ndio riziki yako mola aliyokupangia
 
Saida Kalori
Mr Nice
Ferooz
Daz Baba
Chid Benz n.k

Hawa wasanii wanatoa funzo kubwa kwa hawa wasanii wachanga.

Hawakutakiwa kuwa ni wasanii wa kuishi maisha ya namna hiyo tuyasikiayo na hii nadhani sababu ya Elimu.

Big Up kwa AY, PRO JAY, MWANA FA Elimu yao kidogo walioipata imeweza kuwasaidia katika kuundeleza Muziki wao na Mavuno yao.
hapo MR NICE usimueke kayataka mwenyewe ebzii hizo yupo na mpunga nilikuwa namjua nje ndani tatizo lake akuwekeza katika VITEGA UCHUMI yeye aliwaza atakuwa juu siku zotee hata wasanii wa marekani kabla hakujaingia mfumo kuuza kwa internet kazi zao walipokuwa wakitoa album na kuuza copy nyingi ama nyimbo ikiwa hit wakawa na show nyingi walikuwa hawatumii pesa hovyo walikuwa wanaingiza katika vitega uchumi na kununua aset nyingi zikiwemo nyumba za gharama nk
kwa wakati ule mr nice alikuwa na uwezo wa kujenga nyumba hata kumi mbagara au bunju 7bu siku moja nilishuudia kwa macho yangu akinunua cheni ya silva zile nene zile kwa laki 6(na ukumbuke nyingne alikuwa nazo) sasa wakati huo mbagara au bunju ulikuwa unapata viwanja vi3 au viwiri
hivyo mr nice haya maisha aliyataka mwenyewe 7bu utajir aloupata ulikuwa unajulikana wazi
 
"Mpenzi nakupenda, mapenzi sio kila kitu....
Mpenzi nakupenda mapenzi ni uamuzi wa mtu....""

Hii nyimbo ni fumbo kwa wengine... Ujumbe uliojaa huba, mapenzi na mahaba....

Wezi wa kazi za wasanii, Mungu anawaona...
 
Saida Karoli anaogopa kugusa hata jani, akidhani
ni nyoka anayetaka kumng’ata
View attachment 412452
Ni kwasababu licha ya kufanya vizuri kimuziki
miaka kadhaa iliyopita, hakupata chochote na
bado anaishi katika mazingira magumu.
“Niliumizwa kuanzia mwanzo, ni vitu vichache
nilivyovipata, kama mkibahatika waandishi wa
habari wenye makamera na wakija kwangu
watashuti kulingana na nilivyo, wataona
mazingira ninayoishi ndipo watanzania watazidi
kufunguka zaidi,” Saida alimwambia mtangazaji
wa Jembe FM, Natty E.
Kwa sasa Saida Karoli anaishi jijini Mwanza. Hivi
karibuni amerejea tena kwenye midomo ya watu
baada ya Diamond kurudia wimbo wake Salome.
halidi na felemoni walipendana mapenzi yao yakadumuuu....mwenye wivu ajinyonge kweli mwenye wivu ajinyonge[emoji95] [emoji95]

SASA SAIDA HAO WANAUME WALIPENDANA VP AU BUKOBA KUNA JINA LA KIKE KAMA HAYO...AU NI VINA AU NI MAMBO YA MOMBASA?????
 
Pole sana mama,haya jaribu kurudi tena maana umeshapewa promo na DIAMOND.
 
Radio mbao za uchochezi hizo.... anapewa interview ili iwe nini!!???
 
Nice amejimaliza mwenyewe
Kama nafasi alipata Sema hakuitumia...

Ova
Saida Kalori
Mr Nice
Ferooz
Daz Baba
Chid Benz n.k

Hawa wasanii wanatoa funzo kubwa kwa hawa wasanii wachanga.

Hawakutakiwa kuwa ni wasanii wa kuishi maisha ya namna hiyo tuyasikiayo na hii nadhani sababu ya Elimu.

Big Up kwa AY, PRO JAY, MWANA FA Elimu yao kidogo walioipata imeweza kuwasaidia katika kuundeleza Muziki wao na Mavuno yao.
 
Huyu Dada na wasanii wenzake wengi wa kipindi cha nyuma wanaishi maisha ya chini kwasababu kipindi wao wanafanya mziki walikuwa hawauchukulii mziki Kama kazi zinazoweza kuwalipa wakawa wanabweteka na umaarufu na pesa kidogo walizokuwa wanapata sasa wanaona hawa vijana wakina alikiba wanatumia fursa ya mziki vizuri kupiga pesa ndo na wao wanashtuka wanaanza kutoa lawama kwa watu!
Ivi kiba ni kijana halafu hadi leo anaishi n wazazi wke k'koo anafanikio gani ya kupitia mziki
 
Saida Kalori
Mr Nice
Ferooz
Daz Baba
Chid Benz n.k

Hawa wasanii wanatoa funzo kubwa kwa hawa wasanii wachanga.

Hawakutakiwa kuwa ni wasanii wa kuishi maisha ya namna hiyo tuyasikiayo na hii nadhani sababu ya Elimu.

Big Up kwa AY, PRO JAY, MWANA FA Elimu yao kidogo walioipata imeweza kuwasaidia katika kuundeleza Muziki wao na Mavuno yao.
Hivi chidbenx nae ni msanii wa zamani?

[emoji817]
 
Shida ni kwamba saida alikuwa hana hatimiliki ya nyimbo zake so hata mrabaha ukiingia hauendi kwake moja kwa moja

Fine, lakini kibibadamu muhusika alipashwa kumpatia %ge fulani ya mapato, ni kweli jamaa ndiye alimtoa kijijini na kumleta kwenye limelight lakini alikuwa na wajibu wa kumuelemisha kuhusu haki zake hata kama ni ndogo, alicho mfanyia Saida sio fresh hata kidogo.

Kitu kingine na huyo dada yetu alifanya vibaya kumkimbia mtu aliye mtoa kijijini, alijikuta anaigia mkenge baada ya kushawishiwa na wajanja akakimbilia Uganda sijui na Kenya na huko akijikuta wanatumia tu, sijui walimlipa kiasi gani?

From now on ajifunze kutulia na anapo ingia mkataba na mtu amshirikishe mwana sheria sio anafanya mambo kienyeji tu.

Mwisho namshauri amwendee mtu aliye mtoa kijijini na kumtangaza waombane msamaha maana wote naona kila mmoja wao ana makosa yake - Saida vile vile asiwe anamtangaza vibaya mshiriki/mmiliki wake wa mwanzo - asahau kila kitu atafute maisha mapya.
 
Back
Top Bottom