Saida karoli " Nilitumiwa, ukiona ninapoishi utasikitika

Saida karoli " Nilitumiwa, ukiona ninapoishi utasikitika

Huyu Dada na wasanii wenzake wengi wa kipindi cha nyuma wanaishi maisha ya chini kwasababu kipindi wao wanafanya mziki walikuwa hawauchukulii mziki Kama kazi zinazoweza kuwalipa wakawa wanabweteka na umaarufu na pesa kidogo walizokuwa wanapata sasa wanaona hawa vijana wakina alikiba wanatumia fursa ya mziki vizuri kupiga pesa ndo na wao wanashtuka wanaanza kutoa lawama kwa watu!
Alikiba nae c wa kitambo kaka au kaanza lini mziki
 
Anapenda vitu vya bei kali
Nikiwa sina kitu yeye hanijali[emoji445]
.....aliimba chameleone kumuimbia
 
huyu mama nae wakati wake alikuwa anamatumizi ya hovyo. Mzee FM aliwahi kuonesha bank statement ya huyu mama akitoa bank pesa zaidi ya mara kumi kwa siku. Hakujua kuwa usanii ni suala la muda. Kama alitaka ajengewe nyumba ndipo alipobugi
 
Saida ana kipaji jamani...Mzee Muta hebu Fanya kama yameisha mrudi kutupa utamu kama wa enzi zilee
 
Shida ni kwamba saida alikuwa hana hatimiliki ya nyimbo zake so hata mrabaha ukiingia hauendi kwake moja kwa moja
Unaweza usiwe na hakimiliki lakini mrahaba bado ukapata! Tatizo la msingi ni waliokuwa wanamsimamia kutofahamu msanii wao anatakiwa kupata nini kwenye mkataba husika. Kati ya Saida Karoli na Mzee Mutta palitakiwa awepo mtu anayeangalia maslahi ya Saida... huyu ndie Meneja wa Saida ingawaje kwa hapa unaweza kukuta meneja wake mwenyewe alikuwa mkono wa kuume wa Mzee Mutta!

Kwahiyo hata kama hakimiliki ingekuwa ni ya FM Studio; Meneja angehakikisha kwamba mrabaha wa Saida kwa kazi zake ni asilimia fulani kwa kipindi chote; inapotokea mtu anarudia kazi zake, Meneja hapo hapo angehakikisha Saida atapata asilimia fulani... kama mtu anatumia idea ya wimbo uliotungwa na Saida mwenyewe kisha mtu akatumia hiyo idea kutengeneza filamu (lakini kuna mipaka ya idea kuwa copyrighted); meneja hapo hapo angetakiwa kujua hata kama hilo litatokea miaka 20 ijayo, Saida angepata asilimia fulani... kama hata kama baada ya miaka 10 mtu angetengeneza T Shirts za Chambua Kama Karanga na Chambua Kama Karanga ina trademark, from the beginning Meneja alitakiwa kuhakikisha kuna kipengele kwenye mkataba kinachosema hapo Saida atapata asilimia fulani!

Kwahiyo tatizo la msingi sio hakimiliki per se bali inaonekana mkataba haukua na vipengele vya msingi vinavyoonesha haki na wajibu wa Saida! Ingekuwa ni ngumu sana kwa Saida kuwa na hakimiliki kwavile kazi zake zilikuwa zinagharamiwa kwa 100% na FM Studio! Ni sawa na mwanamuziki aliye kwenye bendi! Akihama, nyimbo zinabaki kuwa ni mali ya mwenye band!
 
Huyo Saida Aache Uongo..anadhani hatukumbuki Alikuwa anatapanya Pesa ivyo Mr.Nice cha Mtoto..pia alimwachaga Mpaka.mumewe wa toka kijijini akachukua Serengeti Boy..Watu wanamlaumu Mzee Lutta but I still remember Na Kuna kipindi alikuwa akielimishwa kuhusu utumiaji wa Pesa akawa anangangania aachwe guru..vijana wakamgeuza Sugar Mumy Atoke zake
 
Back
Top Bottom