Saidi Miraj: Spika bora ni yule mwenye weledi, anayejitambua, na anayeweka maslahi ya taifa mbele

Mafyangula

JF-Expert Member
Joined
Jan 16, 2025
Posts
557
Reaction score
1,039
Mwanasiasa mkongwe na mchambuzi wa masuala ya siasa, Saidi Miraj, amesema kuwa nafasi ya Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni nyeti na ina mchango mkubwa katika kulinda utulivu na amani ya nchi.

Akizungumza katika mahojiano maalum na Jambo TV leo Novemba 10, 2025, Miraj amesema kuwa Spika ni nguzo muhimu ya uongozi katika kuhakikisha Bunge linabaki kuwa chombo huru, makini, na kinachowajibika kwa wananchi.

Amefafanua kuwa Spika mara nyingi hukabiliwa na changamoto za kusawazisha nguvu za mihimili mikuu ya dola, jambo linalohitaji hekima na ustahimilivu ili kuhakikisha uhusiano wa taasisi hizo unabaki kuwa wa kuheshimiana na wenye tija kwa taifa.

Aidha, Miraj amebainisha kuwa Spika bora ni yule mwenye weledi, anayejitambua, na anayeweka maslahi ya taifa mbele ya maslahi binafsi.

Zingatia neno “maslah ya taifa mbele”
 
Tuache porojo na kudanganya, Hakuna spika bora bila bunge lenye ubora lililochaguliwa na wananchi walio wengi, hakuna spika bora kwenye bunge la chama kimoja.
 
Spika Mzuri ni yule atakayeweza Kushawishi Wabunge wote waseme NDIOOO...
 
Back
Top Bottom