Mbona hata NJE madudu kibao? Tena makampuni makubwa tu kama BAYER na lipo USA. Jana tu makala ilikuwa hapa na waweza kuisoma:
Kampuni ya ya kutengeneza BAyer ya amerika imetengeneza Vidonge vya HIV na kupeleka ulaya
READ: https://www.jamiiforums.com/jamii-p...geneza-vidonge-vya-hiv-na-kupeleka-ulaya.html
Ni Bayer hawahawa walishatengeneza madawa ya kuzuia Mimba na akina Mama walioacha kipindi hiyo kuyatumia na wakshika Mimba, karibu wote walizaa watoto vilema kwa kukosa Miguu na au Mikono.
Hivi unajua matunda yanatoka sehemu za joto na yanapelekwa Ulaya na wakifika huko wanasindika hata yawe yameoza na mwisho wanayarudisha Africa baada ya kuweka Chemicals kibao na wewe ndiyo unaona ya maana? Kwa nini usitengeneze mwenyewe juice ya Matunda nyumbani kwako na matunda yawe ya Tanzania? Kwa nini ule Nyanya za Makopo na siyo za Sokoni au za kulima mwenyewe?
Kuhusu Fanicha, si kweli kuwa zote zipo barabarani. Kuna watengenezaji wa kuaminika sana na ukitaka naweza kukupa hata anwani zao na wanakupa hata jina la mbao iliyotumika na unapewa muundo kabisa wa unataka iwe vipi. Kutapeliwa na sisi tunakutaka wenyewe kwa kutokujua kuwekeana mikataba. Sasa wewe unampa fundi hela na hakuna masharti wakati unajua ni matapeli? Andikiana kabisa na yeye Mkataba au mwambie atengeneze na akimaliza, hela atachukua Bank na asipomaliza, wewe hiyo hela unaenda kuichukua. TUBADILIKE.
Cement ya Tanzania haijaangusha majengo hata SIKU MOJA. Acha uongo wa waziwazi na kama jambo hulijui heri ukae kimya. Hata Cement ya Mfaransa yenye sifa ya kufikisha 400Mpa bado na yenyewe ikiletwa Tanzania, itaangusha tu majengo kwa Uzembe wetu na Ufisadi wetu. Ujenzi una masharti yake na yakivunjwa, siyo kosa la Cement.
Ubora wa vitu ni kosa la TBS na hii haijalishi vitu vya NJE au vya ndani. Sasa tunauziana Mavitu kibao yaliyokataliwa Majuu na wanatuletea sisi hadi Condoms na wewe unakaa unafurahia kuwa zimetoka nje. Watu kama nyie, Mchina atatajirika sana maana itatosha tu kitu atengeneze huko Morogoro na anaweka karatasi "Made in Taiwan" na wewe utakuwa radhi kulipa Malaki kwa kudhani ni cha nje kumbe Wachaga wamefyatua hapo Himo.
Solution siyo kugoma kununua vya Tanzania bali ni kuwabana TBS wafanye kazi yao vizuri. Kwa ujumla ni kuibana SERIKALI ifanye kazi vizuri na hapo tutapata bidhaa vya ubora wa juu na tutanunua vitu vya Tanzania IMARA na bila kudanganywa. Ni jambo linalowezekana.
Kila la kheri Mzee wa CONDOM IMPORTED, ambazo zimeshakwisha muda wake huko USA.
condom za tanzania zinapasuka kama maputo kwanini nisitumie condom za nje
cement ya tanzania zinaangusha majengo we jengo kifusi kimekuwa mchanga mchanga kwanini nisinunue za nje
juice za bakhresa zina ma uchafu chafu kesi zake zimeletwa hapa mara nyingi nadhan tumeshuhudia kwanini nisinywe TANG
makochi na fanicha ziko pale keko barabarani zimepangwa vumbi lote la barabarani liaishia pale unanunua kochi jeupe lakini ukiliangalia ni jeusi kwanini nisiende kwa Mchina
suti unashonesha ila unapata suti baada ya kumweka fundi polisi ndio anamalizia nguo yako kwanini nisinunue Gucci
viatu vile vya mbeya design mbovu kiatu kimekaa kama mkate bwana na sio ngozi kwanini nisinunue viatu vya Italy
Sabuni zinazotengenezwa na wajasiliamali wetu hazikawii kuchubua mikono kwanini nisinunue Dettol
ARV mnawatengenezea feki
Bia Bingwa ulikuwa ukinywa lazima uharishe kwanini watu wasinywe heinekeen
Angalia bidhaa FEKI aka REPLICA:
http://www.oureplica.com/
http://www.replicahandbags.hk/category/gucci#
http://www.gucciwatchreplicas.com/
http://www.cheapdesignerhandbag.us/