Saidia Nchi Yako: NUNUA bidhaa MADE IN TANZANIA.

Made in Tanzania:





Hicho kigari cha VETA ni SUZUKI, not made in Tanzania, ni Modified......oh,no!....Asembled....aah hapana...Sjui nini in Tanzania, la Chini ni IVECO, Bandikwad Nembo ya Nyumbu in Tanzania!
 
Ata hizi bidhaa za nje zinazoingia zinachangia sana pato la taifa zikisimamiwa vizuri ndio maana tra wanasema wanakusanya 600ml kwa siku chache tu...huu ni ushuru wa bidhaa za nje,ukiingiza cement kwa mfano Tbs wanatakiwa kupima ubora na gharama ya kupima ni 350,000/tsh hachilia mbali ushuru wa tra na gharama za port...kama tax ikisimamiwa vizuri ni sawa tu bidhaa za nje zije watu wapate ajira na tra wakusanye mapato..nchi nyingi zinakua kwa kukusanya ushuru na kuutumia vizuri,tukitengeneza bidhaa nzuri zenye ushindani si lazima tutegemee soko la ndani twaweza ku export nje..india,pakistan,bangladesh,nepal ni nchi zinazoongoza kwa kunywa chai yaani hawa jamaa wanakuywa sana chai na Kenya wame monopolise soko lao la chai wanapenda sana chai ya kenya,tutengeneze bidhaa nzuri zitapata soko la ndani na nje...ukienda Geita mananasi yanaoza wakati tunakuywa juice za nchi zisizona mananasi..njombe nyanya zinaoza ndoo moja tsh 500 tungekuwa na kiwanda kizuri cha tomato ketchap zenye ubora mzuri tungeuza nje na ndani ya nchi...tulikuwa na kiwanda cha dabaga nakikumbuka sana pale iringa lakini hakuna mazingira mazuri kwa viwanda maana umeme ni wa kubahatisha sana...tutengeneze bidhaa bora soko la ndani na nje ni kubwa sana
 
Mbona hata NJE madudu kibao? Tena makampuni makubwa tu kama BAYER na lipo USA. Jana tu makala ilikuwa hapa na waweza kuisoma: Kampuni ya ya kutengeneza BAyer ya amerika imetengeneza Vidonge vya HIV na kupeleka ulaya

READ: https://www.jamiiforums.com/jamii-p...geneza-vidonge-vya-hiv-na-kupeleka-ulaya.html

Ni Bayer hawahawa walishatengeneza madawa ya kuzuia Mimba na akina Mama walioacha kipindi hiyo kuyatumia na wakshika Mimba, karibu wote walizaa watoto vilema kwa kukosa Miguu na au Mikono.

Hivi unajua matunda yanatoka sehemu za joto na yanapelekwa Ulaya na wakifika huko wanasindika hata yawe yameoza na mwisho wanayarudisha Africa baada ya kuweka Chemicals kibao na wewe ndiyo unaona ya maana? Kwa nini usitengeneze mwenyewe juice ya Matunda nyumbani kwako na matunda yawe ya Tanzania? Kwa nini ule Nyanya za Makopo na siyo za Sokoni au za kulima mwenyewe?

Kuhusu Fanicha, si kweli kuwa zote zipo barabarani. Kuna watengenezaji wa kuaminika sana na ukitaka naweza kukupa hata anwani zao na wanakupa hata jina la mbao iliyotumika na unapewa muundo kabisa wa unataka iwe vipi. Kutapeliwa na sisi tunakutaka wenyewe kwa kutokujua kuwekeana mikataba. Sasa wewe unampa fundi hela na hakuna masharti wakati unajua ni matapeli? Andikiana kabisa na yeye Mkataba au mwambie atengeneze na akimaliza, hela atachukua Bank na asipomaliza, wewe hiyo hela unaenda kuichukua. TUBADILIKE.

Cement ya Tanzania haijaangusha majengo hata SIKU MOJA. Acha uongo wa waziwazi na kama jambo hulijui heri ukae kimya. Hata Cement ya Mfaransa yenye sifa ya kufikisha 400Mpa bado na yenyewe ikiletwa Tanzania, itaangusha tu majengo kwa Uzembe wetu na Ufisadi wetu. Ujenzi una masharti yake na yakivunjwa, siyo kosa la Cement.

Ubora wa vitu ni kosa la TBS na hii haijalishi vitu vya NJE au vya ndani. Sasa tunauziana Mavitu kibao yaliyokataliwa Majuu na wanatuletea sisi hadi Condoms na wewe unakaa unafurahia kuwa zimetoka nje. Watu kama nyie, Mchina atatajirika sana maana itatosha tu kitu atengeneze huko Morogoro na anaweka karatasi "Made in Taiwan" na wewe utakuwa radhi kulipa Malaki kwa kudhani ni cha nje kumbe Wachaga wamefyatua hapo Himo.

Solution siyo kugoma kununua vya Tanzania bali ni kuwabana TBS wafanye kazi yao vizuri. Kwa ujumla ni kuibana SERIKALI ifanye kazi vizuri na hapo tutapata bidhaa vya ubora wa juu na tutanunua vitu vya Tanzania IMARA na bila kudanganywa. Ni jambo linalowezekana.

Kila la kheri Mzee wa CONDOM IMPORTED, ambazo zimeshakwisha muda wake huko USA.

Angalia bidhaa FEKI aka REPLICA:

http://www.oureplica.com/

http://www.replicahandbags.hk/category/gucci#

http://www.gucciwatchreplicas.com/

http://www.cheapdesignerhandbag.us/
 
Nitaanza kununua bidhaa za Tz pale ambapo jamaa zangu wa TBS na TFDA wakianza kuwa serious.
Ila niko na mkakati binafsi jana tuu nilitoka kataa maziwa packed yale toka Zambia nikanunua ya ASAS.
Kwa bidhaa ambazo nina uhakika na ubora wake huwa nanunua sana
 
Mkuu,

Opel ni kampuni ya General Motors ambayo waliinunua kutoka German. Ila kiwanda kilipopata matatizo (Kampuni mama yaani GM-USA) Chancellor wa German, Angela Merkel, alipigana hadi kuvunja sheria za European Union ili tu kuhakikisha anakiokoa kiwanda cha Opel hapo German.

Sasa hapo utashangaa, kwa nini huyu Mama ahangaike na kiwanda cha KUUNGA magari kutoka USA? Jibu ni dogo AJIRA.

Hata wao walinunua Viwanda vya magari (Volkswagen) nchini Czech-kiwanda cha SKODA na SPAIN-kiwanda cha SEAT. Ila siku zote Waczech wanajivunia sana kuwa ni Kiwanda chao na ukweli unabaki kuwa Kiwanda kama kipo huko, Ajira inatolea kwa watu wa nchi hiyo.

Leo hii TBS ingawa ni kiwanda cha Adam Miller (Sub Miller) kutoka South Africa (sasa anaishi UK) ila bado wanaopata ajira ni Watanzania na siyo South Africa au UK.
Hivyo basi, hata kama tutakuwa tuna kampuni ya KUUNDA au KUUNGA hapa Tanzania, hayo magari bado yataitwa MADE IN TANZANIA. Sasa utasema Made in JAPAN wakati zilikuja PARTS kutoka sehemu nyiingi duniani?



Pichani ni Magari ya VW yakiwa na namba za nchi yanakotengenezwa...... I wish na sisi tungelikuwa na kakiwanda ketu hata kama Asilimia 100 ni VW ila cha muhimu ajira wapate Watanzania.


Hicho kigari cha VETA ni SUZUKI, not made in Tanzania, ni Modified......oh,no!....Asembled....aah hapana...Sjui nini in Tanzania, la Chini ni IVECO, Bandikwad Nembo ya Nyumbu in Tanzania!
 
Ni kweli kuwa inaingiza sana tu pato la TAIFA ila hako kamchezo ndiyo kameshusha sana uchumi wa USA na Uingereza. Walitegemea sana bidhaa za nje na wao wakawa wanafanya kazi za ofisini tu. Muingereza viwanda vya magari karibu vyote kauza na sasa wanajuta maana kazi zinaanza kuwa za shida.

Sasa ukitegemea uangize kila kitu na Serikali ichukue kodi, siku moja utakuta watu hawana kazi maana kila kitu unaagiza. Hilo linawezekana kwa nchi za Waarabu maana wao wana mafuta. Sehemu kama Dubai wametumia hela nyingi sana kuwekeza kama watu wa kutoa SERVICE. Soko la Dubai ni kubwa sana na hata kama hawatozi kodi, bado watu wanalipia Umeme, majengo kukodisha, utafika hapo kwa Emirates Air na kulala, kula, kwenda Disco nk na mwisho wa siku hela yao itaingia tu ingawa ni kidogokidogo.

Ni kweli linawezekana ila inabidi uwe na Capital kubwa sana na hili pia linaweza kubadilika muda wowote mara akija kichaa mwingine na offer nzuri zaidi yako kama ilivyokuwa zamani UK na USA na sasa watu wamehamia ASIA. USA sasa wameanza kuhaha kuwekeza katika viwanda na ndiyo maana unaona Obama alipigana sana ili viwanda vya magari (Big 3) visife kwani ni hatari sana kwa uchumi wa nchi.

Tatizo la usafiri linafanya bidhaa mikoani zioze. Nyanya hapo Morogoro tu bei rahisi sana wakati Dar bei zaidi ya mara mbili. Nakubaliana na wewe kuwa kuwepo kiwanda walau cha Katchup ni faida kubwa sana kwa wenyeji. Sasa hivi bakresa anakwenda hadi mikoani au vijijini kununua bidhaa kama Miwa na matuda na anatengeneza Juice, sasa kwa nini tusinywe Juice zake au kununua product zake ili kesho akanunue tena Matunda huko kijijini?

Kwa dunia ya sasa, kuna hii MINADA ya Kimataifa, wewe kama una bidhaa nzuri utauza tu. Hakuna kitu kama Monopoly ya kuuza chai au kahawa duniani. Huko ni BEI yako na UBORA wako. Ni Uwongo tu wa baadhi ya viongozi ili kuficha uzembe wao.
 
Usiniambie hata MANANASI, Maembe, Nyanya (made in Tanzania) nk unataka hadi TBS na TFDA waje wakague ndipo ule na vinginevyo utanunua nyanya na Juice za Makopo. Kama hao ndiyo wanakagua bidhaa, basi hata za nje ni mbovu na huko ndiyo hatari zaidi maana watu wanaokota bidhaa zinazotakiwa kutupwa na wanakuja kubadilisha tarehe na kuuza.

Hata huyu Mwenyekiti sijui wa CCM aliyekamatwa na bidhaa feki za kutengenezea madawa ya kurefusha maisha kwa waathirika wa ukimwi, hizo bidhaa zilikuwa zimetoka South Africa. Mlimani City mwanzo walisifika sana hadi watu walipogundua kuwa wanauza bidhaa zilishokwisha muda wake kutoka South Africa.

TBS na TFDA ndiyo wakaguzi wa bidhaa zinazotoka nje pia. Ni hawa TBS walikuwa wakikagua na kutoa Kibali cha matari ya magari kutoka nje na matairi kibao yamepasuka na kuuwa Watanzania wengi tu kwenye ajali za Mabasi. Au umesahau? Haya bana, waaamini tu hao TBS na TFDA kwa ukakuzi wao wa bidhaa za nje kuwa huko wanafanya kazi kwa ufanisi ila za ndani ndiyo wanazembea.
 
Unaweza oma vyema comment yangu ukaielewa?Bahati nzuri iko kwa kiswahili nilizani ni rahisi kuielewa
 
Hapo kwenye BOLD Blue, ndiyo panaleta matatizo. Nashindwa kuelewa kwa nini unaamini bidhaa za NJE ya Tanzania wakati bidhaa hizo pia zinakaguliwa na TBS na/au TFDA. Au huji hilo kuwa hao jamaa hutakiwa kugaguwa? Na wanaweza kuzuka hata dukani kwako kukagua kama bidhaa unazouza hapo dukani ziliingizwa kwa kibali chao.

Mie pia niliandika KISWAHILI na nikategemea utanielewa. Ila naona tatizo lipo mbali zaidi. Nafikiri kuna haja ya kufungua mjadala wa JINSI TBS na TFDA ZINAVYOFANYA KAZI.

Mwisho, hapo kwenye BOLD RED, maanadamu unajisifu unaandika Kiswahili fasaha, basi neno ni niliDHAni na siyo kuZAni. Na ukiandika na kuweka alama ya kuuliza, unaacha SPACE moja. Neno OMA, sintakushambulia kwa sababu ni makosa ya uandishi na ninaelewa hilo. Sorry kwa Kiswahili changu kibovu hata hivyo.

Tuache Porojo: Nafikiri wote tupo kwenye mstari mmoja ila tunapishana kidogo tu. Ukweli ni kuwa bidhaa za nje ni HATARI sana kwa afya ya mtu na hasa ukichukulia Uzembe unaofanyika kwenye Vitengo kama TBS na TFDA. Hawa jamaa ndiyo wanaokagua hata bidhaa kutoka Nje ya nchi. Kila kinachopita pale Bandarini basi ni TBS na TFDA wanakagua kwa kuchukua Sample na kupima na mwisho wanaruhusu bidhaa ziingizwe ndani. Ila kinachotokea hapo na hasa inapokuwa ni MZIGO MKUBWA au mzigo wa Wakubwa, ni Mungu anajua.

Unakumbuka NGANO ya Mhindi/Muarabu ilimwagwa wakati wa Mkapa? Walidai ilikuwa mbovu na haifai kuliwa. Baadaye kampuni iliyouza ya Uholanzi, iliishitaki Serikali ya Tanzania kwa kuwachafulia jina kwa sababu ngano yao ilikuwa safi. Jamaa walishinda na tulikuja kulipa fidia kwa Mhindi huyo na gharama za kesi kwani ilikuja kuonekana kuwa jamaa alikuwa kakosana na Wakubwa na wakaamua kumpa hasara. Ndiyo mambo ya TBS/TFDA hayo. Kwa kuanguka kwa ghorofa lilikuwa linatakiwa kuwa na ghorofa 10 ila zilishafikia 16, ndiyo hapo utaelewa ninasema nini.

Lowassa alidai jengo Masaki lilijengwa kimakosa na likabomolewa ila jamaa wakaja kushida kesi na sisi tunalipa fidia.

Waingereza wanasema "Can Only Count On Yourself. "
Nitaanza kununua bidhaa za Tz pale ambapo jamaa zangu wa TBS na TFDA wakianza kuwa serious.
Unaweza oma vyema comment yangu ukaielewa?Bahati nzuri iko kwa kiswahili nilizani ni rahisi kuielewa
 
Uzuri nilisha wai kuwa mwalimu so nimeelewa wapi tunapishana kwa kiswahili chepesi
TBS na TFDA wakiwa serious na ukaguzi pia na utoaji wa bidhaa such that tukawa na bidhaa genuine sokoni apo ndipo nitakuwa nanunua bidhaa bse right now 30% ya bidhaa sokoni ni feki this is general za nje na ndani.
Mfano kuna jamaa wanatengeneza the so called nondo unaweza kunja ata kwa mkono yes made in Tz but poor quality, wachina wanafyatua bati kule vingunguti na wanafoji mihuri na are cheaply sold in the market yes made in Tanzania but poor quality.Otherwise kwa vitu ambavyo nina ufahamu navyo ambavyo sihitaji TBS au TFDA huwa nanunua hasa vyakula na matunda ya asili au products ambazo nilishawai tumia au shauliwa na wataalamu.
Uzuri wangu kabla sijanunua kitu ni lazima niwaconsult wahusika au wadau wa iyo item au waliowai tumia bse niko na friends from almost all the fields based on the my 20 years of study plus 10 years of work.
 

jamani kuhusu kuhusu nyanya za packet-mie ni mnunuzi mkubwa! sababu-kila wakati umeme unakatka manyanya yanaozaoza frijini na muda wa kwenda sokoni kila wakati sinao so kwanini nisinunue nyanya za pakistan...??? Ili kampeni hii ifanikiwe ni kila mtu aplay part yake
 
Ndugu Watanzania,

MADE IN TANZANIA KWANZA.

Mimi huwa na nunua Africafe Amazon mara kwa mara na wakati mwingine bahatisha chaibora kwa supplier, kwakweli nafahari sana na vitu vya kwetu.
 
Safi sana Mkuu wangu. Hata walio nje ni VEMA wakachangamkia bidhaa za Tanzania. Tupo pamoja sana tu.

[/CENTER]

Mimi huwa na nunua Africafe Amazon mara kwa mara na wakati mwingine bahatisha chaibora kwa supplier, kwakweli nafahari sana na vitu vya kwetu.
 
Ndiyo maana nikasema tupo pamoja ila hunielewi tu na mie nilikuelewa tangu mapema. Bidhaa zote zinazopitiwa kwenye mikono ya TBS na TFDA ni hatari sana kwa afya yako na bahati mbaya kwa sheria ya Tanzania, bidhaa zote za nje ni LAZIMA zipitie kwao ila za ndani si LAZIMA. Hapo sasa akili yako itumike kwa kuamini za ndani za nje.

Kuhusu Nondo na Cement, hivi vyote unaweza hata wewe mwenyewe kuvitest. Kwa mfano nondo nina imani ukienda Mlimani (UDSM) wataweza kuivuta na kukuambia uimara wake (Stress test). Na kwenye Cement huwa wanafanya Crush test na unapata ubora wake baada ya siku 7, 14 na 28.

Mwisho, kwenye ujenzi wa nyumba hadi ghorofa nne, tumieni matofali ya kuchoma jamani. Hapo Nondo na Cement unatumie tu kwenye Floors za jengo. Tofali za kuchoma zinajenga ghorofa. Ila tafadhali sana, waone wataalamu wakupe msaada na hasa baada ya kujua uimara wa tofali zako na wakupe UNENE gani utumike kwa jengo lako. Kila la kheri.
 
Ni kweli nyanya zinaharibika ila siyo kiasi hicho. Zinaweza kuishi hata siku nne bila kuharibika.

Kama unanunua Nyanya za Makopo na kuzitumia sana na tena kutoka Pakistan na wakaguzi wenyewe ndiyo hayo TFDA, basi jiandae siku moja uje uambiwe una KANSA. Vyakula vya Makopo vikimbieni kama Ukoma na utumie tu pale kuna ULAZIMA na huna jinsi nyingine ya kufanya. Mngelijua mnalishwa nini kwenye hayo Makopo, haki ya nani ungelielewa ninasema nini na ungelihakikisha hata saa 12 asubuhi unawahi kwanza sokoni kununua vyakula Fresh na matunda na ndiyo unaenda kazini.

Vyakula vya Makopo? Kila la kheri ila nakuombea Mungu akuepushe na madhara yake kwa uchafu unaowekwa humo ndani.
 
Mkuu mada yako ina maana sana , ila nadhani kuna mambo serikali inatakiwa iyafanye kwanza (hasa kwenye kodi na kusimamia ubora ),ndipo watu wataanza kufikiria hizo home made.La sivyo tutalaumiana bure. Huwezi ,kwa akili ya kawaida ukanunua cement ya dar kwa 15000 wakati kuna cement bora tu kutoka pakistan kwa 12500.
 
Nakubaliana na nyie wote ila si kila kitu jamani Serikali inatuzuia. Hata Kitunguu au Embe mtu ananunua la South Africa.

Kuna vitu kadhaa ambavyo tunaweza kabisa kununua vya Tanzania na tukagoma kununua vya nje. Ila kuna baadhi ni kweli hatuna ujanja na haswa linapokuja swala la bei. Ila utakuta mtu ananunua heineken kwa bei juu ili tu wamuone na yeye ananunua wakati ya Tanzania ipo poa tu. Ukifika Ulaya, heineken ni kitu ya kawaida kabisa na hata wana wapinzani wengi tu ila hao jamaa nawasifu kwa kujitangaza.
 
Sijakataa sikonge ila hali ndo inafanya kuwa hivyo, ila unajua nyanya na mbogamboga zinavyolimwa mwanawane, mie nimeshashuhudia hizi mbogamboga za DAR wanaweka ile sijui mnaita chumvi chumvi tena niliwauliza wakaniambia inakuza haraka sasa wataalamu wa killimo nisaidieni katika hili, sijui kama kuna atakaepona na hiyo saratani

 
Chumvi chumvi ni mbolea Mwanawane. Hata Mtwara ndiyo wanataka kujenga kiwanda cha kutengenezea mbolea.

Zimekuwa zikitumika kwa miaka mingi sana. Nafikiri huwa zipo pale ili kuongezea madini yanayopungua kwenye ardhi. Haina madhara kwa binadamu na kwa ardhi kwa sababu ni vitu ambavyo siku zote zipo ardhini ila ni kidogo. Kwa uzalishaji wa mahidi na tumbaku, inatumika sana kwa mikoa kama huku kwetu Tabora. Kuna ya CHANGARAWE na CHUMVI CHUMVI. Ngoja wataalamu wa kilimo waje watakuelezea zaidi.

Naona Mwanawane wewe mtoto wa mjini maana hata mbolea ya Chumvi chumvi huifahamu? Hata Ulaya wanazitumia sana hizi mbolea na nyingine nyingi kama za kuuwa magugu (Siyo nzuri kwa ardhi na binadamu), kuuwa wadudu nk.
 

Jibu lako kwa Mama Dunia umeua mkuu, hakuna ziada. Vyakula vingi tunavyokula asilimia kubwa vimekuzwa kwa mbolea ya chumvi chumvi. Mama Dunia mtoto wa magorofani huyo, sikumoja atembelee mashamba ya mpunga aone ubwawa wake unavyoshindiliwa chumvi chumvi, ha ha haaaa!! Mkuu ninaafiki hatuna budi kuwa wazalendo kujali vya nyumbani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…