Elections 2010 Saidia Slaa Ashinde [SASA]

Luteni

JF-Expert Member
Joined
Jan 9, 2010
Posts
2,274
Reaction score
302
Katika hatua nyingine, chama hicho leo kinazindua mpango wa Saidia Slaa Ashinde (SASA) katika mkutano utakaofanyika mjini Arusha.

Akitangaza mpango huo, Bw. Wilfred Lwakatare ambaye pia ni Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa chama hicho alisema kuwa mkakati huo ni maalumu kwa ajili ya kumpeleka Dkt. Slaa Ikulu kuwakomboa Watanzania.

"Mabadiliko ya nchi ni SASA, maendeleo ya nchi ni SASA, kumpeleka Slaa ikulu ni SASA," alisema Bw. Lwakatare.

Alifafanua kuwa chama hicho kitatumia SASA kufungua akaunti maalumu kwa ajili ya kuchangisha fedha za kumsaidia mgombe wao. Ukitaka zaidi soma hapa HAPA

 
Sio siri jamaa anajenga hoja. Asiyemchagua basi tena, huyo atakuwa mchawi...
 
Yah, Mungu kasikia kilio chetu! Natoa onyo kwa hao waharamia wa demokrasia na wale vibaraka wanao tumika kupora kura za watu, ebu muogopeni Mungu wenu, kuweni waungwana na muache haki itendeke. Hata ndugu yetu JK, siku zote tumekuita Muungwana, dhihirisha uungwana wako kwa kusimamia haki itendeke, na kama hutachaguliwa kubali matokeo na utakuwa umeandika historia nzuri itakayo kulinda maisha yako yote.
 
Nimeikubali hiyo filosofia..wanaiweza kwa kweli..
Muda wa mabadiliko ni sasa..Finally "The time for change"
 
Hiyo akaunti imeshafungliwa au bado?by the nice motive imetumika ili kumchaguamrithi wake.
 

"Mabadiliko ya nchi ni SASA, maendeleo ya nchi ni SASA, kumpeleka Slaa ikulu ni SASA,"
 
Nasubiri akaunti namba jamani. Ikiwezekana uwekwe utaratibu wa kumchangia kwa njia ya sms pia
 
Nasubiri akaunti namba jamani.


Kwa sasa michango kwa ajili ya ziara za Dr Slaa inaweza kupitia kati ya akaunti zifuatazo wakati akaunti nyingine inafunguliwa:

Benki: CRDB, Akaunti Namba: 01J1080100600, Jina: CHADEMA M4C

Au

Benki: NMB, Akaunti Namba 2266600140, Jina: Chama Cha Demokrasia na Maendeleo

Ukiweka mchango tafadhali itaarifu ofisi kupitia info@chadema.or.tz

JJ
 
Asante sana Mnyika kwa akaunti hizi na hiyo nyingine itakapofunguliwa mtujulishe. Unajua hata Obama aliweza kuvunja rekodi ya michango kwa kuwa ilikuwa rahisi na wazi kujua ni sehemu gani utachangia kuliko kuficha akaunti, shukrani tupo nyuma yenu na Mungu atawatangulia.

GO Slaa GO
 
CHADEMA tupeni namba za simu ambazo tutaweza kuwatumia hela kwa M-Pesa au ZAP. Hiyo ni rahisi na nyepesi zaidi.
Shime watanzania TUMCHANGIE Dr. Slaa mpambanaji mlalahoi na mzalendo hasa maana hii ni zamu yetu wazawa kujitawala.
 

Sijawahi kuchangia fedha chama cha siasa..... lakini sasa huo mwiko nitauvunja. CHADEMA watapata mchango wangu.... soon!
 
jamani hilo suala la Mpesa ni muhimu sana kuwa nalo kwa sababu watu wanasisimka na kushawishika wanapo hudhuria hii mikutano na Dr (mheshimiwa rais MTARAJIWA) anapo hutubi mimi ningependekeza kuwepo na njia rahisi ya watu kuchangia wakati mikutano hio inaendeleA wanaweza kuwaambia wanachama na wakereketwa watume messege kupitia no fulani au njia yoyote inayo enekana inafaa kutokana na mazingira waliopo waheshimiwa
 
Mwili unanisisimka kwa jinsi mipango mizuri inavyoendeshwa katika harakati za SASA na sio ile ya kiharamia waifanyayo kwa uficho wale jamaa zetu.
 
Mpesa pls; mnyika fanay hili haraka watu huko wanaona ndio huru zaidi; mfumo wetu una matatizo na kuuondoa tutumie njia nyingine; very simple tafuta line moja ya voda then isajili au ya mtu tu mwaminifu kwa chama then itangazeni; silaha zote zitumike pls mhimu sana
 

Tunaomba SWIFT na IBAN codes za benki ili tulio nje tuchangie.
 
Ninaweka mchango wangu kesho.

Nitatuma email info@chadema.or.tz kuwaarifu

Na nitamtumia John Mnyika kwenye No yake 0784222222.

Nitawafahamisha na marafiki zangu walioko kwenye email list yangu juu ya record hii sasa hivi

Dr.SLAA- Mungu amesikia kilio cha wanyonge.....

Mungu akubariki na hakika utashinda.......... na wanyonge tutashinda na SLAA
 

kama umemsoma vizuri mnyika ajasema umpigie wala kutaja namba yake hapa soma vizuri kwa juu tuma info at....inatosha na si kumtumia msg ama kumpigia tuheshimu usiri wa mtu....ahsante kwa mchango wako
 
Tunaomba SWIFT na IBAN codes za benki ili tulio nje tuchangie.

CRDB'S SWFT CODE: CORUTZTZ

Kwa taarifa zaidi hebu angalia hiyo link!

https://www.jamiiforums.com/business-and-economic-forum/31734-tanzanian-banks-swift-codes.html
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…