Saido Mane anastahili ballondoir

Joined
Jul 18, 2019
Posts
33
Reaction score
32
Baada ya kushinda Uefa na hivi leo kama atashinda Afcon ni jambo lisilopingika, Sadio Mane anastahili kuwa mchezaji bora wa dunia.
 
VP kuhusu Allison Becker maana naye ana copa America gilokipa bora UEFA Champions league pia epl na amechaukua kikombe cha UEFA Huon Kama amepitwa nashangaa huyu atajwi Sana
 
Sioni kwa nini asiwe walau top3, kama zi kuwa winner wa ballon d'or, kafanya vyema sana katika club yake na hata timu ya taifa ya Senegal.

Mane alipata golden boot EPL, moja ya league bora ulimwenguni, ubingwa wa UCL, na sasa anaweza pata ya golden boot AFCON na pia kunyanyua AFCON.

Kama ubaguzi ukiwekwa kando statististics zinamruhusu kutwa tuzo hii. Ni kipi haswa kitazuia yeye kupata tuzo hii????
 
Hiyo tuzo ilikua na ladha zamani tu kwasababu alipewa aliyestahili kwa uwezo na kipaji alichonacho.. siku hizi ukiwa na kajina tu na timu yako ikapata mafanikio basi unapewa haijalishi hata mchango ulioutoa.. tena ukifunga goli fainali ndo utaonekana kama mungu vile...bila kujali huko mwanzoni ulipuyanga ama vip
 
Hawezi pata. Hawa akina Mane wanajitutumua mno wakati wakicheza Ulaya lkn hapa Afrika hawajitumi. Hawana uzalendo wa ukweli. Wanaangalia maslahi zaidi.
 
Ubaguzi nao ni kikwazo sana
 
Kwa maoni yako mleta mada sasa rasmi Sadio Mane hafai kutwaa ballon d'or
 
Ballon d or sio maandazi kwamba kila mtu anaweza pata..
Ukiangalia fact ya makombe basi ALVES anaweza kuwa GOAT kumzidi hata pele na maradona maana kwenye career yake kachukua makombe zaidi ya hao jamaa wote.

Mpira ni kiwango binafsi + jinsi unavyosaidia team. Na sio mafanikio ya team yako tu..
Mane hana kiwango binafsi cha kumfikia Hazard hapo sijataka kumuongelea Messi na ronaldo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…