Saido Ntibazonkiza amemzidi Mayele kwa vigezo vya ufungaji bora, tuache siasa

Leonel Ateba Mbinda

JF-Expert Member
Joined
Feb 20, 2023
Posts
644
Reaction score
2,695
Kwann Ntibazonkiza anastahili ufungaji bora baada ya kufungana sawa na Mayele? Hizi ni sababu ambazo Bodi ya Ligi inapaswa kuzizingatia.

1.Saido alikuwa Geita Gold, mzunguko wa pili amehamia Simba, hivyo kujiunga na timu mzunguko wa pili na kisha ukafunga mabao 13 katika timu mpya ni dhahiri anastahili ufungaji bora.Mayele amecheza Yanga mwanzo mwisho.

2.Saido ameondoka na hatrick mara 2 ukilinganisha na Mayele.

3.Saido ana assists 12 Mayele 4

4.Saido ni kiungo mshambuliaji wakati Mayele ni pure striker lakini kiungo mshambuliaji kafunga mabao sawa na real striker.

5.Saido kacheza mechi chache ukilinganisha na Mayele.

6.Saido amefunga mabao 5 mechi moja, Mayele hajawahi kufikia rekodi hiyo.

7.Saido amefanya maajabu hayo dakika za mwisho na hivyo kuibua hisia kali had Yanga wakaamua kumsafirisha Mayele kwa ajili ya mechi ya mwisho.

Wale wanaobisha kwa facts, waje waniprove kwa kuweka vigezo vyao kwann Mayele apewe badala ya Saido.Napokea maoni.
 
Aisee acha utani na huyo Mzee kwa magoli ya kupika!

Hivyo ni vigezo vyako, ni bora ungekaa kimya ili ufiche upumbavu wako.

Your browser is not able to display this video.


 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…