Saidoo Saidoo dah

Saidoo anatakiwa aondoke baada ya msimu huu.
Nachelea kusema uongozi wa simba ndio wenye kumng'ang'ania saidoo
Walishasema anamalizia msimu huu jamani! Ila ka Saido ni kazee. Nimewahi kukahudumia kwenye makambi ya wakimbizi Kigoma hako!
 
Walishasema anamalizia msimu huu jamani! Ila ka Saido ni kazee. Nimewahi kukahudumia kwenye makambi ya wakimbizi Kigoma hako!
Dirisha dogo la January aliongezewa miaka miwili, bado yupo sana godfather wa Bujumbura
 
Daa nashukuru sasa watu wengi wameona mapungufu ya Saidoo. Na ile mechi ya Wydad hapa Dar Saidoo angecheza Simba angefungwa na sasa hivi tungezungumzia Simba kukamiisha ratiba tu. Niliwashauri viongozi wa Simba hapa kwenye dirisha dogo wamuache huyo Saidoo ili Benchika wakati anapanga listi asiwe anamuona maana huyo jamaa sijui ana mzizi gani maana panga pangua ya wachezaji 11 siyo ya Robertino wala Benchika yupo ndani kikosi. Na akicheza na Jwenang basi mashabiki wa Simba wajiandae kisaikolojia kwa kukaa roho juu maana hata Simba akipata ushindi utakuwa wa taabu na mateso mengi.

Saidoo ni mchezaji hewa ila ni mpaka ujue mpira kiundani ndio utagundua hilo. Anakimbia kila sehemu ya uwanja na kutoa jasho jingi sana lakini ufanisi sifuri. Mipira mingi inafia miguuni kwake na kuifanya Simba safu ya mbele ya Simba isipate huduma inavyotakiwa. Kwa kifupi jamaa anaikaba timu yake mara nyingi kuliko anavyoisadia.
 
Sioni faida ya Saidoo anavheza mpira wa ubinafsi sana ni ujinga kumuacha miquesone nje
 
Sioni faida ya Saidoo anavheza mpira wa ubinafsi sana ni ujinga kumuacha miquesone nje
Nilisema hapa juzi kuwa aliye karibu na Miquisone amshtue aondoke zake Simba akatafute timu itakayoweza kumtumia vizuri kwani benchi la ufundi Simba halijui namna ya kumtumia. Kumpanga Saidoo dakika 87 halafu Miquisone unampa dakika 3 huo ni uzwazwa. Hili limesababisha Miquisone akose "match fitness" aliyoipata baada ya Mapinduzi Cup sasa amerudi tena kujitafuta upya.

Mpira ni mchezo wa wazi sana na Saidoo dakika zake za kucheza vizuri hazizidi 30 baada ya hapo ni kuanguka anguka na kuua "move" ya timu basi. Mbaya zaidi hachezi kitimu anataka afunge mwenyewe wakati timu nzima inaharibikiwa yeye wala hajali. Hivi benchi la ufundi limepewa nini na huyo Saidoo kiasi huwa halioni madudu yake uwanjani? Na viongozi wapo kimya lakini wakumbuke timu ikifanya vibaya wao ndio hupelekewa lawama zote na mashabiki.
 
UTOPOLO nimegundua walikuwa wanasubiri kuingia robo fainali kwà hamu sasa furaha imezidi afya ya akili kifupi MASHABIKI wa UTOPOLO hawako sawa
 
UTOPOLO nimegundua walikuwa wanasubiri kuingia robo fainali kwà hamu sasa furaha imezidi afya ya akili kifupi MASHABIKI wa UTOPOLO hawako sawa
Hakuna mwanayanga anaefurahia robo final kwasababu ni kitu cha kawaida tu ndio maana simba anafika mara kwa mara tunachofurahia ni kumpiga mtu 4 halafu wakawa wanagombana wenyewe
 
Mbona watu wa Yanga ndiyo wanatumia nguvu kubwa kutuaminisha kuwa Saido ni Mzee na anaighalimu timu? Hayo mnayoyaona ninyi Ina maana Kocha Mkubwa kama Benchika hayaoni?
Any way, tufanye Benchika haoni kama mnavyoona nyie, si ndiyo kwenu mngefurahia? Maana anguko la Simba ni furaha kwa Yanga, kwa nini mnatustua mapema kuwa Saido anaighalimu Simba?
Msiaminishe tatizo mahali ambalo hakuna tatizo!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…