Kwa kufahamu mikinzamo iliyopo kati ya akili na tiba ya nguvu za kiume na madhara yachipukiayo imebainika kuwa, mtu anaweza kujitibu tatizo hilo kwa kutumia kanuni za kisaikolojia na mafanikio yasiyo na madhara yakapatikana. Wataalamu wa kisaikolojia wanatambua kuwa kanuni ya ufanyaji mapenzi iko zaidi kwenye ubongo kuliko mwilini. Kinachotokea hadi mtu akapata msisimko wa kufanya mapenzi si mwitikio wa mwili, bali ni utambuzi wa akili juu ya kiwango cha mapenzi kilichopokelewa kwenye ubongo unaojihusisha na hisia.