Saikolojia: Watanzania wengi ni Waoga kwa utafutaji Maisha.

Saikolojia: Watanzania wengi ni Waoga kwa utafutaji Maisha.

bnyanya

Senior Member
Joined
Sep 27, 2013
Posts
178
Reaction score
63
Nionavyo mimi, watanzania wengi ni waoga wa utafutaji maisha. Wengi wanapenda maisha ya dezo...kukaa tu na kusubiri kufanyiwa michongo au maisha ya gwelele. Wanapenda vitu vikubwa na masifa ya kijinga wakati uwezo wa kutafuta maisha hawana.


Ndio maana hata leo tunakosa wagunduzi au watu wenye mawazo chanya kwa ajili ya kudumisha taifa letu.


#RiskTaker ni mtu wa namna gani??


Ukiangalia kipindi cha #MaishaPlus - utagundua: laiti kama watanzania tungekua tunaweza kuishi maisha kama hayo toka awali....nchi yetu ingekua na maendeleo makubwa.


Kwani watanzania wengi wangesambaa nchi mbalimbali kama walivyo nchi za wenzetu mfano WAGHANA,WA NIGERIA, WACHINA etc.


Si tukalia wizi tu na majungu!!!!
 
Ni shehemu gani ya nchi ya Tanzania haina watanzania hadi wakasambazwe huko?

Kwa hiyo, hao wagunduzi wa mambo ya maana kwa taifa, ni function ya kusambaa nchini tu?

Unadhani 'Model ya maisha' ya maisha plus pekee inaweza kutukwamua tulipo?

Unantania aisee
 
Kwani watanzania wengi wangesambaa nchi mbalimbali kama walivyo nchi za wenzetu mfano WAGHANA,WA NIGERIA, WACHINA etc.

Si tukalia wizi tu na majungu!!!!

Watu wengi wanaosambaa sana nchi zingine na hata mikoa mingine huwa population yao inakuwa kubwa mno na kunakuwa na tatizo kubwa linalowafanya wasambae hivyo.Mfano wachaga wana tatizo kubwa la ukosefu wa ardhi kule kilimanjaro hivyo utakuta ndio wanaongoza tanzania kusambaa mikoa yote.

Ukienda KENYA,GHANA,NIGERIA NA CHINA zina idadi kubwa ya watu na matatizo makubwa ya ukosefu wa ardhi, ajira na makazi na hivyo kuwafanya wawe kazi yao kuzunguka kutafuta maisha nchi zingine.Nchi ikiwa na uhakika wa maisha hata wa kiwango kidogo kwa mahitaji yale makubwa matatu ya chakula,malazi na mavazi utakuta watu si wahamaji sana kuzurura nchi za watu sababu walipo japo wanapata kidogo lakini wanaona chatosha kuendelea na maisha.Nchi nyingi tu zina watu wachache sana nje na watu wake wako vizuri kwa viwango vyao sababu satisfaction is subjective kwa kila mtu. Si kila mtu unachoona wewe KIZURI wakihitaji mtu mwingine naye aona akihitaji. Waweza ona kwenda nje ya nchi ni kuukata mwingine anaona ujinga tu wala hawazi na hana mpango wa kwenda nje ya nchi hata umpe tiketi ya bure na umlipie kila kitu.Ameridhika alipo apatacho na aishivyo.

Kusambaa sana nchi za watu hakumaanishi kuwa mtu atokako kuko vizuri au asiyesambaa basi hana akili na hajui kutafuta fursa nchi zingine.Wahenga wanasema ukitukana mke wa mtu haifanyi mkeo awe mzuri kama ni mbaya.
 
king zapata: Elimu ya ujariamali pekee haitoshi. Woga ndio unatusumbua. Wengi wamezoea maisha ya spoonfeeding!..kulialia kila mara....madeko mengi.
 
Last edited by a moderator:
Money Stunna: Kwa mtazamo wangu mimi....kwanza awali ya yote nashukuru kwa swali zuri. Na haya ni mambo ya msingi tunayoweza kufanya.


1. Hawa jamaa wa CCM ndo wametupa maradhi haya. Tuwapige chini 2015.

2. Tuwe creativity kutengeneza migomo na maandamano bila uwoga kama nchi nyingine mfano Ukraine, Greece, Rusia etc :#Lengo: kusafisha viongozi wa ajabu ajabu wenye lugha tamuu bila matendo..eg. Kikwete na wengine ambao wanajisahau mpaka wanaongea ujinga #division 5 etc

3. Mariasili ni ya wote. Tuwe wakali kabisa kwenye hili.


Tell you wat?..viongozi wetu na baadhi ya wafanya biashara na mashirika flanflan wanachofanya ni like...


Wanachukua kitu chenye thaman let say..sh. Bil 5....na wanakuja kutudanganya kwa vitu vya thaman ya sh. Mil.100....bila kujua na kujali tunafurahia kama mazuzu.



4. Tuwe majisiri aisee kama watu8 na kina kb52


3.
 
Last edited by a moderator:
badiebey: we utakua na minyoo si bure!!
 
Last edited by a moderator:
watanzania uliowagusa hapa..
naomba waondoe wachaga na wakinga...
labda wazee wavibarazani maeneo ya pwani.
 
2. Tuwe creativity kutengeneza migomo na maandamano bila uwoga kama nchi nyingine mfano Ukraine, Greece, Rusia etc :#Lengo: kusafisha viongozi wa ajabu ajabu wenye lugha tamuu bila matendo..eg. Kikwete na wengine ambao wanajisahau mpaka wanaongea ujinga #division 5 etc


3.

Nilifikiri kama mtaalamu wa saikolojia ukiongelea creativity unazungumzia ubunifu wa biashara au ubunifu wa teknolojia ya kusaidia watu kuondokana na umaskini wa mtu binafsi au taifa, Kama creativity ni kubuni maandamano na migomo basi creativity ya wasomi wa nchi hii has a very long way to go na itachukua miaka karne nyingi watu wasiosoma kujua mchango halisi wa wasomi wa nchi hii kwao.
 
ile safari yako ya Ghana ulikuwa unafanya utafiti?
back to the topic ni kweli vijana wengi wanabweteka wanapenda kuishi kwa mazoea.
 
Matatizo yetu yanaanzia tangu Utotoni ,tunafundishwa kwa kutishiwa kuanzia shuleni mpaka nyumbani.Mfano mdogo tu siku hizi watoto wa shule binafsi wakihojiwa unaona wanajiamini zaidi kuliko wa shule zetu za kawaida za serikali.Watanzania wengi ujanja mdomoni tu akivuka mpaka hasa wa kaskazini ni waoga balaa.
 
Nionavyo mimi, watanzania wengi ni waoga wa utafutaji maisha. Wengi wanapenda maisha ya dezo...kukaa tu na kusubiri kufanyiwa michongo au maisha ya gwelele. Wanapenda vitu vikubwa na masifa ya kijinga wakati uwezo wa kutafuta maisha hawana.


Ndio maana hata leo tunakosa wagunduzi au watu wenye mawazo chanya kwa ajili ya kudumisha taifa letu.


#RiskTaker ni mtu wa namna gani??


Ukiangalia kipindi cha #MaishaPlus - utagundua: laiti kama watanzania tungekua tunaweza kuishi maisha kama hayo toka awali....nchi yetu ingekua na maendeleo makubwa.


Kwani watanzania wengi wangesambaa nchi mbalimbali kama walivyo nchi za wenzetu mfano WAGHANA,WA NIGERIA, WACHINA etc.


Si tukalia wizi tu na majungu!!!!

UNACHOKISEMA SI KWELI,PENGINE HUNA TAARIFA ZA KUTOSHA KUHUSU NAMNA GANI WATZ WALIVYO MAHODARI KUTAFUTA MAISHA NDANI NA NJE YA NCHI.
1:KWA NDANI YA TZ:NENDA MIKOANI SEHEMU YEYOTE YENYE MIRADI KWA MFANO YA UJENZI WA BARABARA AU MIGODI AU SEHEMU NYINGINE ZINAZOFANANA NA HIZO NDO UTAJUA NI JINSI GANI WA TZA KUTOKA KILA PEMBE YA NCHI WANAVYO SURVIVE KATIKA MAZINGIRA MAGUMU WAKITAFUTA MAISHA.
2:KWA NJE YA NCHI-USITAZAME MAREKANI NA UK----FUATILIA NI WATZ WANGAPI WANAOENDA SOUTH AFRIKA KUTAFUTA MAISHA HATA KWA MIGUU(ref.radio free afrika ___sintasahau _____rojaz___);NENDA CONGO AMBAKO KUNA VITA LAKINI WABONGO WAPO WANACHEMKA,NENDA SUDAN,HUKO NDO UTAKUTANA NA WATAALAM KUTOKA TZ,NENDA LICHINGA UTADHANI NI MJI WA KINA MASAWE..........MKUU NI VYEMA UKATAFUTA DATA ZA UKWELI KUHUSU WA TZ......HAPO HATUJAZUNGUMZIA NI WANGAPI WANAO RISK MAISHA KWENYE DEAL HARAM,WEWE WABONGO HUWAJUI......TENA HATUJAZUNGUMZIA NI WASOMI WANGAPI WA BONGO WANAOHESHIMIKA NCHI ZA WATU KWA KUFANYA MAMBO YALIYO TUKUKA.......KWA KIFUPI UMEZALIWA AFTER .....1985......
 
matatizo yetu yanaanzia tangu utotoni ,tunafundishwa kwa kutishiwa kuanzia shuleni mpaka nyumbani.mfano mdogo tu siku hizi watoto wa shule binafsi wakihojiwa unaona wanajiamini zaidi kuliko wa shule zetu za kawaida za serikali.watanzania wengi ujanja mdomoni tu akivuka mpaka hasa wa kaskazini ni waoga balaa.

tafadhali fafanua kaskazini ipi?
 
Back
Top Bottom