Saikolojia ya chakula na shibe

Saikolojia ya chakula na shibe

uvugizi

JF-Expert Member
Joined
Oct 13, 2012
Posts
1,278
Reaction score
956
Tunavyokula kuna athiri jinsi tunavyojisikia. Inatakiwa unapokula uwe unajisikia vizuri. Kuna wengine wakila wanajisikia tofauti. Ukila sana au kidogo vyote vinaweza kukufanya kusikia vibaya , hata kuleta madhara katika mwili.

Kuna vitu vingi sana vinaweza kuathiri ulaji wetu. Aidha inaweza kuwa, ni utamaduni, mabadiliko ya kidunia, kijamii, ya mtu mwenyewe, hali ya kiuchumi na kisaikolojia.

Kuna watu wengi sana imebainika kuwa wanatumia chakula kama mbadala wa hali zao wanavyojisikia. Aidha mtu anaweza akawa katika hali ya kuchoka, hasira, mfadhaiko, furaha . Imebainika huwa wanaenda kula na kunywa kama mbadala wa hizo hali. (use food as a coping mechanism to deal with stress, boredom or anxiety, even joy). Kwa kufanya hivi huwa kuna hasara zaidi kuliko faida.

Kwa upande wa kisaikolojia. Kuna mtaalam mmoja anaitwa brian wansink the head of the Food and Brand Lab at America Cornell University. Huyu ni food psychologist katika kitengo cha consumer behavior and nutritional science. Katika kitabu chake anaeleza jinsi watu wanavyokula pasipo kujua ametanabaisha kuwa, kula kwa mtu sana au kidogo sana ni swala la kiakili na si njaa pekee.

Anaelezea saikolojia ya chakula na mazingira yake, anaelezea, wapi, kiasi gani na wakati gani watu wanakula.

Anasema kuna mtu anakula kwa mazoea na kwa hamu. anaelezea kuwa utamgundua mtu alivyo , kwa ukubwa wa sahani aliyo beba , hata kupelekea kujua tabia zingine na kiasi cha njaa /hamu aliyo nayo . anasema watu hula sana wakiletewa chakula katika bakuli lenye uwazi mkubwa kwa juu. Hapa nilikumbuka masinia ya wali katika sherehe za uswahilini.

Katika tafakuri zake anasema hotel zenye misingi ya afya watu huwa wanakula sana, hata kama wanadanganywa.

Ametumia muda mwingi kusoma vile ambavyo watu hawavioni. Je, ni jinsi gani vifungashio vinaathiri ulaji wetu. Anaelezea hata namna ya kushusha uzito ingawa si kitabu cha diet.

Ila mwisho anasema ule kidogo na ufurahie chakula, siyo ule sana na ukichukie chakula.
 

Attachments

Back
Top Bottom