Jacob Mulikuza
Member
- Jul 15, 2021
- 16
- 61
Thomas Edison ni mgunduzi na muasisi wa kanuni za msingi za umeme aliyeishi kati ya mwaka 1847-1931. Wakati Thomas akiwa shule ya msingi walimu wake walisema ni mjinga na hana uwezo wa kujifunza hivyo ikampasa Thomas kuacha shule na kurudi nyumbani. Aliporudi nyumbani, Thomas alianza kufundishwa na mama yake na alipata fursa ya kujifunza kile anachopenda.
Akisomea nyumbani, alitengezeza maabara yake ya sayansi aliyoshirikiana na wenzake kujaribu mawazo yao kwa pamoja na kwa uhuru kabisa bila kujali kuwa watakosea au la. Walitumia fursa hiyo ya kukosea kwa pamoja mpaka walipofanikiwa. Kutoka kwenye maabara hii ya sayansi, ndugu Thomas aligundua balbu ya umeme, betri ya kuhifadhi alkali, kamera ya kunasa picha mtembeo, telegrafu na santuri. Haya yote tunaona yameleta magueuzi makubwa sana katika sayansi.
Wakati Fulani akihojiwa na waandishi wa habari aliwezaje kugundua balbu ya umeme alisema kuwa alijaribu mara 10,000 ndipo alipofanikiwa ila Thomas mwenyewe alisema, namnukuu “Sikushindwa ama kufanya makosa, ila nilijifunza njia tofauti 10,000 ambazo hazikuwa sawa”.
Nimeona ni vyema kuanza makala hii kwa kurejea kisa cha ndugu Thomas, kuona ni kwa namna gani makosa ni sehemu muhimu sana kwenye ukuaji na mafanikio ya binadamu. Ila, utashangaa kuona vile ambavyo katika ukuaji wetu kama binadamu tumefundishwa kufanya makosa ni kutu kibaya na cha kuepukwa.
Taasisi kubwa inayochangia kudidimiza makosa ni shule, wengi wetu tumepitia mfumo rasmi wa elimu ambao umetufundisha kufanya makosa ni kitu kibaya na endapo utafanya makosa utaadhibiwa kwa makosa yako. Mfumo wetu wa elimu umetengenezwa kwa namna ambayo mifumo husika ya ufundishaji inapaswa kufanya kazi kama kiwanda cha uzalishaji bila kujali tabia za kibinadamu zenye kuruhusu udadisi na namna tofauti ya kutenda. Nyote mtakumbuka mkiwa shuleni na kupewa mitihani ama majaribio na ukikosea lazima unaadhibiwa na kuonekana uwezo wako wa kufikiri ni mdogo kwa kuwa tu umesema kitu tofauti na kile ambacho mfumo wa elimu ulishakubali kuwa ndio sahihi.
Athari za mfumo wa elimu umeua vipaji vyetu, utayari wetu kujaribu, utayari wa kukosea tena na tena, ujasiri na kutufanya kuamini makosa ni kitu kibaya kwenye jamii na hayapaswi kuzingatiwa wala kuruhusiwa. Kutokana na hili sasa, tumepata ugonjwa wa kisaikolojia unaotufanya kuwa waoga wa kila kitu katika maisha yetu kwa hofu kwamba tutakosea.
Kwa kushuhudia hili, wengi wetu hatuna maendeleo binafsi hususani kiuchumi kwa kuwa tunaogopa kukosea na kuendelea kufanya mambo yale tu ambayo jamii imeyakubali kuwa ndio sahihi hivyo ukiwa na wazo tofauti ama kutaka kutenda jambo tofauti unaonekana mkosaji na unaweza kuadhibiwa ama kutengwa na jamii.
Kwa mfano, leo hii ukitaka kufanya biashara fulani cha kwanza unawaza ukishindwa itakuwaje, ukifanya tathimini ya faida na hasara ukaona hasara ni nyingi unaacha na kukata tamaa. Sisemi ni vibaya kufanya upembuzi yakinifu kabla ya kufanya biashara la hasha! Ila jambo ambalo hatulifikiri ni namna ya kugeuza zile changamoto kuwa fursa badala yake tunaogopa kujaribu na kuacha kwa uwoga kuwa tutashindwa.
Kwa muktadha huu pia, ukiwashirikisha marafiki zako juu ya jambo unalotaka kufanya wataanza kukukosoa na kukubeza kuwa wewe ni nani ufanikiwe huoni watangulizi wako walishindwa na wewe huwezi kufanikwa, ni kauli utazisikia mara nyingi.
Mifano hii ni mingi sana, ila kitu cha msingi kufahamu ni kuwa, kutokana na mifumo mbalimbali tuliyonayo kwenye jamii yetu leo hii utagundua kuwa haithamini makosa hata kidogo na badala yake adhabu ndio huonekana kuwa mbadala wa makosa.
Jitathimini pale ulipo sasa iwe kazini, shuleni, kwenye familia, kwenye jamii na kwingine kwingi hakuna mtu yuko tayari kuona ukikosea wanategema uendane na kile kilochozoeleka na mwishowe inatufanya kuwa wategemezi kwa wale wachache wenye uthubutu na wako tayari kukosea.
Tizama leo hii mathalani, nchi yetu ina mabilionea wangapi, wanamichezo mahiri wangapi, wanasayansi mahiri wangapi na wengine wengi, utagundua wako wachache sana kwa sababu walikuwa tayari kwenda kinyume na mifumo ya hofu ya kushindwa na kufanikiwa. Ni ukweli kuwa ukiwa kwenye dimbwi la uoga na hofu ya kukosea huwezi kufanikiwa hata katika jambo dogo na hii inaathari kubwa kwenye saikolojia ya mwanadamu yeyote yule. Wengi wetu huogopa kufanya jambo fulani kwa hofu ya kuwa jamii ama watu watanionaje, je nikikosea watanichukuliaje na mengine mengi.
Ni muhimu kutambua ya kuwa, kufanya makosa ni jambo la muhimu sana katika maisha ya binadamu kwani uwepo wetu hapa duniani umelenga kufanya mambo kwa upeo mpana sana bila kuwa na vikwazo vya kudumisha upeo huo.
Kuna faida nyingi sana za kufanya makosa mara kwa mara kwani husaidia mtu kujitambua, kugundua kipaji husika, kuleta ugunduzi fulani, kutatua changamoto za maisha katika jamii, kuleta mawazo mbadala, kubadilisha sura ya ukweli katika jamii, kuboresha afya ya ubongo na akili na nyingine nyingi.
Wanasayansi wanakadiria wanadamu tuliowengi tunatumia tu 10% ya ubongo wetu ili hali tunaweza kutumia asilimia zote 100. Na hili linatokana na ukweli kwamba, tumefundishwa kuona ukomo wa ubongo wetu kwa kutoruhusu kufanya jambo lililo nje ya utaratibu maarufu kama makosa, hivyo ubongo wetu unaishia kutuonyesha kuwa uwezo wetu unaishia katika mambo tuliyoyazoea na sio zaidi ya hapo.
Ni muhimu sasa mifumo yetu ya jamii kuanza kuona haja ya kuchochea makosa ili kuwapa watu fursa ya kuwaza nje ya boksi kwa mantiki ya kutaka kujua zaidi, kujifunza, kugundua vipawa na kuona fursa nje ya zile tulizozizoea. Ilikuwa fahari kumsikia Rais Samia Suluhu Hassan akigusia haja ya kuanza kurejea mitaala yetu na kuona haja ya kuibadilisha ili kutoa elimu yenye kuchochea udadisi zaidi itakayofanya tuwe na taifa la watu wenye maono tofauti na haja ya kuleta maendeleo yao binafsi na kwa taifa kwa ujumla.

Upvote
33