Saikolojia ya Mahusiano: Fahamu tabia za watu wasiofanya maamuzi hayohayo mara mbili

Saikolojia ya Mahusiano: Fahamu tabia za watu wasiofanya maamuzi hayohayo mara mbili

spleen

JF-Expert Member
Joined
Apr 24, 2013
Posts
4,079
Reaction score
6,788
Binadamu ni kiumbe cha ajabu sana,kila kundi la binadamu huongozwa na tabia tofauti tofauti,hebu chukulia huu mfano,hujawahi kuta kuna kijana ametoka familia ya kitajiri tu yenye uwezo na ana akili na tabia za wastani.

Au hujawahi ona mdada alikua na mahusiano kwenye ujana wake na wanaume wanaojilewa ila anaishia kua kahaba tu akiuza buku mbili au anaishia kua bar maid,mchoma vitumbua anayeunga unga mtaji.

Mara zote watu hao huangukia kwenye kundi la watu wasiofanya maamuzi mara mbili mbili. Kupitia uzi huu tutaona kwa kirefu kwa nini kundi hili huwaathiri zaidi wanawake kuliko wanaume. Unakuta baba ana hela anamuita mwanae,sasa tukupekele shule ya ufundi,......si unajua zile jeuri za watoto,..."aaah sitaki mimi nataka niwe msanii",unakuta dogo kipaji hana anapigika miaka miwili kwenye usanii anarudi nyumbani analia anataka shule,mzazi anamkazia na hela anazo vizuri tu,ndio imetoka hio ukiwa mpiga debe,teja,kahaba, mzazi ameshamaliza hivo.........Unaweza dhani ni ukatili fulani hivi wa kigaidi[emoji3][emoji3],kumbe ni tabia tu "psychology",ni jinsi tu mtu alivoumbwa.

Wadada hukutana sana na wanaume wa dizaini hii[emoji846][emoji3],unajua saikolojia ya watu wa namna hii wengi hujiamini,wenye akili na wana mafanikio,kwa tamaduni za mwafrika mwanamke ni kiumbe ambaye hana usawa kama mwanaume,nchi zingine kawaida sana kwa mwanamke kumfuata mwanaume na kuanzisha maisha yao ya ndoa,Kwa huku ni kinyume chake.

Kuna kundi kubwa la wanawake wanajuta maisha yao yote,sababu kama utamaduni wa mwafrika ulivo,mwanaume humfuata mwanamke,hata kama huyo mwanamke ana hisia na kumpenda mwanaume atajifanya hamtaki[emoji3][emoji3][emoji23]...........Ndio ile mwana kakamilika kila idara anamfata mwanamke anaanza kumletea nyodo,wengine huenda mbali zaidi kuleta dharau,kutaka matumizi ya bei ghali,ili tu kumkomoa dume,........si kashazoea waigizaji hawachokagi[emoji3],...........dizaini ya watu wasiofanya maamuzi mara mbili,wao wakiona tu "alarm" hawarudi tena,hata wawe na hela kama "Elon Musk"[emoji23][emoji23],.........yaani ukitongozwa tu ukaleta "bad attitude",kibuli,matusi na kizalilisha ndio nitolee hio..........kuna maelfu ya wasichana kwenye umri chini ya miaka 30,wameshawahi kukutana na hili kundi la wanaume na kubaki na majuto maisha yao yote,....kuna wengine hadi wanaamua kuzaa tu ama ndio ile kuolewa na yeyote yule.

Unakuta jamaa tu mstaarabu hana lile wala hili anakutana na mdada sehemu ngeni anaamua kuomba mawasiliano yake,kwa nia njema tu,......mdada "emotional" anaanza kumtolea jeuri,nyodo,......jamaaa anaamua ahirishe zoezi,na sio "temporary" ni "permanent"....usidhani mdada atatulia[emoji3][emoji3],lazima amfatilie jamaa kujua ni mtu wa namna gani,anagundua jamaa ni wale wanaume aliokua anawahitaji sana maishani mwake,...lakini ndio hivo tena jamaa ni aina ya watu wasiofanya maamuzi mara mbili.
Umeshawahi kukutana na watu wa namna hii?,hebu tupeni uzoefu wenu wadau
 
Binadamu ni kiumbe cha ajabu sana,kila kundi la binadamu huongozwa na tabia tofauti tofauti,hebu chukulia huu mfano,hujawahi kuta kuna kijana ametoka familia ya kitajiri tu yenye uwezo na ana akili na tabia za wastani.
Kuna mfanya kazi mwenzangu hapa ofisini kanipiga chini sababu nimeoa, sasa mimi bado namlia tageti isije ikawa na yeye hafanyi maamuzi yaleyale mara mbili.
 
Watu wa hivyo huwa Ni wazuri sana kwenye Yale maamuzi yenye tija sana.

Ila kwa Yale yanayohitaji tafakari ya kina na utulivu Lazima wapuyange.

Mfano mzuri Ni marehemu JPM[emoji18]
[emoji117]Kwenye suala la CORONA-Aliupiga mwingi sana mpk anaingia kaburini.

[emoji117]Kwenye suala la KOROSHO mtwara- Alipuyanga sana mpk leo hii wamakonde wanasota.
 
Mfao mwingine Ni Raisi ZELENSKY kule ukraine,

Sahivi anaitekeleza nchi yake kwa kushupalia misimamo yake ya kuendelea na iyo Vita wkt ndo anazidi kuliangamiza taifa lake.

Anaitwa kwny mazungumzo anadengua,
Anazidi kujinadi anashinda adui ilhali uhalisia anachapika sana na nchi inazidi kua magofu.

Anachoogopa Ni aibu ya kuchutama aonekane alifanya maamuzi mabovu,

Kitu ambacho mtu alieflexible angeweza kuepusha maafa mengi zaidi.
 
FB_IMG_16472760595089928.jpg
 
Watu wa kaliba ya anayoongelea mtoa mada,

Huwa wanapata tabu kua na mafanikio endelevu ktk Yale wanayoyafanya hasa uko wanakoonesha Iyo misimamo yao isiyobadilika.

Iwe kwenye nyanya ya uchumi, kijamii, kisiasa, kimahusiano au kiafya.

Mf:
1. Uchumi- Angalia uchumi wa ZIMBABWE tangu uhuru kipind chote ROBERT MUGABE akiwa madarakani

2. Kisiasa- Angalia maisha ya Polepole na BASHIRU kisiasa, Kisha walinganishe na kina NAPE na MWIGULU.

3. Kijamii, - Angalia maisha ya wale wazee waliong'ang'ania vitu vya kizamani wkt teknolojia ishafika mbali.
Ukienda kwao utadhan nchi ndo imepata uhuru (pako old fashioned).
Kuna ladha fulan wanazimiss.

4. Kimuziki- muangalie Diamond platnuz alivyomwepesi wa kubadili a na mafanikio yake kimuziki na mlinganishe na wasanii wengine wakongwe aliowakuta kwny muziki na bado wako kwny muziki.

5. Kiafya- angalia maisha ya wale wasioamin katika Tiba za kisasa na kutumia Kinga kila tendo. Magonjwa ya zinaa hayawaishi ila bado wamo TU.

6. Kimahusiano,- angalia wanavyopata tabu kudumu kwny mahusiano yao,
-angalia wanavyoongoza trend ya kufanya kudhuru
-angalia wanavyoongoza kudhuru wenza au kujidhuru wenyewe pale wanaposalitiwa,
-angalia wanapata tabu kuelewa wanawake/wanaume Ni viumbe wa namna gani?

Yaan watu wa hivi huwa wanaishi kwa msongo mkubwa wa mawazo,
Pale Jambo lolote wanaloamini sana linapookwenda ndivyo sivyo.

Ni WAGUMU SANA KUTAKUBALI MABADILIKO, Na huu ndio udhaifu wao mkubwa[emoji4]
 
Nadhani Ni Hali ya ukomavu wa akili tu inayo sababishwa na changamoto ambazo tumezipitia, so inafika stage mtu unaona hakuna haja ya ku-pay attention na vitu ambavyo vinaweza kukuumiza au kuku potezea muda wako wakati kuna mengi ya kufanya

Life is so crazy mamaeeeee
 
Watu wa kaliba ya anayoongelea mtoa mada,

Huwa wanapata tabu kua na mafanikio endelevu ktk Yale wanayoyafanya hasa uko wanakoonesha Iyo misimamo yao isiyobadilika.

Iwe kwenye nyanya ya uchumi, kijamii, kisiasa, kimahusiano au kiafya.

Mf:
1. Uchumi- Angalia uchumi wa ZIMBABWE tangu uhuru kipind chote ROBERT MUGABE akiwa madarakani

2. Kisiasa- Angalia maisha ya Polepole na BASHIRU kisiasa, Kisha walinganishe na kina NAPE na MWIGULU.

3. Kijamii, - Angalia maisha ya wale wazee waliong'ang'ania vitu vya kizamani wkt teknolojia ishafika mbali.
Ukienda kwao utadhan nchi ndo imepata uhuru (pako old fashioned).
Kuna ladha fulan wanazimiss.

4. Kimuziki- muangalie Diamond platnuz alivyomwepesi wa kubadili a na mafanikio yake kimuziki na mlinganishe na wasanii wengine wakongwe aliowakuta kwny muziki na bado wako kwny muziki.

5. Kiafya- angalia maisha ya wale wasioamin katika Tiba za kisasa na kutumia Kinga kila tendo. Magonjwa ya zinaa hayawaishi ila bado wamo TU.

6. Kimahusiano,- angalia wanavyopata tabu kudumu kwny mahusiano yao,
-angalia wanavyoongoza trend ya kufanya kudhuru
-angalia wanavyoongoza kudhuru wenza au kujidhuru wenyewe pale wanaposalitiwa,
-angalia wanapata tabu kuelewa wanawake/wanaume Ni viumbe wa namna gani?

Yaan watu wa hivi huwa wanaishi kwa msongo mkubwa wa mawazo,
Pale Jambo lolote wanaloamini sana linapookwenda ndivyo sivyo.

Yaani
Ni WAGUMU SANA KUTAKUBALI MABADILIKO, Na huu ndio udhaifu wao mkubwa[emoji4]
 
Binadamu ni kiumbe cha ajabu sana,kila kundi la binadamu huongozwa na tabia tofauti tofauti,hebu chukulia huu mfano,hujawahi kuta kuna kijana ametoka familia ya kitajiri tu yenye uwezo na ana akili na tabia za wastani.

Au hujawahi ona mdada alikua na mahusiano kwenye ujana wake na wanaume wanaojilewa ila anaishia kua kahaba tu akiuza buku mbili au
Exactly niko hivo sirudii nikirudi sio kwa dhamira njema ujue narudi kuharibu kama grader.
 
Mfao mwingine Ni Raisi ZELENSKY kule ukraine,

Sahivi anaitekeleza nchi yake kwa kushupalia misimamo yake ya kuendelea na iyo Vita wkt ndo anazidi kuliangamiza taifa lake.

Anaitwa kwny mazungumzo anadengua,
Anazidi kujinadi anashinda adui ilhali uhalisia anachapika sana na nchi inazidi kua magofu.

Anachoogopa Ni aibu ya kuchutama aonekane alifanya maamuzi mabovu,

Kitu ambacho mtu alieflexible angeweza kuepusha maafa mengi zaidi.
Umeongea vizuri Sana mkuu,muda mwingine tunahitaji kufanya maamuzi Mara mbili ili tuepushe madhara fulani ambayo yanaweza kutukumba baadae.
 
Najiona mm 🥲yani mkuu kwenye kuanzisha mahusiano ndo nipo ivo nikiona mtu analeta mambo flani namkataa mazima sema hata mahusiano yenyewe nikipata hayadumu nayo
 
Huenda unatuandaa akina dada kisaikolojia kututokea.

Sasa ni mbinu ya kutokataliwa.

Ushindwe na ulegee mkuu. Hakukubali mtu hapa.

😁😁😁🤣🤣🤣🏃🏻‍♀️🏃🏻‍♀️🏃🏻‍♀️🏃🏻‍♀️
 
Back
Top Bottom