Saikolojia za wacheza kamari hutajirisha wenye makampuni ya kamari

Saikolojia za wacheza kamari hutajirisha wenye makampuni ya kamari

Apollo one spaceship

JF-Expert Member
Joined
Jan 28, 2021
Posts
245
Reaction score
457
∆ Aghalabu, mcheza kamari akishinda, huanza kucheza zaidi kwa pupa huku akipuuzia mbinu za kuepuka hasara.

∆ Mcheza kamari akishinda mara nyingi hujisifia kwa mbinu bora aliyotumia katika uchambuzi. Lakini akishindwa huweka lawama kwa kuzingatia madhaifu ya nje kama mchezaji kukosa penalty nk. Hii humfanya kucheza kamari nyingine kwa pupa.

∆ Kucheza kamari za watu wengine kwa kuamini ni za uhakika kisa watu wengine wanazinunua. Hii ni njia rahisi ya kupoteza kwani kila mtu huchambua kwa kukosea kutokana na mahaba na timu, mahaba na njia fulani hata kama haikidhi mechi husika nk.

∆ Mapenzi na timu fulani. Mfano, leo watu wengi watampa Man U moja kwa moja.

∆ Tamaa. Kushawawishiwa na kiasi kikubwa cha ushindi kwa kucheza kamari ambayo haina vigezo vya kwenda kama inavyotarajiwa. Japo inaweza kwenda sawa, ni jambo jema kuchambua kwa usahihi taarifa zilizopita.

∆ Kuto cash out hela inayoenda kuliwa yote, kwa kusubiria maajabu yatokee hata Kama vigezo vilivyopo havisapoti ushindi.
 
Uzi wako lengo lako lilikua kuisema Man-U itapigwa sio Betting..acha kufatilia Mambo ya watu we kama Betting ishakumaliza ni wewe kila Jini na Mbuyu wake.
 
Ndio maana bill gate alishawahi kusema kwamba utajiri unaanzia kwenye akili ndio maana hakuna mcheza kamari tajiri hata ashinde kiasi gani cha pesa atarudi tu kwenye umasikini.

Sent from my SM-N950F using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom