Saint Augusitine University ni Chuo cha Kibabaishaji

Mvaa Tai

JF-Expert Member
Joined
Aug 11, 2009
Posts
6,158
Reaction score
4,449
Nakichukulia kama ni chuo cha kibabaishaji kwasababu zifuatazo.

1.Hawako vizuri kwenye records keeping kwa mfano unaweza kurudishwa usiingie kwenye chumba cha mtihani kwasababu kumbukumbu zao zinaonyesha unadaiwa ada hata kama umelipa kila kitu, hivyo kumlazimu mwanafunzi kutembea na risti zake za ada ili kuepuka usumbufu.

2.Wanafanya kazi zao kama zima moto hivyo kupelekea kusababisha usumbufu kwa wateja, kwa mfano ni kawaida kabisa kusikia mwanafunzi alimaliza chuo lakini walisahau kumuweka kwenye orodha ya wahitimu hata kama hadaiwi kitu chochote.

3. Hawako systematic katika mambo yao, kwa mfano wahitimu wa MASTERS wa mwaka2011 na miaka ya nyuma walipata vyeti vyao ndani ya wiki moja ila wahitimu wa mwaka 2012 tulimaliza mwezi November mpaka sasa hatujapata vyeti vyetu tena bila kupewa sababu zozote za msingi japo kuna tetesi kwamba aliyekuwa anashughulikia vyeti yupo Maternity hivyo tutavipata mpaka akimaliza likizo yake ya uzazi, What a University? Jamani mnaozijua sheria tushaurini kama tunaweza kuwaburuza mahakamani kwa huu usumbufu.
 
Je katika case yako ya madai utaweza kuthibitisha umeathirika vipi na hiki chuo? If yes,then file a petition before the court of law
 
Je katika case yako ya madai utaweza kuthibitisha umeathirika vipi na hiki chuo? If yes,then file a petition before the court of law

Haya mambo yanahitaji ushauri wa kisheria na hohe hahe kama mimi ndiyo maana nimeishia kuandika na kuomba msaada hapa, nilimuuliza jamaa mmoja ni tutoria asistant pale akaniambia niwe mpole tu maana wao kama chuo hawana mkataba wowote na mimi wa kunipatia cheti changu kwa mda gani.
 

Mimi mwenyewe nimemaliza MBA pale mwezi November na nilitunukiwa kama kawaida ila mpaka sasa sijajua nini kinaendelea kwani kila nikienda chuo kuulizia wanajibu kwa kifupi kwamba vyeti bado na nikawashauri basi waweke tangazo linaloweka bayana ni lini vitatoka na kitu gani kimesababisha mpaka sasa hawajatoa ili kutupunguzia usumbufu sisi tunaotoka mikoa mingine kwa mfano mimi nilifunga safari toka Rukwa lakini nilijibiwa kirahisirahisi sana, kwa ufupi katika soma yangu sijawahi kukichukia chuo kama ninavyo kichukia Saint Augustin
 

Mimi nawasiliana na jamaa waliopo Dar maana ni wengi sana, siku moja tukutane maeneo ya mikocheni tuandamane hadi TCU tufikishe malalamiko yetu hiki chuo ni uzushi mtupu
 

Hamna chuo hapo
 
Kafungueni mashtaka mahakaman.
 

ulipokuwa unasoma hapo uliwaambia kuwa ni wababaishaji?
 
Mbona UDSM kuna watu walisomwa majina kupewa vyeti na wako 1st year? UDOM watu wamesomea education wanapewa vyeti vya political science? Ni matatizo ya vyuo vyote vya TZ
 
mkuu taarifa sahihi huanza na utafiti kwanza harafu hitimisho baadae, we ni mgeni nyumba hii but pole sana kwa hiko
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…