Imekuwa ni utamaduni wa kawaida kwa vilabu vya Mpira wa miguu Ulimwenguni kufanya usaliji (kununua Wachezaji) pindi madirisha ya usajili yanapofunguliwa.
Katika harakati hizo kuna baadhi ya Wachezaji ambao sajili zao huwa na mbwembwe nyingi na kuibua taharuki kwa Mashabiki lakini kwa bahati mbaya sajili hizo huenda tofauti na matarajio ya wengi.
Je, usajili wa mchezaji gani ambao uliibua taharuki kwako lakini ukawa tofauti na ulivyotarajia?