Sakafu/ Floor ya meli inaharibiwaje na mwamba(barafu)?

Sakafu/ Floor ya meli inaharibiwaje na mwamba(barafu)?

Sesten Zakazaka

JF-Expert Member
Joined
Sep 10, 2017
Posts
10,559
Reaction score
19,101
Wakuu kuna jambo moja hua najiuliza sana siku zote, kwamba tunaambiwa floor au sakafu ya meli imetengenezwa na pure iron (chuma cha pua). Sasa inakuaje meli ambazo hupata ajali ya kugonga mwamba baharini floor zake hupasuka au huchanika ilhali tunaambiwa hiyo miamba ni milima ya barafu iliyopo chini ya bahari

Naomba wajuzi wenye utaalam wa Marine Engineering wanisaidie kuelewa jambo hili hasa ukizingatia kuna meli kubwa kubwa zilizoundwa kwa ustadi wa hali ya juu kama vile Titanic zimewahi kuzama baada ya kukutana na zahma kama hii ya kugonga miamba baharini
 
Swali fikirishi.

Natarajia kuona maelezo yatakayo ambatana na physics ndani yake.
 
Ni kama tu vile maji ya tsunami yanavyo fagia majengo yaliyojengwa kwa zege na nondo nzito kwa muda wa sekunde chache kabisa. Wakati meli inapogonga hayo mapande ya barafu kuna force kubwa sana inayoigandamiza meli kiasi cha kuchana/ kupindisha vyuma au kuivunja kabisa meli
 
mkuu ukisikia barafu unajua ni kama zile tunanyonya afu uigonge na guta upate pancha haha ha ha barafu barafu kweli imeganda had ikagandika yani ukiipiga kwenz inalia ka chuma imeganda si kitoto fikiria ipo majin na haiyeyuki ukipima pale ina -150 degrees centigrade
 
Na mim nahitj majibu pia kwan naona wajuvi wa masuala ya kifizikia hawajafika
 
Meli imetengenezwa na sakafu ambayo inaitwa "keel" ambayo ni sawa na uti wa mgongo na ni sehemu ya kwanza katika uundaji wa meli.

Miamba ya barafu ambayo meli hugonga na kupasuka ni miamba migumu zaidi ya hayo material.

Pia meli kutokana na kujengwa kwa chuma hivyo vyuma husinyaa meli ikifika ukanda wa baridi hapa kumbuka physic chuma kikipata baridi husinyaa.
 
Kwa sasa ili kupunguza ajali maeneo ya barafu kuna meli ndogo ambazo hutangulia kuvunja barafu nazo hufaamika kama "Ice breakers" na kutengeneza njia kwa meli kubwa zinazoifuata kwa nyuma.

Pia kuna meli ambazo hutumia Bulbous Bow kupasua barafu inapopita maeneo yenye barafu.
 
Back
Top Bottom