kipara kipya
JF-Expert Member
- May 2, 2016
- 18,833
- 23,276
Mjadala unashika kasi na uliopo kwenye masikio ya watu ni kuhusu bandari yetu kuibinafsisha kwa wamanga wa dubai.
Mpaka muda huu kila mmoja anakuja na lake,ghafla bandari wakakurupuka kukanusha kuhusu hiyo habari bila kuweka vielelezo vya hayo wanayokanusha ,pili bandari unakanushaje nawe sio uliyeingia mkataba.
Hapa wa kujibu ni yule tunayemuona kwenye picha akisaini makaratasi na watu waliovaa vilemba na mahegali kichwani yaani serikali.
CCM mwenyekiti amehusika hebu njooni na fact mtutowe kwenye wasiwasi wananchi na huu uwongo mnaojaribu kuukanusha ili hali mwenyekiti na wabunge wanaujua na baadhi ya mawaziri.
Bila ya hivyo tutaamini haya yanayosemwa kuwa mmeuza bandari sijui mmeipangisha kwa muda usiojulikana huu ni wakati wa kuweka mambo hadharani kabla hali haijamuwia ngumu Raisi Mama Samia kwa wananchi waliomuamini katika kipindi hiki kifupi cha uongozi wake na kitafuta mazuri yote aliyofanya.
Wananchi watarudi kwenda kulia kaburini kwa hayati Magufuli aliyekuwa haiingii mikataba kwa siri huweka makamera ya vyombo vya habari.
Chama na serikali tokeni mliweke hili sawa na mtupe ukweli hapa hamkwepi lawama!
Uwongo usipokanushwa hugeuka ukweli!