Sakata la DP World: Kamati ya Bunge Yaahirisha Kupokea Maoni ya Marekebisho ya Sheria za Maliasili ikitaka Ufafanuzi wa Serikali

Sakata la DP World: Kamati ya Bunge Yaahirisha Kupokea Maoni ya Marekebisho ya Sheria za Maliasili ikitaka Ufafanuzi wa Serikali

Tuna rais wa hovyo sana awamu hii.yaani unaamua kubadili sheria ili zimpendeze huyo anayemwita mwekezaji wakati ni jambazi wa rasilimali.Na yeye hata kishtuka tu hamna.Hovyo sana.
TISS ndio wajinga sana tena sana hawafai. Huyu Rais alitakiwa kufanyia kitu kigumu sana hatuwezi kuacha maliasili zetu zichululiwe OUT CCM
 
Bunge la chama kimoja linajifanya kuwa sasa wapo makini baada ya wananchi kuliona bunge hili la mchongo la 2020 limewasaliti raia kwa kugawa mali za walipakodi bila kuwashirikisha wananchi.

Pia bunge kwenda hatua nyingine ya kuwadharau waTanzania ambapo tarehe 10 Juni 2023 kwa kishindo kubariki bandari zote kupewa milele DP World pamoja na miundo-mbinu yote ya Tanzania kama barabara kuu, bandari kavu zote, magodauni ya kampuni za kitanzania za usafiri za malori, container terminal bila kusahau SGR Reli.

Labda TAZARA tu ndiyo imepona kwa kuwa ni shirika la reli linalo milikiwa na nchi mbili za Tanzania na Zambia ama sivyo nayo ingegawiwa bure milele kwa visingizio vya kukosa ufanisi.
 
Sheria hii kaa la moto mikononi mwa wabunge wa chama kongwe dola CCM :

Sheria ya Mamlaka ya Nchi Kuhusiana na Umiliki wa Maliasili. The Natural Wealth and Resources (Permanent Sovereignity) Act, 2017


TOKA MAKTABA
:
Dodoma, Tanzania

3/02/2017 mjini Dodoma
Prof. Palamagamba Kabudi - Mswaada wa The Natural Wealth and Resources (Permanent Sovereignity) Act, 2017 na ibara ya 9 ya katiba


View: https://m.youtube.com/watch?v=31G4xOXY5Dw
inatamka kuwa madaraka ya wananchi, serikali kuwajibika kwa wananchi, kulinda maliasilia na mali inayomilikiwa kwa pamoja.

Bunge limeendelea leo tarehe 3/02/2017 mjini dodoma ambapo serikali imewasilisha mapendekezo ya muswada wa sheria ya mikataba ya maliasili za nchi. Muswada huo wa sheria hiyo unalitaka bunge kuweka utaratibu kikanuni utakaotumika wakati wa mapitio ya mikataba na makubaliano yanayoingiwa na serikali kwenye maliasili za nchi.

Waziri wa katiba na sheria, mhe. Prof. Palamagamba Kabudi ameuwasilisha kwa niaba ya serikali sheria hiyo inapendekeza kulipa bunge mamlaka ya kupitia mikataba ya umiliki wa maliasilia, madini, mafuta, pamoja na gesi.
 
Sasa tuanze kuunganidsha Doti

Mgao wa Dipwiwod
Abduli amepata wapi Fweza za kuunda kampuni ya Ummeme Sola mpaka kuweza kuuza Kwa Mu7 sio jambo dogo muwekezaji kupokelewa vile!!!
Tunapo elezwa wabwabwajaji tu wamelimbuka mpaka kutukoga Kwa kununua brand New Prado(masikini akipata matako uliza mbwata)

Mungu atawaumbua muda mfupi ujao

Ifuatiliwe hiyo kampuni ya Sola imeanza lini?
Wamiliki wake ninan?
Share zao
Mtaji wao
 
Aisee, hivi inakuwaje muwekezaji mmoja tuu anafanya mpaka tubadili sheria za nchi ambazo zilitungwa kwa umakini mkubwa? Hii sheria ya maliasili ni mpya kabisa ya mwaka 2017 tuu hapo, ni kwa nini tubadili sheria inayolinda maliasili kwa ajili muwekezaji mmoja tuu?

Ina maana akija muwekezaji mwingine ambaye sheria itakuwa inambana kwenye masharti anayoyataka pia tutairudisha tena bungeni kuvichomoa hivyo vipengele?

Huyu muwekezaji ana nini hasa cha zaidi mpaka anafanya sheria za nchi zinanyumbulishwa ili tu yeye a-fit in?

Kwa nini yeye kama muwekezaji asi-blend in na sheria za nchi yetu?

Kimsingi yeye ndiyo anapaswa ajinyumbue ili kuendana na sheria halali za nchi zilizowekwa.

★★★★★★★★★★★★★★★★★★★★★★★★★★

Kamati ya Bunge ya Katiba na Masuala ya Kisheria imeahirisha kusikiliza maoni ya wadau kuhusu mapendekezo ya marekebisho ya Sheria ya Mamlaka ya Nchi Kuhusiana na Umiliki wa Maliasili ya mwaka 2017 na Sheria ya Mapitio na Majadiliano Kuhusu Masharti Hasi Katika Maliasili ya nchi ya mwaka 2017.

Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Joseph Mhagama, ameiambia The Chanzo Alhamisi hii kwamba wameomba ufafanuzi zaidi kutoka kwa Serikali kuhusu mabadiliko hayo ambayo yameibua mjadala mkubwa miongoni mwa wafuatiliaji wa mambo nchini.

Sheria hizo ni miongoni mwa sheria zilizojumuishwa katika Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali Na. 2 wa Mwaka 2023, uliokusudia kurekebisha, pamoja na sheria nyingine, sheria hizo mbili ili zisitumike katika uendeshaji wa miradi ya uendeshaji, uendelezaji na bandari.

Huku wadau wengi wakihusisha sheria hii na mkataba unaotegemea kuipa kampuni ya DP World ya Dubai, kazi ya kuendesha, kuboresha na kuendeleza bandari Tanzania.

Muswada huo uliosomwa bungeni kwa mara ya kwanza Juni 28, 2023, na Kamati ya Bunge ya Katiba na Masuala ya Kisheria ilialika maoni ya wadau kuhusu marekebisho yaliyotazamiwa kabla ya muswada huo kurejeshwa bungeni baadaye Agosti. Kamati ilisikiliza maoni ya wadau hao mnamo Agosti 16, 2023.

Sehemu ya IV na V ya muswada wa marekebisho zinapendekeza marekebisho ya sheria tajwa ili kuhakikisha kuwa utekelezaji wa sheria hizo hauathiri uwekezaji utakaokuja kufanywa katika uendelezaji na uendeshaji wa bandari.

Serikali inasema marekebisho hayo yanalenga kuwezesha bandari za Tanzania “kufanya kazi katika viwango vya kimataifa na kuvutia meli nyingi za mizigo mikubwa kuhudumiwa na bandari” za Tanzania.

Sheria hizi mbili ambazo zilipitishwa mwaka 2017 ziliwekwa kwa madhumuni ya kuhakikisha Tanzania inanufaika na maliasili zake, lakini pia inatoa nafasi ya kurekebisha mikataba mibovu.

Dk Mhagama ameiambia The Chanzo kwamba kamati yake ilipokea maoni kuhusu sehemu nne za sheria ambazo Serikali inataka kuzifanyia marekebisho, na kuacha sehemu mbili zilizoundwa ili kuipa Tanzania mamlaka juu ya maliasili zake.

“Muswada huo una sehemu sita, kamati iliona ifanyie kazi vipengele vinne tu, na kuviacha vingine viwili ili kutengeneza njia ya mashauriano na Serikali kwa lengo la kupata ufafanuzi wa maudhui ya sheria hizo mbili,” Mhagama, ambaye ni mbunge wa Madaba (Chama cha Mapinduzi – CCM), anasema.

Anasema kuwa wadau wataalikwa kuwasilisha maoni yao mara baada ya kupata ufafanuzi na Serikali pindi ikiamua kuendelea na marekebisho yaliyopendekezwa na kuongeza kuwa kamati hiyo inatakiwa “kujiridhisha” na yaliyomo kwenye muswada huo kabla ya kuamua kuendelea nao.

Dk Mhagama ameiambia The Chanzo kwamba kamati yake iliomba maelezo kutoka kwa Serikali kuhusu marekebisho ya sheria hizo mbili, huku akishindwa kueleza ni lini hasa anatarajia mamlaka kujibu hoja zilizoibuliwa.

“Serikali itakuwa hapa milele; wakati wowote watakapoona inafaa kujibu hoja tulizoibua watakuja kwenye kamati na mapendekezo yao,” Dk Mhagama anafafanua. “Si lazima iwe leo, kesho au mwakani.”

Mapendekezo ya marekebisho ya sheria hizo yanakuja wakati mjadala mkubwa wa kitaifa ukiendelea kuhusu makubaliano baina ya Serikali ya Tanzania na Dubai ili kuiruhusu DP World kuiendesha bandari ya Dar es Salaam.

Mnamo Juni 10, 2023, wabunge waliridhia kwa kauli moja mkataba huo tata ambao unaendelea kuleta mgawanyiko wa taifa, huku mgawanyiko wa maoni kati ya wafuasi wake na wakosoaji ukionekana wazi kila siku.

Serikali na chama tawala wanauelezea mkataba huo kuwa “mkataba bora zaidi kuwahi kutokea,” huku wanaharakati na vyama vya upinzani wakiuelezea kuwa “mkataba mbaya zaidi.”

Miongoni mwa waliokataa mpango huo ni Maaskofu wa Kanisa Katoliki, ambao kwenye taarifa yao ya pamoja ya Agosti 18, 2023, waliitaka Serikali kusikiliza matakwa ya wananachi ya kufuta mpango huo, wakisema, “Sauti ya watu ni sauti ya Mungu.”

“Ni lazima miradi kama hii [ya maendeleo ya bandari] iendeshwe na kusimamiwa na Watanzania wenyewe, huku wakikaribisha ushirikiano ambao wao wenyewe wataudhibiti,” Maaskofu hao 37 walisema katika taarifa yao hiyo ya pamoja.

“Hili ndilo ambalo wananchi wamekuwa wakililia ili tuweze kuboresha uwezo wetu wa kusimamia uwekezaji muhimu,” waliendelea kueleza. “Kwa sababu tayari tumeshachambua mapungufu ya jinsi tunavyoendesha bandari zetu, tunaweza kuyafanyia kazi huku njia za uchumi zikisalia mikononi mwetu.”

Source: The Chanzo
Huu muswada aliuleta Magu,

Ni kama alijua kitachoenda Kutokea akapiga pin!!

Kweli Tunakumbuka Magu🙏🙏
 
Kwa msimamo huu mpya wa bunge kuchelewesha au kupinga muswada wa sheria kubadilishwa maalum kwa ajili ya kuipendelea DP World, nalo(bunge) litashutumiwa na kugawiwa upande unaoegemea.
 
IGA is just a framework aina lolote la maana, mziki upo kwenye ‘concession agreements/project agreements.

Kama serikali ingekuwa imepeleka watu sahihi kusoma maswala ya business contracts. Wenye background ya finance, business management au accountancy: IGA si lolote si chochote zaidi ya watanzania kujazana ujinga tu.

Ukisoma mambo ya mikataba ya kimataifa na kuelewa historia yake (to get the background/perspective) ya kuanzishwa kwa taratibu za BIT na aina ya tabia za watu walio influence hiyo mikataba.

Inabidi tu rudi kuanzia na watu kans hakina ‘John Rockefeller’ senior na biashara yake ya utapeli wa ‘snake oil’ marekani, kuelewa history ya biashara ya mafuta from Texas first rigs, people who funded first explorations, finding early usages of the commodity, msingi wa capitalism ya US (trust me it’s unique to date compare to many other western nations), how ‘John Rockefeller Jr’ adopted his father’s canny business skills as well as his own ruthless approach to capitalism ya awali US (which is still somewhat the predominantly thinking in US), kuanzishwa kwa ‘standard oil’, it’s ill practices to be a monopoly in US market.

Overall immoral practices of other investors on the era which are beyond today acceptable today, fraudulent activities of the so called money men businesses models in sifting government coffers, baadae makampuni ya mabeberu kutafuta new source za mafuta global nje ya US hadi kuundwa kwa (seven sisters), ushindani hayo makampuni kupata new source za mafuta duniani, investment agreement walizoingia nazo na waarabu, uelewa wa matumizi ya mafuta kwa sababu mbali mbali za uchumi duniani, uelewa wa umuhimu wa kumiliki mafuta duniani, waarabu na wengineo wenye mafuta kutaka kufaidika na resources zao, kasheshe ya wenye nchi kupambana kuchukua maliasili zao walizogawa karibu bure kwa kuingia mikataba mibovu, sababu za mabeberu kuja na ideology za divide and rule, sababu za UN kutoa definition ya nani mmiliki wa maliasili za nchi, sababu za kutunga aina ya mikataba ya kimataifa PSA/concession agreements (etc), wawekezaji wa nje kutaka kuona stabilisation clause zinakuwa sehemu ya framework za negotiations (that’s pretty much BITS and IGA) kuwa sehemu ya contract terms na kuheshimika.

Ukielewa mambo yote hayo na kujua msingi wa stabilisation clauses IGA sio lolote si chochote that’s just a norm today in investment protection. Nitty Gritty zipo kwenye ‘concession agreements’ ndio maana hiyo mikataba wanataka iwe siri popote duniani.

Hizo sheria za 2017 hazibadilishwi kwa sababu ya IGA (ni viazi tu kama hakina Mwabukusi wenye uelewa mdogo kudhani ile ni big deal) hiko cha mtoto tu if anything waarabu wana good intentions.

Kama umeelewa strategically kwa kusoma phase I & II DPW wanalenga nini impact yake it’s a game changer kwa uchumi wa bandari. Issue labda ni quality ya negotiators tutakaopeleka kujadili ‘concession agreements’ make no mistake that’s where unahitaji wataalamu wa finance, MBA au accountancy or else utaumia sana; sasa hiyo aitakuwa sababu ya IGA ni framework mbaya ila ni upuuzi wetu wenyewe kwenye kupeleka watu wasio na uelewa mdogo wa maswala ya finance.

Sababu hasa za kubadili hizo sheria za 2017 ni LNG plant ambapo mkataba inabidi uende bungeni. Ni hivi $42 billion LNG plant hiyo itakuwa the second most expensive plant in the world. Maana yake nini jamaa wana data ambazo sisi hatuna.

Tanzania ina 500,000 sq km ya potential area of ‘oil and gas’ reserves mpaka sasa only 100,000 km sq has been explored; from that there is enough reserve to recoup $42 billion investment. However utaminywa kweli in the period hili hiyo hela irudi.

Trust me wasingeweka hela hiyo for 50 cubic million of gas, faida yao ingekuwa ndogo sana. Wameshaona potential za mbele kubwa mno katika maeneo ambayo hayajaguswa so they can justify that investment na malipo ya mbeleni. Vinginevyo $42 billion investment ni gharama za plant ambazo hazilipi kabisa kwetu unless kama unasikiliza uthenge wa Zitto na Makamba na hiyo ndio sababu kuu ya kubadili hiyo sheria ili mkataba wa PSA tulioingia usiende bungeni; kuna madudu wazungu ambayo wataki public ujue that’s to say the nation is fu*cked.
 
Aisee, hivi inakuwaje muwekezaji mmoja tuu anafanya mpaka tubadili sheria za nchi ambazo zilitungwa kwa umakini mkubwa? Hii sheria ya maliasili ni mpya kabisa ya mwaka 2017 tuu hapo, ni kwa nini tubadili sheria inayolinda maliasili kwa

Source: The Chanzo
Shukrani ziwaendee TEC. WALE WA ASKOFU SHOO endeleeni na UKIMYA .
 
Aisee, hivi inakuwaje muwekezaji mmoja tuu anafanya mpaka tubadili sheria za nchi ambazo zilitungwa kwa umakini mkubwa? Hii sheria ya maliasili ni mpya kabisa ya mwaka 2017 tuu hapo, ni kwa nini tubadili sheria inayolinda maliasili kwa ajili muwekezaji mmoja tuu?



Source: The Chanzo
Msichanganye SIASA na DINI
 
IGA is just a framework aina lolote la maana, mziki upo kwenye ‘concession agreements/project agreements.

Kama serikali ingekuwa imepeleka watu sahihi kusoma maswala ya business contracts. Wenye background ya finance, buni. Plant ambayo haulipi kabisa kwetu unless kama unasikiliza uthenge wa Zitto na Makamba na hiyo ndio sababu kuu ya kubadili hiyo sheria ili mkataba wa PSA tulioingia usiende bungeni; the nation is fu*cked.
Noted
 
Aisee, hivi inakuwaje muwekezaji mmoja tuu anafanya mpaka tubadili sheria za nchi ambazo zilitungwa kwa umakini mkubwa? Hii sheria ya maliasili ni mpya kabisa ya mwaka 2017 tuu hapo, ni kwa nini tubadili sheria inayolinda maliasili kwa a

Source: The Chanzo
Wafanye wafanyavyo hao wote wasirudi bungeni 2025
 
IGA is just a framework aina lolote la maana, mziki upo kwenye ‘concession agreements/project agreements.

Kama serikali ingekuwa imepeleka watu sahihi kusoma maswala ya business contracts. Wenye background ya finance, businabu kuu ya kubadili hiyo sheria ili mkataba wa PSA tulioingia usiende bungeni; the nation is fu*cked.
Illegible scrawl
 
Illegible scrawl
I can live with that and I am not offended with the comment. Its the reason I stated in my post to understand where I coming from it requires a background knowledge on the evolution of international contract frameworks (BITS/IGA).

Laws are established either as a result of society morals viewpoints, past experience or for functional purposes (administration purposes).

Bearing in mind the technical aspects of my post is doesn’t surprise me if it comes across as a scrawl to others but for those with appropriate background to how VCLT 1969 came about it makes a lot of sense.

Trust me the whole thing began with the ‘snake oil’, how it influenced ‘standard oil’ business model and its implications on global business (those were the first global FDY’s).
 
I can live with that, it’s the reason I stated in my post to understand where I coming from it requires a background on the evolution of international contract framework.

Laws are either a result of morals, experience or functional purposes (administration purposes).

It’s the reason the post might come across as a scrawl to others but for those with appropriate background on international up to VCLT 1969 it makes a lot of sense.
More illegible scrawls
 
Bunge ni la ovyo

Legalese na dhaifu

Ova
 
Back
Top Bottom