Sakata la DP World: Kamati ya Bunge Yaahirisha Kupokea Maoni ya Marekebisho ya Sheria za Maliasili ikitaka Ufafanuzi wa Serikali

ujui kitu mkuu, hujui financing business, hujui kabisa, huwezi kubadili domestic laws to accomodate international law, that is the highest degree of stupidity, so stupid, only a mind lamed person can do such stupidity.
Aliekwambia hiyo ni finance nani. Mimi naongelea sheria na vipengele vya mikataba ya kimataifa.

Embu ingia google tafuta academic papers/vitabu vya ‘stabilisation clauses’ uelewe zinahusu nini, umuhimu wake kwenye mikataba na background yake kwanini watu wakafikiria kuweka hizo clauses.

Hizo sheria za kimataifa zina lengo la kutengeneza implied terms za contract. wakati sheria za mwaka 2017 waliondaa mambo ya biashara za kimataifa inaonekana yanawapiga chenga.

Hakuna shortcut ya kupambana na watu dunia ya leo zaidi yakupeleka kunoa watu wako na wewe.
 
tulia hujui kitu, hakuna msomi mwenye akili akakupa reference ya google, hata mashuleni kwenye reseach ukiweka google unaliwa kichwa, kiufupi hujui kitu na wewe ni mjinga na migoogle yako. siitaji hata kuargue na wewe. mnaelekezwa na wanasheria mnaacha mnathanimini siasa. eti kagoogle ujinga mtupu. mshauza nchi kwa mikataba ya ovyo, unadhani kila mtu mjinga?
 
Walio tunga ni hao hao na ndo wanao badilisha sasa matatizo yako wapi,? kuna kujiumiza stress za kujitakia kwani kubadili vifungu vya sheria ni kinyume na katiba? yetu, hiyo ndo mara ya kwanza, muhimu wa fuata taratibu zote.......ndo mjue umuhimu wakupiga kura za bunge sahihi sio kulia lia hapa wakati sheria haijavunjwa hayo ndo matunda ya wa bunge wetu.
Huna unachojua zaidi ya uchawa
 
Mimi nadhani tumekosa mwelekeo,nakubaliana na Zito Kabwe ebu tutumie njia ya partnership kwenye uwekezaji huu kila upande uwe mbia,hiyo itaondoa kelele na nchi kunufaika na kujenga uwezo. hili hata Pengo alilidokeza. Lakini pia ni suala la sera ya PPP.
Zito muhuni yule
 
tulia hujui kitu, hakuna msomi mwenye akili akakupa reference ya google, hata mashuleni kwenye reseach ukiweka google unaliwa kichwa, kiufupi hujui kitu na wewe ni mjinga na migoogle yako. siitaji hata kuargue na wewe. mnaelekezwa na wanasheria mnaacha mnathanimini siasa. eti kagoogle ujinga mtupu. mshauza nchi kwa mikataba ya ovyo, unadhani kila mtu mjinga?
Wewe hata dunia ya leo hujui ilipo kielimu wala wanafunzi wengi wanatoa wapi research material.

Hakuna mtu mwenye akili timamu anasoma likitabu au sijui kutafuta journal katika first draft ya academic writing. Hata primary research ya Phd chapter 1 and 2 mradi Unafahamu concept/theory na angle yako ya research work.

Google inakupa article, web page (ata journals no one has time for those at first draft) muhimu ni kuelewa tu credentials za mwandishi kama ni news article na web page kama wana authority ya kuandika kuhusu hiyo sector.

Ukishaandika makolokolo yako unaingia electronic library ya chuo kutafuta journal sahihi na hiyo ni kazi rahisi sana kama umeshawahi kutumia hizo library. Kwanza unaanda search criteria, ukimaliza hapo type ‘Boolean search’ inakupa journal zenye concept zile zile kama mia (pick your poison inayofanana na ulichoandika).

If you are lazy like most students are these days na huko library unachukua majina na mwaka for in-text referencing only; ukimaliza huko unarudi ‘google reference’ uki-type same author/s name ya in-text na mwaka wa jarida, voila google washakuandikia reference chagua wewe sasa unataka APA, Havard or whatever ni copy and paste tu.

Hakuna mtu mwenye akili timamu anaandika academic papers kama enzi za Tanzagiza wakati unasoma.

Hiyo ilikuwa kukupa elimu tu jinsi google alivyokuwa mkombozi kwa wanafunzi leo. Ningeshakwita poyoyo at this point, ila inaonekana age yako imeenda ufahamu mambo yanavyofanyika leo.

Hata hao lectures wenyewe baadhi yao siku hizi wanaokota lectures zao google. Chezea google.

Now back to my post sijakwambia uende google tu nimekueleza ukifika huko tafuta academic journals au vitabu vinaovyoelezea umihimu wa stabilisation clause kwenye mikataba ya kimataifa, soma background ya hizo clauses (migogoro ya uwekezaji iliyosababisha watu kufikiria hizo clauses) uelewe kwanini hayo mambo ni muhimu kwenye FDI. Kitu ambacho sheria za 2017 imetoa hizo clauses hasa zile muhimu. Sasa hakuna mwekezaji wa muda mrefu ataingia mkataba bila ya hizo clauses for security reasons zake.
 
Hivi kwani badtola haziuzwi sokoni kama nyanya????ningeonesha mfano kwa mbunge wa jimbo langu ili liwe fundisho kwa majimbo mengine
 
Zito muhuni yule
Kwo mama ndo mtakatifu????yaani mkuu mwanao hata akiwa kibaka haina maana kila jambo atakalotenda litakuwa baya kumbuka hata saa mbovu kuna mda inaongea ukweli
 
Mbunge mmoja wa CCM ameonekana Vatican akisalimiana na Papa wa Kanisa Katoliki la Roma,ni wazi kapeleka ujumbe kwa Papa wa Kanisa Katoliki la Roma kufuatia Maaskofu wa Kanisa Katoliki la Roma Tanzania kupinga mkataba wa kuiuza bandari ya Dar es Salaam,na nguvu hiyo tayari Serikali imesitisha kukusanya maoni ya kuibadili sheria ya kulinda maliasili za Tanzania inayoitaka kesi ya Maliasili za Tanzania kusikilizwa hapa hapa Tanzania.
 
Aisee, hivi inakuwaje muwekezaji mmoja tuu anafanya mpaka tubadili sheria za nchi ambazo zilitungwa kwa umakini mkubwa? Hii sheria ya maliasili ni mpya kabisa ya mwaka 2017 tuu hapo, ni kwa nini tubadili sheria inayolinda maliasili kwa ajili muwekezaji mmoja tuu?

Ina maana akija muwekezaji mwingine ambaye sheria itakuwa inambana kwenye masharti anayoyataka pia tutairudisha tena bungeni kuvichomoa hivyo vipengele?

Huyu muwekezaji ana nini hasa cha zaidi mpaka anafanya sheria za nchi zinanyumbulishwa ili tu yeye a-fit in?

Kwa nini yeye kama muwekezaji asi-blend in na sheria za nchi yetu?

Kimsingi yeye ndiyo anapaswa ajinyumbue ili kuendana na sheria halali za nchi zilizowekwa.

★★★★★★★★★★★★★★★★★★★★★★★★★★

Kamati ya Bunge ya Katiba na Masuala ya Kisheria imeahirisha kusikiliza maoni ya wadau kuhusu mapendekezo ya marekebisho ya Sheria ya Mamlaka ya Nchi Kuhusiana na Umiliki wa Maliasili ya mwaka 2017 na Sheria ya Mapitio na Majadiliano Kuhusu Masharti Hasi Katika Maliasili ya nchi ya mwaka 2017.

Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Joseph Mhagama, ameiambia The Chanzo Alhamisi hii kwamba wameomba ufafanuzi zaidi kutoka kwa Serikali kuhusu mabadiliko hayo ambayo yameibua mjadala mkubwa miongoni mwa wafuatiliaji wa mambo nchini.

Sheria hizo ni miongoni mwa sheria zilizojumuishwa katika Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali Na. 2 wa Mwaka 2023, uliokusudia kurekebisha, pamoja na sheria nyingine, sheria hizo mbili ili zisitumike katika uendeshaji wa miradi ya uendeshaji, uendelezaji na bandari.

Huku wadau wengi wakihusisha sheria hii na mkataba unaotegemea kuipa kampuni ya DP World ya Dubai, kazi ya kuendesha, kuboresha na kuendeleza bandari Tanzania.

Muswada huo uliosomwa bungeni kwa mara ya kwanza Juni 28, 2023, na Kamati ya Bunge ya Katiba na Masuala ya Kisheria ilialika maoni ya wadau kuhusu marekebisho yaliyotazamiwa kabla ya muswada huo kurejeshwa bungeni baadaye Agosti. Kamati ilisikiliza maoni ya wadau hao mnamo Agosti 16, 2023.

Sehemu ya IV na V ya muswada wa marekebisho zinapendekeza marekebisho ya sheria tajwa ili kuhakikisha kuwa utekelezaji wa sheria hizo hauathiri uwekezaji utakaokuja kufanywa katika uendelezaji na uendeshaji wa bandari.

Serikali inasema marekebisho hayo yanalenga kuwezesha bandari za Tanzania “kufanya kazi katika viwango vya kimataifa na kuvutia meli nyingi za mizigo mikubwa kuhudumiwa na bandari” za Tanzania.

Sheria hizi mbili ambazo zilipitishwa mwaka 2017 ziliwekwa kwa madhumuni ya kuhakikisha Tanzania inanufaika na maliasili zake, lakini pia inatoa nafasi ya kurekebisha mikataba mibovu.

Dk Mhagama ameiambia The Chanzo kwamba kamati yake ilipokea maoni kuhusu sehemu nne za sheria ambazo Serikali inataka kuzifanyia marekebisho, na kuacha sehemu mbili zilizoundwa ili kuipa Tanzania mamlaka juu ya maliasili zake.

“Muswada huo una sehemu sita, kamati iliona ifanyie kazi vipengele vinne tu, na kuviacha vingine viwili ili kutengeneza njia ya mashauriano na Serikali kwa lengo la kupata ufafanuzi wa maudhui ya sheria hizo mbili,” Mhagama, ambaye ni mbunge wa Madaba (Chama cha Mapinduzi – CCM), anasema.

Anasema kuwa wadau wataalikwa kuwasilisha maoni yao mara baada ya kupata ufafanuzi na Serikali pindi ikiamua kuendelea na marekebisho yaliyopendekezwa na kuongeza kuwa kamati hiyo inatakiwa “kujiridhisha” na yaliyomo kwenye muswada huo kabla ya kuamua kuendelea nao.

Dk Mhagama ameiambia The Chanzo kwamba kamati yake iliomba maelezo kutoka kwa Serikali kuhusu marekebisho ya sheria hizo mbili, huku akishindwa kueleza ni lini hasa anatarajia mamlaka kujibu hoja zilizoibuliwa.

“Serikali itakuwa hapa milele; wakati wowote watakapoona inafaa kujibu hoja tulizoibua watakuja kwenye kamati na mapendekezo yao,” Dk Mhagama anafafanua. “Si lazima iwe leo, kesho au mwakani.”

Mapendekezo ya marekebisho ya sheria hizo yanakuja wakati mjadala mkubwa wa kitaifa ukiendelea kuhusu makubaliano baina ya Serikali ya Tanzania na Dubai ili kuiruhusu DP World kuiendesha bandari ya Dar es Salaam.

Mnamo Juni 10, 2023, wabunge waliridhia kwa kauli moja mkataba huo tata ambao unaendelea kuleta mgawanyiko wa taifa, huku mgawanyiko wa maoni kati ya wafuasi wake na wakosoaji ukionekana wazi kila siku.

Serikali na chama tawala wanauelezea mkataba huo kuwa “mkataba bora zaidi kuwahi kutokea,” huku wanaharakati na vyama vya upinzani wakiuelezea kuwa “mkataba mbaya zaidi.”

Miongoni mwa waliokataa mpango huo ni Maaskofu wa Kanisa Katoliki, ambao kwenye taarifa yao ya pamoja ya Agosti 18, 2023, waliitaka Serikali kusikiliza matakwa ya wananachi ya kufuta mpango huo, wakisema, “Sauti ya watu ni sauti ya Mungu.”

“Ni lazima miradi kama hii [ya maendeleo ya bandari] iendeshwe na kusimamiwa na Watanzania wenyewe, huku wakikaribisha ushirikiano ambao wao wenyewe wataudhibiti,” Maaskofu hao 37 walisema katika taarifa yao hiyo ya pamoja.

“Hili ndilo ambalo wananchi wamekuwa wakililia ili tuweze kuboresha uwezo wetu wa kusimamia uwekezaji muhimu,” waliendelea kueleza. “Kwa sababu tayari tumeshachambua mapungufu ya jinsi tunavyoendesha bandari zetu, tunaweza kuyafanyia kazi huku njia za uchumi zikisalia mikononi mwetu.”

Source: The Chanzo
Bahasha yake ni nzito sana... Ushi humo mkuu!!
 
Bandari na viwanja vya ndege ni milango ya kuingia na kutokea nchini, ni vyanzo vya mapato, huwezi kuviweka kundi moja la maliasili za nchi.

Pale bandarini kipi utakiweka katika kundi la maliasili?. ni yale maji?, ni zile mashine za kushusha na kupakia mizigo?.

Pia bandari inaweza kuongezwa ukubwa au kupunguzwa au kujengwa mpya kabisa kulingana na muda husika, tofauti na rasilimali halisi za nchi ambazo siku zote zinabakia kuwa ni hizo hizo.
 
Back
Top Bottom